- Loss of Direction, Very unfriendly Environment
Hapa nazungumzia huduma simple na ya moja kwa moja ya kuchukua na kutoa fedha. Mimi ni mteja wa branch ya kijitonyama. Uzoefu wangu ni muda wanaotumia kuhudumia wateja na ufanisi wa matela. Wahudumu wako very slow, na ukiwauliza siku zote watakwambia system yao ama iko down, ama iko slow.
Lakini pamoja na hayo wahudumu hawa wanaingiza mambo yasiyo ya kikazi kwama vile kuongea na simu katikati ya huduma, kuchat ama kutuma messages wakati mteja akiwa dirishani kwao, kuongeleshana na watendaji waenzao ndani ya madirisha yao wakitokea milango ya ndani, yaani usumbufu ni mkubwa sana. haijalishi umefika saa ngapi, haijalishi siku gani ya juma, wala haijalishi umefuata huduma gani kila kitu ni slow kuliko unavyoweza kufikiri.
Naamini hii ni taswira ya kawaida sana, hata ukiwa kwenye foleni kila mteja analalamika na hakuna improvement. kinachonishangaza ni namba ambavyo si bodi wala serikali ambaye ni mdau anayeonekana kusumbuliwa na hii lack of efficiency na incompetence ya timu yao.
Kwa sasa watu wafanyabiashara wengi sana wanategemea benki za nje, ambazo ni ndogo tu kama baclays, FNB, stanbic kupitishia transactions zao, jambo ambalo halionekani kuwasumbua viongozi wa benki hii, zaidi ya kulalamikia serikali kuhamishai hela zake BOT.
2.Nini Kifanyike
Tunaomba Bodi na serikali kuchukua hatua za haraka ili kuinusuru banki hii. Ni muda sasa kufanyike yale yaliyofanywa na BOT ya kuiondoa management nzima na safu zima ya wakurugenzi manake wanachofanya ni kujali maslahi yao na siyo kazi yao.
Management iwapatie wafanyakazi mafunzo muafaka ili kuboresha utendaji wao. Wafanyakazi wananuna masaa yote, they look very tired and exosted, na hawana content inapowahitaji kuuza huduma.
Nawasilisha