CRDB yakiri kuitaifisha Sekondari kufidia deni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CRDB yakiri kuitaifisha Sekondari kufidia deni

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by PayGod, Jan 11, 2011.

 1. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #1
  Jan 11, 2011
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  CRDB yakiri kuitaifisha Sekondari kufidia deni
  BENKI ya CRDB imekiri kuichukuwa Shule ya Sekondari ya Mkandawile kwa kufidia mkopo wake walioutoa kwa mmiliki wa shule hiyo.

  Ofisa uhusiano wa benki hiyo aliyejulikana kwa jina la Manel alisema shule hiyo kwa sasa ipo chini ya benki ya CRDB, lakini hawezi kuongelea lolote kuhusu shule hiyo kwa sababu taratibu zote ziko chini ya Bodi ya wakurugenzi.

  Inadaiwa mmiliki wa shule hiyo anadaiwa zaidi ya Sh 500 milioni.
  “Siwezi kuongelea chochote kile kuhusu suala la Shule ya Mkandawile kwa sababu mkurugenzi mkuu hajazungumzia lolote kuhusiana na shule hiyo,”alisema Manel.

  Shule ya Mkandawile iliyopo Majohe, Kata ya Chanika Wilaya ya Ilala ilichukuliwa na Benki ya CRDB tangu Oktoba mwaka jana, ambapo wanafunzi pamoja na walimu waliachwa kuachwa njiapanda bila ya kujua la kufanya.

  Hii ni wiki ya tatu sasa, baadhi ya walimu wa shule hiyo walihamishia makazi yao kwa aliyekuwa mmiliki wa shule Alfan Mkandawile ambaye naye baada ya shule hiyo kutokuwa mikononi mwake aliamua kutokomea kusikojulikana.

  Walimu wa shule hiyo, akiwemo Kaimu Mkuu wa Shule, Michael Sigore kwa nyakati tofauti walilidokeza gazeti hili kuwa wamdai kiongozi wa shule mishahara ya miezi saba na kwamba wenye nyumba walikopanga wamewafukuza ndio maana wamehamishia familia zao kwa Mkandawile  Huyu mkandawile alikuwa mwalimu mzuri wa chemistry form V na VI, na wakati anazisha hii shule ilikuwa nzuri sana, na sijuhi kwanini ameshindwa kulipa hili deni.
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Jan 11, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,157
  Trophy Points: 280
  Legal mortgage
   
 3. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #3
  Jan 11, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  Mikopo katika benki za Tanzania ni shughuli pevu, maderni yana riba kubwa mno
   
 4. Freestyler

  Freestyler Senior Member

  #4
  Jan 11, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 199
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nasikia alikuwa anaongeza wake tu!..Kalaa!
   
 5. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #5
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  .....this guy was a very good Chemistry teacher........! I remember those old days kule Pugu na Tambaza alikuwa anawajaza vijana kwelikweli aisee....!
   
 6. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #6
  Jan 11, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Yeah katika kupata mkopo nadhani mmiliki alilijua hilo!
   
 7. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #7
  Jan 11, 2011
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Duh, ngombe wa maskini hazai! Huyu Mkandawile alihangaika sana kuipata hiyo shule, alikuwa anfundisha tuition ya Chemistry usiku na mchana! Yaelekea alikosa tu elimu ya ujasiriamali
   
 8. Ngoreme

  Ngoreme Senior Member

  #8
  Jan 11, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 130
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  poor debt management
   
 9. shanature

  shanature JF-Expert Member

  #9
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 718
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  mwalimu na mikopo ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,ndio kazi yao,,,,wanaaminika sana na benki,,,na wakopeshaji wa mitaani mwisho wake ndio huo
   
 10. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #10
  Jan 11, 2011
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  • Rates kubwa za mabenk yetu,
  • Elimu ya ujasiliamali kutotolewa kwa wakopaji
  • bank nyingi kutowaelimisha wakopaji kabla ya kuwapa mikopo.
  Pole mkandawile, hiyo ndo mikopo, na hapa pia CRDB wamechangia sana COZ wanamtindo wa kuwakopesha watu kiwango kikubwa sana cha pesa bila kuangalia RISK ya hiyo biashara, kuna kipindi waliwakopesha vyama vya msingi na makampuni yanayohusika na kununua na kuhuza pamba kanda ya ziwa, mabilioni ya fedha na kulivyotokea mtikisiko wa kiuchumi dunia, ilibidi crdb wamtume moja ya wafanyakazi wao China, kwenda kutafuta masoko, kwa ajili ya pamba, na kilichokuja kuwaokoa ni JK kukubali kuwapa fedha kwa hiyo HARASA walioingia.
   
 11. Kiresua

  Kiresua JF-Expert Member

  #11
  Jan 11, 2011
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 1,202
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Yes I rem him too, he was brilliant Teacher, poor him!! I feel very sorry for him, hope things will finally work out in his favour!
   
 12. October

  October JF-Expert Member

  #12
  Jan 11, 2011
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 2,147
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Basi Benki Wamuajiri Huyo Mkandawire kuiendesha hiyo shule, Badala ya kuwakatili wananfunzi waliokuwa wakisoma hapo.
   
 13. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #13
  Jan 11, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Huyu Mkandawile amejitahidi kinoma na ndio watu wa kuwapa ruzuku. Natamani serikali ingemsaidia kama mwekezaji wa ndani na si kuwapa tumakampuni ya kuchimba madini tax holiday ambayo haina msingi wowote.
   
 14. A

  Adili JF-Expert Member

  #14
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 2,010
  Likes Received: 432
  Trophy Points: 180
  Wanajamvi mmeongea mengi. Tisa yote lakini la kumi ni swali - CRDB haikuwa na responsibility ya kuhakikisha shughuli za shule zinaendelea wakati ikirudisha hela zake? Hii ni on-going social undertaking implying that CRDB has a moral and social responsibility to oversee the continued functioning of the school.
   
 15. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #15
  Jan 11, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Mkuu - CRDB haiwezi kuendesha shughuli zote wanakokopesha - sio jukumu lao. Wao ni bankers.
   
 16. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #16
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,441
  Likes Received: 5,693
  Trophy Points: 280
  mi nilijua tu huyu MNGONI NI KWELI KICHWA KIZURI CHA CHEMISTRY LAKINI ALIKUWA TAPELI MKUBWA
  HATA MKOPO ALICHEZA DILI NA WAHUNI FULAN PALE CRDB WAKIFWATILIA WATAONDOKA NA WENGI
  KIJANA YUKO MBWENI KAJIHIFADHI LAKINI ALICHOFANYA SI UUNGWANA ....NAMKUMBUKA AKIWA DARASANI KAMA UNASOMA AZANIA ANAITA AZA BOY,PUGU BOY NK..ANYWAY HII LIWE FUNDISHO KUKIMBILIA SHULE ZA BEI POA NA MAZARA YAKE..ANYWAY KUKAMATIKA NI RAHSI LAKINI NI AIBU SANA KWA WALIMU WENGINE WENYE MAWAZO YA KUFUNGUA SHULE KAMA YAKE
   
 17. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #17
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,441
  Likes Received: 5,693
  Trophy Points: 280
  tusilalamikie sana crdb, unaweza kukuta alipeleka mradi wa kuchimba madini kama kiwira shule ikawa top up ya mafao yake mwisho wa siku wanasalia na majengo..polen sana
   
 18. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #18
  Jan 11, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  millioni 500 ,for school project,mh huu ni wizi mtu,unless alikuwa anataka kujenga lab and college or mkandawile university.kwani Darasa moja kulijenga ni around 8million,sasa madarasa 10 it will be 80mil,kumbuka tayari alikuwa na shule ambayo ndiyo ilitumika kuwa collateral
  hapa ilikuwa imesukuwa dili kati ya mkandawilie na crdb loan officers+branch manager,na kwa kuwa mkandawile ni smart sana and a risk taker hakujali maslahi ya watoto na shule akachukua pesa akijua kabisa watalichukua jengo ambalo thamani yake ni ndogo.hapa inabidi serikali ifuatilie kwa makini.
  namkumbuka enzi zile akipiga day waka ktk kufundisha chemistry for A levels
   
 19. Wa Kwilondo

  Wa Kwilondo JF-Expert Member

  #19
  Jan 12, 2011
  Joined: Sep 15, 2007
  Messages: 1,083
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  mismanagement tu!!!, yeye ndiyo alikuwa director ,finance yeye na mkewe unadhani hesabu zitakaa sawa kweli?...wanajamii real situation jamaa kwa sasa kachoka kweli hana kitu kabisa anapiga mizinga tu isitoshe anahitaji tiba ya saikolojia la sivyo atakuwa chizi.:smile-big:
   
 20. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #20
  Jan 12, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  sasa siwangemwachia shule waiendeshe chni ya uongozi wa crdb hela wachukue au kama kawaida yao wanataka kupiga mnada tu
   
Loading...