Habari wakuu,
Nimetafuta jukwaa la fedha au malalamiko sijaliona, so kama haifit hapa mnisamehe.
Iko hivi, jananimekwenda kulipa ada kwaajili ya kijana wangu anaanza Kidato cha kwanza (shule ipo Dodoma). Sakata lilianzia shuleni, hawataki malipo ambayo hayajapitia dirishani kwa benki.
Yaani lazima uwe na pay slip ya bank. So, hauwezi kufanya mobile payment wala internet banking. Hii ikawa kero kubwa sana maana kwa ulimwengu huu ulivyo sipiiiidiiii haifai watu hasa taasisi kubaki analojia.
Kufika bank (CRDB tawi lipo Moro), nikaambiwa, kila transaction ya kuweka pesa kwenye akaounti ya hiyo shule natakiwa nilipie charge ya Tshs 1,180.00 Hii kwangu ilikuwa na mpya, ya ajabu na wizi. Unaanzaje kutozwa fedha kwa kudeposit? Sijawahi kuiona popote dunia nzima
CRDB acheni hizi mambo, mnatuibia, hakuna gharama ya kudeposit
Ni hayo tu