CUF Ina mgogoro na Vyombo vya Habari? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF Ina mgogoro na Vyombo vya Habari?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by CRITO, Sep 11, 2012.

 1. C

  CRITO Member

  #1
  Sep 11, 2012
  Joined: Aug 30, 2012
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Juzi Chama Cha CUF Kilifanya mkutano mkubwa wa hadhara katika viwanja vya Jangwani.

  Nilikuwepo binafsi nikichukua picha na kusikiliza hotuba mbalimbali. Pamoja na mambo mengine, CUF Inaonekana kutokuwasema vizuri wana habari na nilisikia mwenyewe kutoka hotuba za viongozi, isipokuwa Lipumba pekee mashambulizi, ama vijembe kwa wanahabari.

  Viongozi wa CUF wanaamini vyombo vya habari havipendi, ama vinapotosha, ama vinabeza habari kuhusu chama chao, na nilisikia watu wa kawaida wakiazimia kupiga waandishi watakaohudhuria mkutano wao baadaye ikiwa ule wa Jangwani hautaonekana kupewa kipaumbele kwenye vyombo vya habari,hususani magazeti.

  Na kweli nimefuatilia magazeti ya jana, mengi hayakutoa uzito wowote kwa habari ya CUF. Mtanzania waliweka picha ya umati,lakini habari yao kuu ilihusu taarifa ya awali ya mkutano wa kamati kuu ya CHADEMA, vivyo hivyo magazeti mengine.


  Sasa ni kweli upo mgogoro kati ya waandishi na CUF? Kama ndiyo, umesababishwa na nini, na kama hakuna ugomvi, nini kinapelekea habari za CUF kutopata uzito unaostahili kwenye vyombo vya habari? Je, yawezekana ni mikakati ya washindani wao kisiasa yaani CCM na CHADEMA kwamba CUF wasipewe uzito? Ama ni udhaifu wa idara ya habari ya chama cha CUF yenyewe kutotenda kazi ipasavyo?

  Maana nikiri pia kuwa japo mimi ni mwanahabari sikumjua afisa habari wa CUF hadi juzi alipotambulishwa mkutanoni. Na katika mengi ama yawezekana hii ni kutokana na CUF kushuka umaarufu kisiasa kiasi kwamba habari zake hazivuti wasomaji?

  Naomba mitazamo yenu

  Chanzo: Mjengwablog
   
 2. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #2
  Sep 11, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,351
  Trophy Points: 280
  Umewauliza kama kipigo cha kwanza walichokitoa hadi wakasusiwa waliweka maridhiano ya uhakika? Kabla ya kutoa kipigo cha pili,na iwe mwisho wao wa kuandikwa ?
   
 3. S

  SHEMGUNGA JF-Expert Member

  #3
  Sep 11, 2012
  Joined: Jan 13, 2012
  Messages: 653
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  wamefulia hawana jipya!
   
 4. Sabung'ori

  Sabung'ori JF-Expert Member

  #4
  Sep 11, 2012
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 150
  Trophy Points: 160
  ...hawana jipya,ukisha-sikia ya CCM-A ya CCM-B(CUF) ni marudio...
   
 5. S

  Seif al Islam JF-Expert Member

  #5
  Sep 11, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 2,158
  Likes Received: 141
  Trophy Points: 160
  Ni lazima tuelewe waandishi wanaiandikia jamii ya nama gani.kwa sasa jamii ya watanzania imechoka sana na kukatishwa tamaa na serikali dhaifu ya ccm .watanzania hawapendi tena kusikia stori za ccm na vibaraka. Wakekimsingi cuf wamejinasibisha kwa maneno na matendo kuwa ni vibaraka kama sio sehemu ya seikali dhaifu inayowatesa watanzania hivyo waandishi hawawezi kuiandika sana kwani watu hawataisoma.kimsingi watu wanataka kuisikia cdm ambayo kwa maneno na matendo inapambana vilivyo kuiondoa ccm madarakani na ndio hasa tumaini pekee la watanzania.cuf hawana ugomvi na waandishi bali watanzania wanaoandikiwa na waandishi
   
 6. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #6
  Sep 11, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,477
  Likes Received: 784
  Trophy Points: 280
  Mh. CUF ya waislam haya bana! Vyombo vya habari hususani magazeti yapo kibiashara unapoweka habari kuu inayohusu CUF gazeti linadoda, kwa hiyo CUF haina soko yaani haiuziki.
   
 7. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #7
  Sep 11, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Ukiwaalika waandishi wa habari siku hizi ,zama hizi za mkono mtupu haulambwi lazima uwape bahasha ya kaki.Kama wao CUF(viongozi) wanatafuna fedha za ruzuku peke yao kwa nini wasipigwe chini kurushwa hewani!!!
  JINO KWA JINO
   
 8. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #8
  Sep 11, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,751
  Likes Received: 6,022
  Trophy Points: 280
  Ulimsikia Makamu Mwenyekiti, CUF Taifa juzi pale Jangwani na wito wake kwa waislamu? Aliongea as if yuko kwenye Islamic Republic.
   
 9. h

  hans79 JF-Expert Member

  #9
  Sep 11, 2012
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  Si ndivyo hivyo,ikiandikwa habari ya serikali ni sawa umeandika za cuf.Tatizo li wapi wakati wao lao moja!
  Hao wameungana tatizo li wapi? Hebu chukua nukuu chache kiongozi wa CHADEMA kazoea kuongoza disco na pia haina hazina ya viongozi, habari kama hiyo iliandikwa siku si nyingi na magazeti kwa hiyo si habari mpya.
   
 10. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #10
  Sep 11, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Matoto ya KIKRISTO a.ka. CHADEMA mnatia kinyaa kwa post zenu. Hamjajifunza tuu? Kejeli za KIDINI kwa CUF hazisaidii kuijenga CHADEMA, wanaonufaika ni CCM! Hakuna muislam atajiunga CHADEMA wakati munawakashifu kila uchao! Tokeni nyuma ya vinanda enyi watu!
   
 11. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #11
  Sep 11, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,496
  Likes Received: 1,053
  Trophy Points: 280
  Wanachama wana akili sana wanajua hiki chama feki!!!! Kina mgombea uraisi wa maisha!!
   
 12. Las Mas Bobos

  Las Mas Bobos JF-Expert Member

  #12
  Sep 11, 2012
  Joined: Jun 15, 2012
  Messages: 993
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nani ale migagi Morogoro ilhali miwa ipi Kilombero na Mtibwa?

  Habari za CUF za zinatosha kuandikwa kwenye Al-Nuur na Zanzibar Leo
   
 13. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #13
  Sep 11, 2012
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,561
  Trophy Points: 280
  Mungu wangu wakatoliki mbna tunawaonewa sana nchi hii.. Hivi cardinal Pengo angekuwa na yeye upeo wake mdogo kama ponda, kundecha n.k, bila shaka tungekuwa na vita vya kidini.
   
 14. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #14
  Sep 11, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 8,999
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280
  TBC na UHURU watatangaza na kuandika.
   
 15. P

  Pure Number Member

  #15
  Sep 11, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani hii nenda google,,ni kwamba ccm ilikua chama cha kanisa na maaskof wa kikatoliki enzi za mkapa kwani walimuandaa wenyewe kua rais tokea anasoma ndanda karibu na ndanda mission,,na nadhani mnajua kuna watu watano ktk nchi wanaotoa maamuzi mazito ya nchi,hivyo mkatoliki mkapa akamweka pengo ktk hao watu watano kisirisiri ila kwa akili ya kawaida huezi jua,,then ndo maana mkapa wakati wake wakatoliki walitimiziwa mahitaji yao yoooote kwani ccm ilikua chini ya maaskofu na kuiunga mkono,,sasa chanzo cha ccm kupigwa vita ni pale jakaya alivoingia madarakani na akaona upuuzi alioufanya mkapa wa kumweka pengo ktk kutoa maamuzi mazito ya nchi,alicho fanya ni kumtoa na kumwambia "HAPA SI PAHALA PAKO,WEWE NENDA KANISANI NDO panakufaa"..sasa hilo ndo kosa jakaya kafanya ndo maana uongozi wake anafanyiwa njama nyingi ili aonekane hafai,ndo maana maaskofu wakaihama ccm kwa kuona haiwatimizii matakwa yao,wakahamia chadema,na kusema kwamba chadema ni chama cha maaskofu kisirisiri ni pale uchaguzi wa 2011 mkoani Iringa ambapo maaskofu walihimiza waumini wao kipigia cdm kura,lakini wale walioipa ccm wakaandikiwa barua za kufukuzwa dini kisa walimchagua muislan(jk)na sio askofu(slaa),,na kibaya zaidi udini ktk vyama umeanzshwa na cdm kwani pita kila kanisa utakuta maaskofu wana wahimiza waumini waipe cdm,,mfano mzuri ni kanisa katoliki pale ndanda mission,,hivyo na sisi tuseme kua kanisa ndo ofis za cdm???hivyo cdm kupata nguvu ni kutokana na nguvu zooote za maaskofu kuziamishia cdm toka ccm,,


  Si maneno yangu,ila explanations ndo zangu ,zaidi

  Vist on google TZCHURCH.com


  Yang ni hayo,hivyo sishangai kusikia kwamba waandish kuipendelea cdm kwani nao wote ni cdm..ndo maana wanaipa kipaumbele ktk magazeti,,,na nyinyi waislam msiogope kujitangaza wazi wazi kua ni CUF kama wakatoliki wanavyofanya katika makanisa yao hadi kufukuzwa dini ukienda against(eg Ndanda mission-mtwara)

  Thnx
   
 16. K

  Kikwebo JF-Expert Member

  #16
  Sep 11, 2012
  Joined: Aug 25, 2006
  Messages: 352
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35  Wewe ni mnafiki mkubwa..sio mwanachama wa CUF, umeandika kinafiki tu. CUF hawezi andika hivyo, simply kwa sababu anajua kwenye chama chake wapo wakristo..kina Mh! Sakaya, Mtatiro n.k. Kiufupi ulitaka ujenge hoja lakini imeonekana kama hoja yako ni dhaifu mno.

  Mgogoro wa CUF na waandishi wa habari ni wa muda mrefu. Hata miaka hiyo ya 2000 mpaka 2010 CUF hawakuwa wakiandikwa kwenye vyombo vya habari na ndio iliyopelekea kupigwa kwa waandishi miaka ile. Ajabu ni kuwa waandishi wakienda kwenye mikutano ya CUF badala ya kuandika positives za CUF wao wanaangalia udhaifu hata wakutunga na wanaupa publicity kubwa tu. Sababu kubwa CUF ilinasibishwa na UISLAMU na media owners wengi ni wakristo. Walikuwa wanadhani kama CUF ikiingia madarakani basi nchi itasilimishwa na dawa yake ilikuwa ni moja tu..kutoaipa publicity. Sasa kumezuka nyimbo mpya..CUF wameolewa na CCM hivyo sio wapinzani na then hakuna haja ya kuandika habari zao...lakini tutake tusitake..MFUMO kandamizi umeshika hataku mpaka kwenye media.
  Ni kipindi hiki ambacho hiyo inayodaiwa kuwa ni ndoa ilikuwa hata posa haijatoka. CCM wakiwatumia watu wao wa habari na huku IPP media na vyombo vyake vikiimba wimbo ule ule na wakiwa mstari wa mbele kuipa negative emage CUF. Vijana wengi humu harakati hizi za kimageuzi wanadhani zimeanzia CDM. Nimekuwa nikiangalia kwa uchungu kabisa jinsi wafuasi w CDM walivuokuwa wakipigwa vibaya na askari wetu kwa kutumia marungu na vitako vya bunduki, kwa kweli ni ukatili. Ila kwa taarifa tu CUF walifanyiwa makubwa MNO zaidi ya haya ambayo wanafanyiwa CDM, lakini publicity sifuri.
  Nakumbuka jamaa walikuwa wana sambaza habari zao kupitia mikanda ya video na ikawa inaangaliwa kwenye mabanda ya kuonyesha sinema ya mitaani, simply vyombo vya habari vilikuwa haviatoai habari zao.
  Kwegole, Muheza.

  Wewe ni mnafiki mkubwa..sio mwanachama wa CUF, umeandikakinafiki tu. CUF hawezi andika hivyo, simply kwa sababu anajua kwenye chamachake wapo wakristo..kina Mh! Sakaya, Mtatiro n.k. Kiufupi ulitaka ujenge hojalakini imeonekana kama hoja yako ni dhaifu mno.

  Mgogoro wa CUF na waandishi wa habari ni wa muda mrefu.Hata miaka hiyo ya 2000 mpaka 2010 CUF hawakuwa wakiandikwa kwenye vyombo vyahabari na ndio iliyopelekea kupigwa kwa waandishi miaka ile. Ajabu nikuwa waandishi wakienda kwenye mikutano ya CUF badala ya kuandikapositives za CUF wao wanaangalia udhaifu hata wakutunga na wanaupa publicitykubwa tu. Sababu kubwa CUF ilinasibishwa na UISLAMU na media ownerswengi ni wakristo. Walikuwa wanadhani kama CUF ikiingia madarakani basi nchiitasilimishwa na dawa yake ilikuwa ni moja tu..kutoaipa publicity. Sasakumezuka nyimbo mpya..CUF wameolewa na CCM hivyo sio wapinzani na then hakunahaja ya kuandika habari zao...lakini tutake tusitake..MFUMO kandamizi umeshikahataku mpaka kwenye media.
  Ni kipindi hiki ambacho hiyo inayodaiwa kuwa ni ndoailikuwa hata posa haijatoka. CCM wakiwatumia watu wao wa habari na huku IPPmedia na vyombo vyake vikiimba wimbo ule ule na wakiwa mstari wa mbelekuipa negative emage CUF. Vijana wengi humu harakati hizi za kimageuziwanadhani zimeanzia CDM. Nimekuwa nikiangalia kwa uchungu kabisa jinsiwafuasi w CDM walivuokuwa wakipigwa vibaya na askari wetu kwa kutumiamarungu na vitako vya bunduki, kwa kweli ni ukatili. Ila kwa taarifatu CUF walifanyiwa makubwa MNO zaidi ya haya ambayo wanafanyiwa CDM, lakinipublicity sifuri.
  Nakumbuka jamaa walikuwa wana sambaza habari zao kupitiamikanda ya video na ikawa inaangaliwa kwenye mabanda ya kuonyesha sinema yamitaani, simply vyombo vya habari vilikuwa haviatoai habari zao.
  Kwegole, Muheza.
   
 17. B

  Bontowar JF-Expert Member

  #17
  Sep 11, 2012
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 524
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
 18. C

  Concrete JF-Expert Member

  #18
  Sep 11, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 3,607
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Yaani hata gazeti lao la Fahamu halikuandika habari zao?

  Magazeti ya Uhuru, Mzalendo, Habari leo, Daily News, Alnoor nayo yamegoma?

  Vipi radio na TV kama vile kipeperushi cha magamba, Clauds, Imani Fm, Radio uhuru nk ?

  Hapa kuna haja ya kuunda tume huru kuchunguza maana kuna utata umegubika suala hili.
   
 19. C

  Concrete JF-Expert Member

  #19
  Sep 11, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 3,607
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Tafadhari sana, sahihisha maneno yako, Anaitwa Mtatiro Julius na ni muislam safi.
   
 20. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #20
  Sep 11, 2012
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Waandishi hawawezi kuandika kila mtu maana kama Nape akisha sema basi yatosha si lazima na Mtatiro aandikwe .Kubana matumizi ya pages bora kuachana nao kama ilivyo sasa .
   
Loading...