CUF Taasisi iwe makini na hujuma za mwisho kuelekea hukumu ya tarehe 22 Februari, 2019

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,224
3,290
Huo ndio ujumbe wa leo. Kwanza kutokana na hukumu ya jana tarehe 18 Februari, 2019 kuhusu UHALALI WA BODI YA LIPUMBA na namna maamuzi yalivyofanywa bado inaonesha kuna kiwingu ama mitego mingi ambayo imewekwa na pengine inaweza kutumiwa kama fursa ya kukwamisha baadhi ya mambo mengine ikiwemo kesi ya Uhalali wa mwenyekiti Lipumba.

Jee ni kweli bila shaka yoyote kuwa bodi ya zamani ndio inayotambulika kisheria ?

Viongozi hawapaswi kubweteka kwa maamuzi ya jana ambayo akina sisi tusiokuwa wanasheria bado hatujapata grounds za maamuzi zaidi ya kuona kuwa labda kuna mitego tu hasa kwa kuzingatia TAARIFA ZA SIRI ZILIZOVUJA KUHUSU NJAMA ZA JAJI MUTUNGI , VIONGOZI WA SERIKALI NA HAKIMU kuhusishwa na rushwa ili kesi iamuliwe visivyo. Jee bado kuko salama ?

Kunahitajika umakini kuhusu kutumiwa mwanya wa hujuma ili kesi iliyopo isisomwe ama kusogezwa mbele na mambo mengine kama hayo. Kwa mfano jee upande ulioshindwa kesi ya USAJILI WA RITA hawawezi kukata rufaa na kuchelewesha maamuzi ya kesi ya tarehe 22 Februari, 2019 ? Nini mnapaswa kufanya kisheria kabla ya hujuma kuanza ? yote hayo yazingatiwe.


Jee kwa maamuzi ya jana hayatoi nafasi za kiufundi kwa kesi ya tarehe 22, kukosa mashiko ya maamuzi na kisheria na hivyo LIpumba kupata fursa ya kufanya hujuma zaidi kwa kushirikiana na wadhamini wao ? Na jee huo sio mpango wa kuhujumu kesi ya Msingi ya UENYEKITI WA LIPUMBA AMBAO KAMA IKITOKEA ITAKUWA UMEPANGWA NA JAJI ?



Vyovyote iwavyo, Bado kunahitajika umakini zaidi maana ni wazi waliomtuma Lipumba walikusudia lao kwenye hili sakata la Mgogoro wa kupandikizwa.



Kishada
 
Huo ndio ujumbe wa leo. Kwanza kutokana na hukumu ya jana tarehe 18 Februari, 2019 kuhusu UHALALI WA BODI YA LIPUMBA na namna maamuzi yalivyofanywa bado inaonesha kuna kiwingu ama mitego mingi ambayo imewekwa na pengine inaweza kutumiwa kama fursa ya kukwamisha baadhi ya mambo mengine ikiwemo kesi ya Uhalali wa mwenyekiti Lipumba.

Jee ni kweli bila shaka yoyote kuwa bodi ya zamani ndio inayotambulika kisheria ?

Viongozi hawapaswi kubweteka kwa maamuzi ya jana ambao akina sisi tusiokuwa wanasheria bado hatujapata grounds za maamuzi zaidi ya kuona kuwa labda kuna mitego tu hasa kwa kuzingatia TAARIFA ZA SIRI ZILIZOVUJA KUHUSU NJAMA ZA JAJI MUTUNGI , VIONGOZI WA SERIKALI NA HAKIMU kuhusishwa na rushwa ili kesi iamuliwe visivyo. Jee bado kuko salama ?

Kuinahitajika umakini kuhusu kutumiwa mwanya wa hujuma ili kesi iliyopo isisomwe ama kusogezwa mbele na mambo mengine kama hayo. Kwa mfano jee upande ulioshindwa kesi ya USAJILI WA RITA hawawezi kukata rufaa na kuchelewesha maamuzi ya kesi ya tarehe 22 Februari, 2019 ? Nini mnapaswa kufanya kisheria kabla ya hujuma kuanza ? yote hayo yazingatiwe.


Jee kwa maamuzi ya jana hayatoi nafasi za kiufundi kwa kesi ya tarehe 22, kukosa mashiko ya maamuzi na kisheria na hivyo LIpumba kupata fursa ya kufanya hujuma zaidi kwa kushirikiana na wadhamini wao ?



Vyovyote iwavyo, Bado kunahitajika umakini zaidi maana ni wazi waliomtuma Lipumba walikusudia lao kwenye hili sakata la Mgogoro wa kupandikizwa.



Kishada
Subiri tarehe 22 mahakama itatenda haki kama ilivyotenda Jana kwenye maamuzi.Ondoa Shaka.Stay tuned
 
Subiri tarehe 22 mahakama itatenda haki kama ilivyotenda Jana kwenye maamuzi.Ondoa Shaka.Stay tuned
Mkuu kauli yako ina utata. Inawezekana unajuwa kinachoendelea. Jee ile ya jana sio danganya toto ili kupata fursa ya kuimaliza Taasisi pale maamuzi yakifanywa ioinekane mahakama iko fair? hasa ikizingatiwa SHUTUMA ZA HUJUMA NA RUSHWA HAZIJAKANUSHWA ?
 
Jambo moja liko wazi kuhusu kuhusishwa viongozi waandamizi wa SMZ na SMT kwenye hujuma na rushwa kwa Jaji. Kuelekea uchaguzi wa 2015 mmoja wa waliohusishwa na Rushwa kwenye maamuzi ya kesi hizi za CUF kutoka Serikalini(Zanzibar) alinukuliwa akisema wanakusudia kuifuta CUF kwenye ramani baada ya uchaguzi wa 2015.

Leo hii kuelekea kwenye maamuzi muhimu anatajwa tena kwenye taarifa za siri.

CUF kuweni makini.
 
Kwa mujibu wa vyanzo vyengine, inaarifiwa kwamba kwa upande wa Zanzibar, hali inaonesha viongozi mbali mbali wa CCM na serikali hawakufurahi juu ya kilichoendelea mahakamni jana.

Aidha tokea kumaliza uchaguzi wa 2015 na ule wa marudio , inaarifiwa kwamba CCM na viongozi wao Zanzibar wamekosa furaha na AMANI zaidi ikilinganishwa na awamu zote zilizopta licha ya vurumai kama hizi kujirudia kila baada ya uchaguzi.
 
Ile hukumu ya jana inawezekana ikawa ni njia ya kuhalalisha hukumu itakayofuata, vyovyote iwavyo.

Ile shutuma ni kubwa sana kwa viongozi wetu na mbaya zaidi wamekaa kimya, inawezekana kuna jambo linasubiriwa liishe kwanza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umakini unahitajika hasa hapa.

Kwamba Kesi ya Usajili wa bodi ya Lipumba ulitengulkiwa kwa sababu kuu mbili.

1. Uteuzi ulifanywa bila kufuata matakwa ya kisheria kwa kuitisha mkutano usiotambuliwa kihalali.

2. Mkutano ushuhudiwe na Mamlaka za Serikali jambo ambalo kwanza lilikosekana katika uteuzi wa awali. Hapa Jaji Benhaji ameshawapa njia ya kupita Lipumba kuitwaa Bodi ya wadhamini.



HAPA ieleweke kwamba Tayari Lipumba na wenzake wanakwenda kufanya tena mkutano na kwa sababu wao ndio wanatambuliwa na msajili, bila shaka watakuwepo wawakilishi wa ofisi ya Msajili kama SERIKALI.

Hatua za haraka zinapaswa kuchukuliwa kuzuiya Uovu mwengine unaoandaliwa kwenye kesi hii.
 
Jambo moja liko wazi kuhusu kuhusishwa viongozi waandamizi wa SMZ na SMT kwenye hujuma na rushwa kwa Jaji. Kuelekea uchaguzi wa 2015 mmoja wa waliohusishwa na Rushwa kwenye maamuzi ya kesi hizi za CUF kutoka Serikalini(Zanzibar) alinukuliwa akisema wanakusudia kuifuta CUF kwenye ramani baada ya uchaguzi wa 2015.

Leo hii kuelekea kwenye maamuzi muhimu anatajwa tena kwenye taarifa za siri.

CUF kuweni makini.
Hivi huyu Seif Idd anadhani Mungu ni mjinga ? pigo lile alilopigwa hajifunzi tu ?
 
Jambo lengine la kuwa Makini.

Kwa nini mahakama isiwatambuwe wajumbe wa awali wakati mdai (Mbunge Ally Saleh ) alitaka mahakama itamke kuwa wale ni wajumbe halali ?

Ikiwa hoja ni kuwa hawakuchaguliwa na vikao halali na hapakuwepo uwakilishi wa serikali, basi huo uhalalali tayari ameshapewa Lipumba na watu wake. Ni suala la kufuata utaratibu tu ili kupewa bodi Lipumba.

Hata hoja kwamba iliyokuwepo muda wake unaisha 2019, huo muda ukifika bado kunahitajika kikao halali na uwakilishi wa mamlaka za sertikali ambazo kwa sasa amepewa Lipumba labda maamuzi ya uhalali wa uenyekiti wa Lipumba umtengue.

Taarifa zilizopo uamuzi wa jana ulikuwa unasubiriwa sana na WASALITI na kambi Lipumba ili kufanya hayo yaliyoagizwa yakiwa na Baraka za MAAMUZI YA MAHAKAMA. ilki kufikia azma yao na wadhamini wao.

Na ikiwa hilo litatokea basi ule WARAKA WA SIRI NDIO UTAKUWA UMEPROVE KUHUSIKA KWA JAJI BENHAJ kuhusu ile shutuma ya RUSHWA.

Mchezo itakuwa umepigwa kitaalamu.

Nadhani CUF taasisi mnauona huu mtiririko ulivyo. Kazi kwenu.


Na ikiwa maelezo ninayotoa hapo juu yatakuwa sahihi, basi HAKUNA UWEZEKANO WA KESI YA UENYEKITI WA LIPUMBA KUTOLEWA MAAMUZI.

Nionavyo hivyo ndivyo itakavyokuwa au kutolewa maamuzi yenye UKAKASI USIO NA MWISHO.
 
Back
Top Bottom