CUF kwa nini tumefanya vibaya sana katika uchaguzi mdogo wa Igunga

Namwonea huruma Mtatiro, kijana mdogo kapotea njia.Inabidi tukufanyie maombi, utaanza kuona, na utahamia kwetu!
 
Ndoa mliyonayo inawagharimu na itaendelea kuwapotezea wanachama na mtazidi kupoteza nguvu mliyokuwa nayo kabla ambayo hata CHADEMA haikuwa nayo!!!vunjeni hiyo ndoa,kila moja apigane kivyake,hapo ndo mnaweza fika,lasivyo mtazidi didimia kisiasa
 
Hapa nmdipo napokoma na wanasiasa wa Kitanzania.. Huyu Mtatiro kaandika mengi walikumbana nayo huko Igunga na walijaribu kuwaelimisha wananchi lakini hawakumsikiza. Na akafikia majibu ambayo pengine yanamfurahisha yeye kuwa Tatizo ni wananchi sio CUF..
sasa amekuja hapa JF na kuleta hadithi ile ile kaulizwa maswali kaingia kizani kisha bila aibu anajitukuza kwamba dhamana alopewa ni kubwa na yuko tayari kuibeba. Mbona umeingia mitini?
Karibu, njoo, wape watu majibu tena ujumbe huu utawafikia wananchi wengi zaidi na sii jimbo la Igunga pekee..
 
Mtatiro mlikwenda Igunga mkijua kwa hakika kuwa mtapata matokeo mliyopata.

Ndio sababu mlipofika Igunga vita yenu ikawa ni Chadema na sio CCM. Kwa hiyo usije unalia lia hapa ili kudhani tapata huruma zetu.

Labda nikuhakikishie jambo moja tu kwamba hivi ndivyo itakavyokuwa hata chaguzi zijazo. Wewe baki tu ukijiridhisha kwa maneno mengi yasiyo na maana. Ile dominance ya kafu kwa siasa za upinzani bara na visiwani imekwisha. Nakuahakikishia hata kule Pemba mmekwisha.

Nashangaa kwa nini hukuzungumzia kwa nini wale wapiga kura wenu wengi wa october 2010 wamewapa kisogo!!!! Najua utabaki na story za ndoa yenu na ccm. Sawa kama ndio sababu huoni kwamba mmekwisha? Mmebaki nyie na ccm kuhubiri udini tu.

Hivi ndivyo NCCR walivyokwisha pia, now your the next. Na wewe utakwisha kisiasa na kafu yako.

. Tatizo nilisha sema,wapinzani we2 ni ccm. Sasa 2mewafanya cdm ndo wapinzani. Wananchi wanajiuliza,inakuwaje cuf wanampinga cdm?, mbili 2meendekeza udini, . Mtatiro waeleze wanachama kuwa udini hatuutaki. Toeni tamko la kupinga kauli za bakwata tabora,kuhusu waisilamu wasiipigie kura cdm, mulaani
 
Mtatiro, wewe ni mtu mzima

acha upuuzi wako na wenu wana-kafu... be a serious political party (na sio nyumba ndogo ya CCM or quit politics

to be honest, nakuheshimu sana tu, ila wewe kuwa kafu ni sawa na wasirra kuimba taarbu au Mrema kucheza kiduku

Stop cheap party shitty and be real, join chadema or CCM uwe na heshima na sauti
 
Umesema huwezi hamia kwenye chama chenye nguvu kama CHADEMA, hongera kwanza kwa kukiri kuwa CHADEMA wana nguvu, sasa nyie CUF hamna nguvu mnafanya nini sasa, maana ni sawa unaenda kupigana huku ukisema hauna nguvu, mimi binafsi nakuona wewe ni mpambanaji, tatizo ni chama chako, ushauri wangu kwako, HAMIA CHADEMA, 2015 nenda kachukue jimbo la RORYA, maana TARIME, yupo Rais wako WAITARA.

Baada ya kusikiliza michango iliyotolewa na wabunge wa CUF toka Pemba/Zanzibar kuhusu muswaada wa kuandika Katiba Mpya,nimekumbuka ushauri huu aliopewa ndugu yetu kijana Mtatiro.
 
Mngesimama nyinyi wenyewe bila ya huo muungano wenu na magamba hakika mngekua pazuri xana.Uchaguzi ujao hakikisheni mnauvunja huo muungano.
 
Lazima nikiri kuwa washindani wetu wakubwa CCM na CHADEMA wametushinda katika uchaguzi mdogo wa Igunga.

Kwa matokeo ambayo nimeyashayapokea kutoka kwenye asilimia 88 ya vituo kwa ujumla tumefanya vibaya sana. Japokuwa tumekuwa na mgombea mzuri sana na tumemnadi kwa kutumia uwezo wetu wote ambao kwa hakika kila mtu ameuona, lakini matokeo hatuwezi kuyageuza.

Ninachojifunza zaidi ni kuwa wapiga kura wengi ndani ya Tanzania bado wanaamini zaidi propaganda kuliko hali halisi ya mazingira yanayowakabili na hii ikizidi kushabikiwa ndivyo ambavyo wananchi watakosa fursa bora siku za mbele.
Ikiwa hali hii itaendelea hivi ina maana bado nchi ina safari ndefu ya kufikia demokrasia ya kweli na maendeleo yatakayoonekana kwa macho.

Katika uchaguzi huu wa Igunga CUF tumepambana na changamoto kubwa ya kujibu propaganda zilezile kuwa eti "Sisi ni CCM B", kila tulikoenda tumekutana na kikwazo hiki, tumejaribu kwa dhati kuwaelimisha wananchi bila mafanikio na muda umekuwa ukikimbia kuliko upepo.

Hata hivyo bado naamini kuwa tutapata fursa kubwa ya kuwaelimisha wananchi siku za usoni. Mimi na wenzangu hatutakata tamaa kwani MAFANIKIO KATIKA NYANJA YA SIASA huhitaji mioyo migumu.

Natambua kuwa uongozi ni dhamana nzito inayohitaji kujipanga zaidi na zaidi, Na CUF itazidi kujipanga zaidi na zaidi na kila tutakapoanguka tutanyanyuka na kuanza safari, hakika TUTAFIKA.

Chama changu kinakabiliwa na changamoto kubwa sana mbele ya safari na kwa hakika inahitaji tuzidi kujipanga na kujiimarisha. Kama chama hatutajilaumu kamwe, tumeonesha uwezo mkubwa na kufanya kampeni sahihi tukiwa na mgombea wa kiwango kizuri kwa mpiga kura yeyote anayehitaji kiongozi. Lakini kusimamisha mgombea mzuri na kufanya kampeni nzuri wakati mwingine siyo sababu ya kufanya vizuri. Maamuzi ya nani awe mbunge, ni mzuri au mbaya, anafaa au hafai yako kwa wananchi.

Wananchi wa Igunga tunawashukuru kwa namna walivyotuunga mkono na tunawaomba wawe kitu kimoja katika kuiendeleza Igunga yao kwani mshindi akishatangazwa yeye ni mbunge wa wananchi wote. Vyama vyetu hivi vipo ili kuisaidia jamii kupata kiongozi mzuri tu, nasi kama chama tumetimiza wajibu wetu.

Mimi kama kiongozi wa ngazi ya juu wa CUF - Tanzania Bara(Bila kujali nimekuwa kiongozi wa ngazi ya juu miezi minne tu iliyopita tu) nabeba dhamana kwa matokeo yote tuliyopita, najitwika mzigo wa kusimama imara kuiimarisha CUF. Sitatoka CUF na kukimbilia kwenye vyama vyenye nguvu Tanzania bara kama CHADEMA n.k. eti kwa sababu tu CUF imefanya vibaya kwenye uchaguzi. Ninaamini katika CUF na nitaisaidia Tanzania yangu nikiwa CUF, ninaamini siku moja wakati CUF imeimarika nitatajwa kati ya watu ambao hawakukata tamaa na hawakuyumbishwa na magumu yaliyowakabili na walisimama kidete kwenda mbele.

Tunawashukuru wale wote waliotuunga mkono katika uchaguzi huu na wale wanaotuunga mkono siku zote na wale watakaotuunga mkono siku zijazo. Kwa hakika wote tunawashukuru sana na CUF itasimama imara.

Mungu awabariki sana.

"HAKI SAWA KWA WOTE"

Julius Mtatiro,
Hamia ....CHADEMA
 
Vunjeni ndoa yenu na CCM na acheni siasa za udini

Na wewe umeingia kwenye mtego wa ccm kudai cuf ina udini wa kiislam na upemba mwingi kama ambavyo ccm hao hao wanavyodai chadema ni chama cha wachagga na wakristo!kweli ccm wanawapatia sana aisee!lakini nimejifunza kitu;ccm inawaogopa,haitaki muungane,inajua mkiungana mtaishinda ndio maana inawagawa kwa propaganda hiyo ya udini,bahati mbaya na nyie bado mko usingizini ccm inasonga mbele,mkija kuamka too late kumeshakucha!
 
poleni CUF,lakini fanyeni utafiti wa kina yaani ktaalamu kwanza lakini lililo wazi mko upande wa utawala pia someni nyakati.wananchi wanahitaji yale ya arobaini na saba? badilisheni mwendo wenu
 
Back
Top Bottom