CUF kwa nini tumefanya vibaya sana katika uchaguzi mdogo wa Igunga

Poleni sn Cuf,me nna wasiwasi hata ule mtaji Wa kura 11,000 mlisaidiwa na magamba ktk uchakachuaji.
 
Kaka tafakari kwa makini soma alama za nyakati Safari hakuwa mwendawazimu wewe uliona wapi chama kikashindwa mahali kilipoanzishwa ur smart ila umzito kuchukua hatua Julius itakugarimu likiwa limekuchwa
 
Umesema huwezi hamia kwenye chama chenye nguvu kama CHADEMA, hongera kwanza kwa kukiri kuwa CHADEMA wana nguvu, sasa nyie CUF hamna nguvu mnafanya nini sasa, maana ni sawa unaenda kupigana huku ukisema hauna nguvu, mimi binafsi nakuona wewe ni mpambanaji, tatizo ni chama chako, ushauri wangu kwako, HAMIA CHADEMA, 2015 nenda kachukue jimbo la RORYA, maana TARIME, yupo Rais wako WAITARA.

kaka nipo huku home bado(tarime),honestly mtatiro hawezi kushinda rorya kwa sbb kadhaa,ntazitaja
1.sidhani kama ni mkazi wa eneo husika
2.kule asilimia 90 ni wajaluo,mtatiro ni mkurya,ie kumbuka hawa watu walivyo na ukabila,bht nzuri nimehudhuria mazish mara mbili kwa kipindi hiki jimbon rorya,kowack na ochuna,yaan wanamsifu mbunge wao kama mungu wao vile.
3.magamba bado wana nguvu sana rorya kwa sbb mbunge wao anatumia pesa zake binafs kusambaza umeme vijijini,pale nyanchabakenye,marasibora umeme utawaka muda wowote,ikumbukwe mbunge huyu ndo mmiliki wa La Kairo hotel ya kirumba,mwanza.

Ushauri wangu,mtatiro kama ana nia ya dhati ya kuwa mwanamageuzi,ahamie CHADEMA haraka sana,make ndo chama kinachosound huku nyumbani,akienda nccr ausahau ubunge!
Achague kati ya jimbo la Serengeti au Bunda pale kwa msinziaji wasira,nina hakika 2015 atabeba jimbo,othewise hapo cuf anazidi kupoteza mwelekeo wake kisiasa.
Ni hayo tu wakuu!
 
bdo nachelea kuamini,
Pamoja na kutumia chopa?
Mwaka jana hawakutumia chopa bt matokeo yao yalikuwa mazuri.
 
pole sana mkuu mtatiro,acheni siasa za udini na chuki kwa chadema pia vunjeni ndoa yenu na magamba ndipo mtaeleweka
 
Mtatiro ahsante kwa kuikubali nguvu ya umma, kwamba cdm ni chama cha upinzani 'chenye nguvu (ya umma)'.
Hebu ungana na hii nguvu kuleta uhuru wa kweli wa tz yetu. Umoja ni nguvu ndivyo wahenga wetu walivyotuasa.
 
Tatizo lenu ni propaganda chafu za udini na ukabila ndo zimewaua, nakuhakikishia kua huo ni mwanzo tu, gharika kubwa inakuja mbele yenu. Ndio nyie ni CCM B kwani uongo? Kule Zanzibar nyie si ni sehemu ya serikali?, tuwaiteje sasa?. Hata mkijipanga vp kama hamtaachana na hayo, mtakua kama NCCR 2015
 
Lazima nikiri kuwa washindani wetu wakubwa CCM na CHADEMA wametushinda katika uchaguzi mdogo wa Igunga.

Kwa matokeo ambayo nimeyashayapokea kutoka kwenye asilimia 88 ya vituo kwa ujumla tumefanya vibaya sana. Japokuwa tumekuwa na mgombea mzuri sana na tumemnadi kwa kutumia uwezo wetu wote ambao kwa hakika kila mtu ameuona, lakini matokeo hatuwezi kuyageuza.

Ninachojifunza zaidi ni kuwa wapiga kura wengi ndani ya Tanzania bado wanaamini zaidi propaganda kuliko hali halisi ya mazingira yanayowakabili na hii ikizidi kushabikiwa ndivyo ambavyo wananchi watakosa fursa bora siku za mbele.
Ikiwa hali hii itaendelea hivi ina maana bado nchi ina safari ndefu ya kufikia demokrasia ya kweli na maendeleo yatakayoonekana kwa macho.

Katika uchaguzi huu wa Igunga CUF tumepambana na changamoto kubwa ya kujibu propaganda zilezile kuwa eti "Sisi ni CCM B", kila tulikoenda tumekutana na kikwazo hiki, tumejaribu kwa dhati kuwaelimisha wananchi bila mafanikio na muda umekuwa ukikimbia kuliko upepo.

Hata hivyo bado naamini kuwa tutapata fursa kubwa ya kuwaelimisha wananchi siku za usoni. Mimi na wenzangu hatutakata tamaa kwani MAFANIKIO KATIKA NYANJA YA SIASA huhitaji mioyo migumu.

Natambua kuwa uongozi ni dhamana nzito inayohitaji kujipanga zaidi na zaidi, Na CUF itazidi kujipanga zaidi na zaidi na kila tutakapoanguka tutanyanyuka na kuanza safari, hakika TUTAFIKA.

Chama changu kinakabiliwa na changamoto kubwa sana mbele ya safari na kwa hakika inahitaji tuzidi kujipanga na kujiimarisha. Kama chama hatutajilaumu kamwe, tumeonesha uwezo mkubwa na kufanya kampeni sahihi tukiwa na mgombea wa kiwango kizuri kwa mpiga kura yeyote anayehitaji kiongozi. Lakini kusimamisha mgombea mzuri na kufanya kampeni nzuri wakati mwingine siyo sababu ya kufanya vizuri. Maamuzi ya nani awe mbunge, ni mzuri au mbaya, anafaa au hafai yako kwa wananchi.

Wananchi wa Igunga tunawashukuru kwa namna walivyotuunga mkono na tunawaomba wawe kitu kimoja katika kuiendeleza Igunga yao kwani mshindi akishatangazwa yeye ni mbunge wa wananchi wote. Vyama vyetu hivi vipo ili kuisaidia jamii kupata kiongozi mzuri tu, nasi kama chama tumetimiza wajibu wetu.

Mimi kama kiongozi wa ngazi ya juu wa CUF - Tanzania Bara(Bila kujali nimekuwa kiongozi wa ngazi ya juu miezi minne tu iliyopita tu) nabeba dhamana kwa matokeo yote tuliyopita, najitwika mzigo wa kusimama imara kuiimarisha CUF. Sitatoka CUF na kukimbilia kwenye vyama vyenye nguvu Tanzania bara kama CHADEMA n.k. eti kwa sababu tu CUF imefanya vibaya kwenye uchaguzi. Ninaamini katika CUF na nitaisaidia Tanzania yangu nikiwa CUF, ninaamini siku moja wakati CUF imeimarika nitatajwa kati ya watu ambao hawakukata tamaa na hawakuyumbishwa na magumu yaliyowakabili na walisimama kidete kwenda mbele.

Tunawashukuru wale wote waliotuunga mkono katika uchaguzi huu na wale wanaotuunga mkono siku zote na wale watakaotuunga mkono siku zijazo. Kwa hakika wote tunawashukuru sana na CUF itasimama imara.

Mungu awabariki sana.

"HAKI SAWA KWA WOTE"

Julius Mtatiro,
Naibu Katibu Mkuu,
Chama Cha Wananchi - CUF,
Tanzania Bara,
02 Oktoba 2011,
Igunga - Tabora.

Mkuu Hongera sana kwa kukubali kushindwa, Ingawa sijapenda namna unavyotoa visingizio. Ushauri wa bure kwenu wanasiasa wa Tanzania ni kwamba "msiwadharau wananchi" hizo tabia zenu za kupigana "vijembe wapinzani kwa wapinzani" zitaendelea kuwapa matokeo ya hovyo katika kila Uchaguzi mdogo ulioko mbele yenu, mtaendelea kupoteza mapesa mengi kukodi helikopta kwa ajili ya dharura za nyakati za Chaguzi ndogo bila mikakati endelevu ya kuwaamsha wananchi na wanachama wenu. Adui yenu ni mmoja, kaeni kama wapinzani na mpange namna ya kupambana kumtoa madarakani huyo adui yenu. CUF na CHADEMA mmeingizwa kwenye mtego wa kijinga wa UDINI na UKABILA unaowachukulia muda mrefu wa kampeni zenu kujisafisha na upuuzi huo. Wako wapi watu wenu wa "fitna/propaganda?."

Mnawatumia ipasavyo?

.........Ukichoshwa na kuibeba CUF, kuna Chama makini unaweza kuhamia na huenda ukaweza kushirikiana na Makamanda waliopo kujenga upinzani wa kweli.

Wasalaam,

Kombo
 
Tumeshakuzoea kubwabwaja. Ulibwabwaja katika jali ya MV Spice Isander kuhusu kujiuzulu kwa waziri wa Miundo mbinu wa (SUK) ambaye anatoka CUF lakini umeshindwa kulisimamia. Ni dhahiri kuwa kidogo kidogo unridhishwa mienendo na tabia za Magamba.
 
Lazima nikiri kuwa washindani wetu wakubwa CCM na CHADEMA wametushinda katika uchaguzi mdogo wa Igunga.

Ninachojifunza zaidi ni kuwa wapiga kura wengi ndani ya Tanzania bado wanaamini zaidi propaganda kuliko hali halisi ya mazingira yanayowakabili na hii ikizidi kushabikiwa ndivyo ambavyo wananchi watakosa fursa bora siku za mbele.
Chama chako kitaendelea kuzama kwa kuwa inaonekana hamjajifunza chochote kutokana na kuanguka kwenu vibaya Igunga. Mliivamia Igunga kwa propaganda zaidi, bila kujua wana-Igunga wanataka nini. kuanzia zile za mtaji wenu wa kura 11,000 hadi zile za CDM kukosa base huko. Binafsi nilishangaa sana kumsikia Hamad Rashid akiwaomba wana-Igunga wainyime kura CDM kwa kuwa si chama cha kitaifa, ni utaifa gani aliokuwa akimaanisha, Upemba?

Hamjachelewa sana, lakini hiki si kizazi cha kucheza na akili za watu kwa propaganda. Wananchi wanajua wanahitaji nini. Wanachotaka kusikia toka kwako ni namna gani utawasaidia kupata haki zao.
 
Lazima nikiri kuwa washindani wetu wakubwa CCM na CHADEMA wametushinda katika uchaguzi mdogo wa Igunga.

Kwa matokeo ambayo nimeyashayapokea kutoka kwenye asilimia 88 ya vituo kwa ujumla tumefanya vibaya sana. Japokuwa tumekuwa na mgombea mzuri sana na tumemnadi kwa kutumia uwezo wetu wote ambao kwa hakika kila mtu ameuona, lakini matokeo hatuwezi kuyageuza.

Ninachojifunza zaidi ni kuwa wapiga kura wengi ndani ya Tanzania bado wanaamini zaidi propaganda kuliko hali halisi ya mazingira yanayowakabili na hii ikizidi kushabikiwa ndivyo ambavyo wananchi watakosa fursa bora siku za mbele.
Ikiwa hali hii itaendelea hivi ina maana bado nchi ina safari ndefu ya kufikia demokrasia ya kweli na maendeleo yatakayoonekana kwa macho.

Katika uchaguzi huu wa Igunga CUF tumepambana na changamoto kubwa ya kujibu propaganda zilezile kuwa eti "Sisi ni CCM B", kila tulikoenda tumekutana na kikwazo hiki, tumejaribu kwa dhati kuwaelimisha wananchi bila mafanikio na muda umekuwa ukikimbia kuliko upepo.

Hata hivyo bado naamini kuwa tutapata fursa kubwa ya kuwaelimisha wananchi siku za usoni. Mimi na wenzangu hatutakata tamaa kwani MAFANIKIO KATIKA NYANJA YA SIASA huhitaji mioyo migumu.

Natambua kuwa uongozi ni dhamana nzito inayohitaji kujipanga zaidi na zaidi, Na CUF itazidi kujipanga zaidi na zaidi na kila tutakapoanguka tutanyanyuka na kuanza safari, hakika TUTAFIKA.

Chama changu kinakabiliwa na changamoto kubwa sana mbele ya safari na kwa hakika inahitaji tuzidi kujipanga na kujiimarisha. Kama chama hatutajilaumu kamwe, tumeonesha uwezo mkubwa na kufanya kampeni sahihi tukiwa na mgombea wa kiwango kizuri kwa mpiga kura yeyote anayehitaji kiongozi. Lakini kusimamisha mgombea mzuri na kufanya kampeni nzuri wakati mwingine siyo sababu ya kufanya vizuri. Maamuzi ya nani awe mbunge, ni mzuri au mbaya, anafaa au hafai yako kwa wananchi.

Wananchi wa Igunga tunawashukuru kwa namna walivyotuunga mkono na tunawaomba wawe kitu kimoja katika kuiendeleza Igunga yao kwani mshindi akishatangazwa yeye ni mbunge wa wananchi wote. Vyama vyetu hivi vipo ili kuisaidia jamii kupata kiongozi mzuri tu, nasi kama chama tumetimiza wajibu wetu.

Mimi kama kiongozi wa ngazi ya juu wa CUF - Tanzania Bara(Bila kujali nimekuwa kiongozi wa ngazi ya juu miezi minne tu iliyopita tu) nabeba dhamana kwa matokeo yote tuliyopita, najitwika mzigo wa kusimama imara kuiimarisha CUF. Sitatoka CUF na kukimbilia kwenye vyama vyenye nguvu Tanzania bara kama CHADEMA n.k. eti kwa sababu tu CUF imefanya vibaya kwenye uchaguzi. Ninaamini katika CUF na nitaisaidia Tanzania yangu nikiwa CUF, ninaamini siku moja wakati CUF imeimarika nitatajwa kati ya watu ambao hawakukata tamaa na hawakuyumbishwa na magumu yaliyowakabili na walisimama kidete kwenda mbele.

Tunawashukuru wale wote waliotuunga mkono katika uchaguzi huu na wale wanaotuunga mkono siku zote na wale watakaotuunga mkono siku zijazo. Kwa hakika wote tunawashukuru sana na CUF itasimama imara.

Mungu awabariki sana.

"HAKI SAWA KWA WOTE"

Julius Mtatiro,
Naibu Katibu Mkuu,
Chama Cha Wananchi - CUF,
Tanzania Bara,
02 Oktoba 2011,
Igunga - Tabora.

Umejieleza vizuri sana KATIBU hongera. Tatizo la CUF si muafaka uliopo kati yake na CCM, tatizo linajitokeza pale ambapo kunakuwepo na jambo la msingi kwa maslahi ya taifa wabunge wa CUF wanakuwa kama vile wamepigwa ganzi.
 
Kushindwa mahali kilipoanzishwa ni mkakati wa maksudi ili chama kisonekane kina ukabila
 
Mtatiro nimekusoma kwa makini umeeleweka, propaganda za chadema zina mwisho wake, mbona wao ndio walio anzisha ndoa tena ya jamvi huko kigoma, au ndoa ya cuf ni ya godoro thet why wana cry????????????????????????????????????
 
Mr.Mtatiro Iam among those people who admiring u so badly for your political boldness.

However have been always convinced that you are in a wrong boat.Come and join us so that we may sail through together in liberating our beautiful country.
For instance Kinondoni constituents to my opinion is still vacant and hence need a strong candidate as you are.Nazan ungekuwa cdm in the 2010
and vie for that constituents ungekuwa mh.mbunge wetu.Anyway thats my opinion tu.
 
Back
Top Bottom