Sio kweli kwamba hizo pesa walizotoa CRDB ni gawio, ni pesa ambazo walipewa ili kuinusuru miaka ya 90, sasa baada ya kuona wanaweza kujiendesha kwa faida imebidi wazichukue na sio gawio kama mpokeaji alivyokuwa anasema.Inasikitisha sana kuona kuwa bado Watanzania tuna safari ndefu kwenye matumizi ya mitandao kuwasilisha maoni yetu. Hivi mtu anaanza kwa kusema kuwa CRDB Bank ni most inefficient bank of the all time.
Hivi hii benki ambayo tangu ilipo binafsishwa imekua ikipata faida mfululizo hadi kufikia kuwa benki ya inayoongoza kwa kuwa na largest balance sheet nchi hii unaweza kuiita ni inefficient bank of all times ? Hivi benki ambayo imekua benki ya kwanza nchini inayoongozwa na wazalendo kuvuka mipaka na kufungua tawi nje ya nchi unaweza kuiita ni inefficient bank of all times?
Hivi benki ambayo imeajili takribani wafanyakazi wazawa elfu 3 na kutoa fursa ya biashara kwa mawakala zaidi ya 2500 unaweza kuita inefficient bank of all times? Hivi benki ambayo imefika mikoa yote nchini na kuchochea financial inclusion unaweza kuita inefficient bank of all times? Hivi benki ambayo imetunikiwa tuzo ya SuperBrand tangu mwaka 2009 unaweza kuita inefficient bank of all times?
Hivi benki ambayo imekua benki ya kwanza nchini kupata tuzo ya Euro Money unaweza kuita inefficient bank of all times? Hivi benki ambayo mwaka huu tu imepata tuzo ya kuwa benki bora kwa upande wa SME na kurudisha faida kwa jamii unaweza kuita inefficient bank of all times?. Tuachane na hayo mana orodha ni ndefu ya mafanikio ya benki hii.
Lakini kubwa zaidi ni mtoa hoja ameonyesha kuwa na chuki binafsi kwa uongozi wa benki kwani mafaniko ya Benki ya CRDB huwezi kuyaweka mbali na uongozi wake chini ya Dr. Kimei ambae wakati anafika benki ilikua katika hali mbaya na kwa kushirikiana na wenzake katika uongozi wameweza kuifanya benki hii kuwa mfano wa kuigwa kwa taasisi ambazo zinaongozwa na wazawa.
Naamini kabisa haya yote yamekuja baada ya kuona serikali imefurahishwa mchango wa Benki ya CRDB na hasa baada ya kupokea gawio la hisa la bilioni 19.5. Inafahamika kwamba benki ya NMB walitumia ushawishi gawio lao la hisa kufanya Mheshimiwa Raisi awapigie debe kwenye uzinduzi wa tawi lao la Mtwara.
Hivo kuona uongozi wa Benki ya CRDB kwa kushirikiana na DANIDA kukabidhi gawio la hisa kwa serikali imewakwaza hawa watu wa NMB na kuanza kampeni hizi chafu dhidi ya uongozi wa Benki ya CRDB. Nafikiri mabenki yanapaswa kushindana kutoa huduma bora na sio kutumia mitandao ya kijamii kuchafuana pasipo hoja za msingi.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app