CRDB: The most Inefficient Bank of all times

CRDB: The most Inefficient Bank of all times

Waboreshe huduma! inashangaza saa mbili na nusu wanafungua milango halafu wateja wakiingia unakuta mfano tellers ndio kwanza hata hawajawa tayari kwenye madirisha yao kuhudumia wateja, tena wanachukua hata dakika ishirini ndio wanaanza kutoa huduma
CRDB Kwa sasa huduma zao ni hovyo sana. Bora NMB pamoja na kuwa na wateja wengi wanajitahidi.

Sent from my GT-I9500 using JamiiForums mobile app
 
Nafikiri haya mabenki wakati mwingine wanaajiri incompetence staff. Kama mwezi hivi nilikwenda kufungua account ya kampuni pale CRDB Holland branch. Nikapewa checklist na afisa moja mdada. Nilivyorudi nikaelekezwa kwa mwingine, naye kanipa za kwake na kudai yule dada alikosea.
Kwa jinsi unaweza kuona namna ambayo mteja anapata usumbufu usio na maana.
 
Bank binafsi unataka serikali ibadilishe management? Hahahha
Jamaa bado ana tafsiri ya Co-operative and Rural Develepment Bank ya Nyerere; hana taarifa kwamba hata hilo "neno" CRDB siku hizi halina tafsiri yoyote; ni meaningless.
 
CRDB Kwa sasa huduma zao ni hovyo sana. Bora NMB pamoja na kuwa na wateja wengi wanajitahidi.

Sent from my GT-I9500 using JamiiForums mobile app
Top management ya NMB ni "ngozi nyeupe".
 
Slogan ya CRDB inabidi ibalike kutoka Bank that listens to bank that listened. Hii bank iliwajali wateja miaka 2000, sio sasa. Kimei umesikia mapovu ya wateja wako?
 
Mkuu mara ya mwisho kupata huduma NMB ilikuwa lini?... kwa mtazamo wangu, ni heri hiyo CRDB mara mia kuliko NMB...huduma mbovu sana
 
  1. Loss of Direction, Very unfriendly Environment
Ninaandika kupata maoni yenu juu ya sekta ya fedha, particularly contribution mbovu ya CRDB katika utoaji wa huduma za kibenki.

Hapa nazungumzia huduma simple na ya moja kwa moja ya kuchukua na kutoa fedha. Mimi ni mteja wa branch ya kijitonyama. Uzoefu wangu ni muda wanaotumia kuhudumia wateja na ufanisi wa matela. Wahudumu wako very slow, na ukiwauliza siku zote watakwambia system yao ama iko down, ama iko slow.

Lakini pamoja na hayo wahudumu hawa wanaingiza mambo yasiyo ya kikazi kwama vile kuongea na simu katikati ya huduma, kuchat ama kutuma messages wakati mteja akiwa dirishani kwao, kuongeleshana na watendaji waenzao ndani ya madirisha yao wakitokea milango ya ndani, yaani usumbufu ni mkubwa sana. haijalishi umefika saa ngapi, haijalishi siku gani ya juma, wala haijalishi umefuata huduma gani kila kitu ni slow kuliko unavyoweza kufikiri.

Naamini hii ni taswira ya kawaida sana, hata ukiwa kwenye foleni kila mteja analalamika na hakuna improvement. kinachonishangaza ni namba ambavyo si bodi wala serikali ambaye ni mdau anayeonekana kusumbuliwa na hii lack of efficiency na incompetence ya timu yao.

Kwa sasa watu wafanyabiashara wengi sana wanategemea benki za nje, ambazo ni ndogo tu kama baclays, FNB, stanbic kupitishia transactions zao, jambo ambalo halionekani kuwasumbua viongozi wa benki hii, zaidi ya kulalamikia serikali kuhamishai hela zake BOT.

2.Nini Kifanyike
Tunaomba Bodi na serikali kuchukua hatua za haraka ili kuinusuru banki hii. Ni muda sasa kufanyike yale yaliyofanywa na BOT ya kuiondoa management nzima na safu zima ya wakurugenzi manake wanachofanya ni kujali maslahi yao na siyo kazi yao.

Management iwapatie wafanyakazi mafunzo muafaka ili kuboresha utendaji wao. Wafanyakazi wananuna masaa yote, they look very tired and exosted, na hawana content inapowahitaji kuuza huduma.
Nawasilisha

Tanzania kuna benki zaidi ya 30 zenye huduma Nzuri kuliko hiyo kwani kuwa na account huko ni lazma hama hamia kwenye benki zenye akili
 
Ukitaka kua crdba nizaid ya mbomu angalia his yao tangu wameanza kuuza haijawah fika 500. Jambo tusilo lijuwa kama ucku wa gza. Crdba plc kiza nikinene na kama unataka kujuwa ukweli chef Kimei apumzike. Hiyo siku itakuwa kiama.
 
crdb wanajitahidi sana ukilinganisha na wakongwe nbc na ndugu yake Nmb huku ni shidaaaaaa
kinachonichekeshaga ni ukitembelea makao makuu ya nmb, mule ndani utakuta wamejenga vi garden yaani utazani wapo paradiso hahaha..vi garden vina ramani na art ya ukweli yaan hata kama umeingia mule una buku mfukoni utatembea mwendo wa kimilonea......hahahahaa, sitasahau ile interview
 
Hawahitaji kusaidika maana hata pande za huku mambo ni hayo hayo. Unaweza simama kwenye foleni dk za kutosha na foleni haisogei na hakuna mhudumu anayekuleza kuwa the so called system iko down! Wanaboa sana kwa kweli hawaelewi tu wanavyotupotezea muda!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo ni kuwa,wateja wa Benki Tanzania hawajaweza kutumia njia mbalimbali za kufanya money transfer,kama vile sim banking na n.k.Bado tunapenda kajazana kwenye mistari.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom