Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,744
Na Mwandishi wetu.
Elias Kundecha.
10.08.2010
Habari za kurudi kwa Zanzibar kama nchi nje ya mipaka yake na ndani ya Jamhuri ya Muungano kumeibua hisia mpya za viongozi waandamizi ndani ya Chama cha CUF ambacho kimekuwa mstari wa mbele katika kudai serikali tatu,madai ambayo ni nambari one katika sera za CUF.
Habari zilizozagaa katika mitaa ya Zanzibar ambazo inasemekana zinategemewa kupitishwa katika kikao cha Baraza La Wawakilishi ni kwa kuibadilisha Katiba ya Zanzibar kwa baadhi ya vifungu vinavyoonyesha kuwa Zanzibar itakuwa Nchi kamili yenye kujiamulia na kujipangia mambo yake bila kupitia katika Bunge la Muungano ,baadhi ya mabadiliko hayo ni Zanzibar ni nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na visiwa vidogo vilivyoizunguuka na bahari yake, ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar iliitwa Jamhuri ya watu wa Zanzibar.Hapa wanadai kuwa hata Mombasa ni sehemu ya Zanzibar ,kumbuka tu kuna kesi inategemea kuwakilishwa katika mahakama ya kimataifa ,ikishitakiwa Kenya na UK kuhusiana na Mombasa.
Pia kuna madai yanayoonyesha kuwa Zanzibar ni miongoni mwa nchi mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Kipande ambacho ndicho kitakachoisukuma CUF kuidai na kuirudisha Tanganyika iwapo itaibuka na Ushindi katika uchaguzi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar,hapo ndipo itakapotekeleza sera ya kuwa na serikali Tatu ,vilevile inatarajia kuibua hoja ya kuitisha kura ya maoni ikiwa wananchi wa Tanganyika watakubali kurudishwa kwa serikali ya Tanganyika kura ambayo maoni au uamuzi wa mwisho ni serikali iliyopo madarakani.
Viongozi hao wa serikali wamesikika wakisema iliobaki ni Tanganyika kwani Zanzibar inazidi kuonyesha mikakati ya kujiongoza katika maendeleo bila ya kuitegemea serikali iliyokuwepo ya Muungano ,serikali ambayo imeshindwa kutekeleza ahadi nyingi ikiwemo suala la kushughulikia wala rushwa wakubwa ,na hivyo kuiwacha nchi ikipoteza dira.Na waliopo madarakani wakiogopana katika kuchukuliana sheria na kuacha ,sheria na hukumu zichukue mkondo wake.
Hata hivyo viongozi hao walisema bado waTanzania wengi wamelala na wapo katika ndoto kuwa ipo siku CCM itawakomboa ,ndoto ambayo haitekelezeki.Na katika mikakati iliyojipangia CUF imesema itaanza harakati zake za kampeni kwa kuwahamasisha wananchi kuwa iwapo itaingia madarakani itahakikisha Serikali ya Tanganyika inarudi na dira watazindua dira mya kwa waTanganyika wote.