Albert Msando
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 1,019
- 171
Nawasalim WanaCUF,
Bila kung'ata wala kumung'unya maneno ninyi ni wanafiki. Wanafiki sana.
Kwa nini nawashutumu? Kwa sababu tabia ya unafiki haijifichi. Hata kama wengine wote hawaioni ila mwenye tabia anajua kwamba anachofanya ni unafiki.
Mnawashutumu CDM kwamba ni kikwazo cha upinzani. Mnasema CDM wanadharau maamuzi ya ya wazanzibari kuhusu serikali ya umoja wa kitaifa.
Mara mnakurupuka na kusema mnaenda kuwashtaki CCM kwa wananchi. Wananchi wapi? Watanzania Bara peke yake au pamoja na Visiwani?
Hayo mnayoenda kuwashtakia kwa wananchi, i.e. Malipo ya dowans, bei za bidhaa, mgawo wa umeme, nk wananchi wanaishi nayo. Wanayajua. Pia CDM wameshawaambia.
Lakini, kama CCM ndio chanzo, ni huku Bara peke yake? CCM wameshindwa Bara peke yake? Visiwani mnamshtaki nani?
Hapa ndipo unafiki unapokuwa wazi. Hakuna asiyeuona unafiki wenu. Visiwani ninyi ni serikali. Matatizo ya wananchi mnatakiwa kuyatatua kama serikali. Hicho ndicho mlichokubaliana na CCM.
Huku Bara ninyi ni upinzani mkishirikiana na TLP, NCCR na UDP. Mnapinga au kukosoa wanayofanya CCM. Mnajidai kutokuona tatizo hapo. Hata kama muungano una matatizo hii nchi bado ni moja. Hatuna serikali tatu.
Tuna serikali mbili. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inawakilishwa kwenye Serikali ya Jamhuri. Kwa hiyo mpo kwenye Serikali.
Je mnataka tuamini mnaenda kujishtaki au hamna uwezo wa kuleta mabadiliko mkiwa ndani ya serikali yenu? Mnataka kuwa serikali na upinzani kwa pamoja?
Huwezi kula keki yako na kubaki nayo; you can not eat your cake and have it.
CUF, you have made a political mistake and error. Rectify it. The train is moving. Acheni kuwa wanafiki. It will push this country further down the abyss.