CUF kwa nini tumefanya vibaya sana katika uchaguzi mdogo wa Igunga

Jun 20, 2009
45
224
Lazima nikiri kuwa washindani wetu wakubwa CCM na CHADEMA wametushinda katika uchaguzi mdogo wa Igunga.

Kwa matokeo ambayo nimeyashayapokea kutoka kwenye asilimia 88 ya vituo kwa ujumla tumefanya vibaya sana. Japokuwa tumekuwa na mgombea mzuri sana na tumemnadi kwa kutumia uwezo wetu wote ambao kwa hakika kila mtu ameuona, lakini matokeo hatuwezi kuyageuza.

Ninachojifunza zaidi ni kuwa wapiga kura wengi ndani ya Tanzania bado wanaamini zaidi propaganda kuliko hali halisi ya mazingira yanayowakabili na hii ikizidi kushabikiwa ndivyo ambavyo wananchi watakosa fursa bora siku za mbele.
Ikiwa hali hii itaendelea hivi ina maana bado nchi ina safari ndefu ya kufikia demokrasia ya kweli na maendeleo yatakayoonekana kwa macho.

Katika uchaguzi huu wa Igunga CUF tumepambana na changamoto kubwa ya kujibu propaganda zilezile kuwa eti "Sisi ni CCM B", kila tulikoenda tumekutana na kikwazo hiki, tumejaribu kwa dhati kuwaelimisha wananchi bila mafanikio na muda umekuwa ukikimbia kuliko upepo.

Hata hivyo bado naamini kuwa tutapata fursa kubwa ya kuwaelimisha wananchi siku za usoni. Mimi na wenzangu hatutakata tamaa kwani MAFANIKIO KATIKA NYANJA YA SIASA huhitaji mioyo migumu.

Natambua kuwa uongozi ni dhamana nzito inayohitaji kujipanga zaidi na zaidi, Na CUF itazidi kujipanga zaidi na zaidi na kila tutakapoanguka tutanyanyuka na kuanza safari, hakika TUTAFIKA.

Chama changu kinakabiliwa na changamoto kubwa sana mbele ya safari na kwa hakika inahitaji tuzidi kujipanga na kujiimarisha. Kama chama hatutajilaumu kamwe, tumeonesha uwezo mkubwa na kufanya kampeni sahihi tukiwa na mgombea wa kiwango kizuri kwa mpiga kura yeyote anayehitaji kiongozi. Lakini kusimamisha mgombea mzuri na kufanya kampeni nzuri wakati mwingine siyo sababu ya kufanya vizuri. Maamuzi ya nani awe mbunge, ni mzuri au mbaya, anafaa au hafai yako kwa wananchi.

Wananchi wa Igunga tunawashukuru kwa namna walivyotuunga mkono na tunawaomba wawe kitu kimoja katika kuiendeleza Igunga yao kwani mshindi akishatangazwa yeye ni mbunge wa wananchi wote. Vyama vyetu hivi vipo ili kuisaidia jamii kupata kiongozi mzuri tu, nasi kama chama tumetimiza wajibu wetu.

Mimi kama kiongozi wa ngazi ya juu wa CUF - Tanzania Bara(Bila kujali nimekuwa kiongozi wa ngazi ya juu miezi minne tu iliyopita tu) nabeba dhamana kwa matokeo yote tuliyopita, najitwika mzigo wa kusimama imara kuiimarisha CUF. Sitatoka CUF na kukimbilia kwenye vyama vyenye nguvu Tanzania bara kama CHADEMA n.k. eti kwa sababu tu CUF imefanya vibaya kwenye uchaguzi. Ninaamini katika CUF na nitaisaidia Tanzania yangu nikiwa CUF, ninaamini siku moja wakati CUF imeimarika nitatajwa kati ya watu ambao hawakukata tamaa na hawakuyumbishwa na magumu yaliyowakabili na walisimama kidete kwenda mbele.

Tunawashukuru wale wote waliotuunga mkono katika uchaguzi huu na wale wanaotuunga mkono siku zote na wale watakaotuunga mkono siku zijazo. Kwa hakika wote tunawashukuru sana na CUF itasimama imara.

Mungu awabariki sana.

"HAKI SAWA KWA WOTE"

Julius Mtatiro,
Naibu Katibu Mkuu,
Chama Cha Wananchi - CUF,
Tanzania Bara,
02 Oktoba 2011,
Igunga - Tabora.
 
kiche

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
456
155
Nakumbuka wakati kampeni zinaaoza CUF walisema wameanza na mtaji wa kura 11 elfu je umeyeyukia wapi?
Hazijayeyuka mkuu!!!!,bado wanaendelea kuhesabu!,kumbuka wapiga kura wapo 170000!!!!zilizohesabiwa hata hizo 11,000 bado!tuwasubiri
 
Eshacky

JF-Expert Member
Apr 26, 2011
962
242
Poleni sana,ila "kama huwez kupingana nao bas jiunge pamoja nao", huo msemo mwepesi hauitaji Phd kuuelewa na kuutekeleza.
 
samirnasri

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
1,388
213
hawakujua tu hizo zilikuwa za chadema jamaa wakaamua kupigia cuf kwa kuwa cdm hawakuweka mgombea.
 
jnuswe

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
1,270
549
Kwamujibu wa matoeo ya awali jimboni Igunga, inaonekana dhahiri shahiri kua CUF sio washindani. Sasa najiuliza ule mtaji waliokua wanajivunia hadi kufikia hatua ya kuwaomba CDM wajitoe umekwenda wapi?

CUF bara haina nguvu na haitatokea kuja kupata kuwa na nguvu, na ile ndoa ndo kabisaa imewamaliza labda waachike ndo watapanda chart
 
Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,882
Ule mtaji wao umeishia wapi ? Yeye si alidhani kwamba KAFU ni chama huku bara ? Yule naye ni chaka mwache ale posho maana akienda kokote hawezi kupokelewa mwache atumike tu .
 
jambo1

JF-Expert Member
Jul 5, 2009
241
29
Katika uchaguzi huu wa Igunga CUF tumepambana na changamoto kubwa ya kujibu propaganda zilezile kuwa eti "Sisi ni CCM B", kila tulikoenda tumekutana na kikwazo hiki, tumejaribu kwa dhati kuwaelimisha wananchi bila mafanikio na muda umekuwa ukikimbia kuliko upepo.

Hata hivyo bado naamini kuwa tutapata fursa kubwa ya kuwaelimisha wananchi siku za usoni. Mimi na wenzangu hatutakata tamaa kwani MAFANIKIO KATIKA NYANJA YA SIASA huhitaji mioyo migumu.

Natambua kuwa uongozi ni dhamana nzito inayohitaji kujipanga zaidi na zaidi, Na CUF itazidi kujipanga zaidi na zaidi na kila tutakapoanguka tutanyanyuka na kuanza safari, hakika TUTAFIKA.

Chama changu kinakabiliwa na changamoto kubwa sana mbele ya safari na kwa hakika inahitaji tuzidi kujipanga na kujiimarisha. Kama chama hatutajilaumu kamwe, tumeonesha uwezo mkubwa na kufanya kampeni sahihi tukiwa na mgombea wa kiwango kizuri kwa mpiga kura yeyote anayehitaji kiongozi. Lakini kusimamisha mgombea mzuri na kufanya kampeni nzuri wakati mwingine siyo sababu ya kufanya vizuri. Maamuzi ya nani awe mbunge, ni mzuri au mbaya, anafaa au hafai yako kwa wananchi.

Wananchi wa Igunga tunawashukuru kwa namna walivyotuunga mkono na tunawaomba wawe kitu kimoja katika kuiendeleza Igunga yao kwani mshindi akishatangazwa yeye ni mbunge wa wananchi wote. Vyama vyetu hivi vipo ili kuisaidia jamii kupata kiongozi mzuri tu, nasi kama chama tumetimiza wajibu wetu.

Mimi kama kiongozi wa ngazi ya juu wa CUF - Tanzania Bara(Bila kujali nimekuwa kiongozi wa ngazi ya juu miezi minne tu iliyopita tu) nabeba dhamana kwa matokeo yote tuliyopita, najitwika mzigo wa kusimama imara kuiimarisha CUF.
Sitatoka CUF na kukimbilia kwenye vyama vyenye nguvu Tanzania bara kama CHADEMA n.k.
eti kwa sababu tu CUF imefanya vibaya kwenye uchaguzi. Ninaamini katika CUF na nitaisaidia Tanzania yangu nikiwa CUF, ninaamini siku moja wakati CUF imeimarika nitatajwa kati ya watu ambao hawakukata tamaa na hawakuyumbishwa na magumu yaliyowakabili na walisimama kidete kwenda mbele.
Hapo kwenye rangi ya Magamba..,mi nadhani Chadema hikina nafasi yako kwa sasa..,lakini kama utakuwa mwanachama mwaminifu kama mimi karibu sana vinginevyo..rudi wa "CCM A" kabisa..!
 
Jackbauer

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
5,955
2,012
najua umeshapata matokeo ya awali,tueleze mwenenendo wa matokeo unadhani nani ni mshindi?be honest!
 
Hossam

JF-Expert Member
Feb 10, 2011
3,399
1,857
Pole kamanda, hilo ndo tatizo la uke wenza, mke mkubwa akikasirika basi bi mdogo huambulia sms fupifupi tu, hiyo ndo faida ya kujidai mnakiherehere kuingia muafaka wa kijinga zenji sasa inawakosti, ni afadhali watu wafe ila haki itendeke, sasa maalim seif anachonga tu sharafu zake huko ikulu zenji wewe unaambulia vumbi, jaribu kukua kaka...
 
Katavi

Platinum Member
Aug 31, 2009
41,812
12,406
Poleni sana, ni muda muafaka wa kujichunguza mlipojikwaa na kujipanga upya.
 
politiki

JF-Expert Member
Sep 2, 2010
2,376
1,504
Pole sana kwa pilikapilika za uchaguzi,

Mmejitahidi ingawa kura hazikutosha lakini nina ushauri kwa CUF ingawa leo siyo siku yake lakini ninachoweza kukisema ni kwamba CUF needs seriuos reform kama kweli chama hiki kinataka kuwa na future hasa kwa Tanzania-bara nitakushauri nini cha kufanya wakati mzuri ukiwadia kwa hivi sasa nawatakia mapumziko mema na hongereni sana kwa kupigana mpaka dakika za mwisho ingawaje press iliwaangusha sana kwa kutowapa coverage ya kutosha jihandae kwa kupata ushaurri wangu na wengineo.
 
tortoise

Member
Oct 6, 2010
39
6
Mkuu naona unawajengea Ccm mazingira ya uchakachuaji ili wakitangazwa washindi kwa Wizi wa kura chadema nao waige uungwana wenu bandia wa kukubali matokeo !
 
palalisote

JF-Expert Member
Aug 4, 2010
8,336
1,447
" The history we read is not based on facts at all but rather the series of accepted judgments"
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

33 Reactions
Reply
Top Bottom