CRDB Mnatuibia, acheni

CRDB Mnatuibia, acheni

kuna benki moja mpaka leo nguvu ya kuweka pesa imekata tamaa.nilikuwa kila siku naweka elfu 10 mpaka ishirini ndicho kiwango kupitia njia zote za kibenki mwaka mzima.mwisho wa mwaka naenda kuangalia salio nakuta laki tatu .nili %€~€%>?€!?,.
 
hili linekuwa libenki la kijizi, mara liwachome wateja wake kwa majambazi, mara liwachome wateja kwa polisi yaani kwa sasa nishida tupu!
 
Hawa jamaa mi hata siwaelewagi, kuna kipindi jamaa alikuwa ananidai 20,000/= akanipa akaunti ya crrdb nimuingizie, baadae jamaa ananipigia mbona umeingiza 10,000/= na kipindi kile utandawazi hakuna ilinichukua miezi 6 kuja kumuonesha ili bps
 
Hawa jamaa mi hata siwaelewagi, kuna kipindi jamaa alikuwa ananidai 20,000/= akanipa akaunti ya crrdb nimuingizie, baadae jamaa ananipigia mbona umeingiza 10,000/= na kipindi kile utandawazi hakuna ilinichukua miezi 6 kuja kumuonesha ili bps
Dah kuna watu "wakatili" duniani...
Yaani elfu 20 mpaka umuingizie benki!!.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani mwenye shule amekwambia makubaliano aliyonayo na CRDB-Bank PLC? Ingawa unataka kuonesha kuwa umefikia kiwango cha digital, ukweli ni kuwa bado uko analogia, tena sana. Wewe lipa tu karo ya mwanao asome badala ya kulalamikia vijimambo vidogo vidogo. Benki zote hutoza bank charges kwa huduma wanazotoa, na hii hulingana na makubaliano baina ya benki husika na wateja wake. Kwanza inaonekana ni mara yako ya kwanza kusomesha mtoto shule binafsi, na umefanya hivyo reluctantly.
Dogo nimemlipia ada kupitia NMB hawana hiyo takataka. CRDB wana hako kamchezo.
 
Hii benki huwa naishiaga kusajili ac tu fedha ziko Mpesa
 
kuna benki moja mpaka leo nguvu ya kuweka pesa imekata tamaa.nilikuwa kila siku naweka elfu 10 mpaka ishirini ndicho kiwango kupitia njia zote za kibenki mwaka mzima.mwisho wa mwaka naenda kuangalia salio nakuta laki tatu .nili %€~€%>?€!?,.
Duuuuh!!
 
Hii inaitwa standard law ambapo sheria inapoundwa mteja hakuwepo ila inatakiwa uifuate hiyo Sheria japo hukuhusishwa kuitunga!
Mfano, nyuma ya tiketi za magari zimeandikwa nyuma kuwa tiketi ikishakatwa fedha hairudishwi kwa namna yeyote
 
Siku hizi benki ni wezi tofauti na makubaliano eti leo kila transaction utakayofanya VAT ni juu yako badala ile hela uliyowalipa kwenye transaction ndiyo wagawane na serikali tunakatwa sisi
Mwisho wa mwezi ukifika wanakata hela yao pia vat unaktwa tena
Card fees wanakata hela yako na vat ni juu yetu
Monthky fees wanakata hela yao na vat juu yetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante sana Sophist
ni kweli kabisa ni mara yangu ya kwanza kusomesha mtoto shule binafsi nikiwa tanzania, lakini that should not be a problem. Pili, si jambo rahisi mimi kujua makubaliano ya mwenye bank na mwenye shule, lakini ninachojua, hakuna sehemu wala taasisi ya fedha inayolipisha deposits. kimsingi wanapaswa wakushukuru kwa kuwapelekea fedha. naamini unaweza kujifunza kuhusu hili.
mwisho ingawa si kwa umuhimu, kuwa digital siyo hiyari, usisubiri mpaka teknolojia ikulazimishe kuifuata, huduma za fedha kiganjani mwako.
Jumapili njema boss
CRDB wana hako katabia. Nilipokuwa masomoni, nikienda kulipa ada kiasi chochote kile lazima nitoe 1,800 cha juu.
 
Aione
-branch manager morogoro CRDB
-zonal manager CRDB
-new managing director CRDB
 
Pili, si jambo rahisi mimi kujua makubaliano ya mwenye bank na mwenye shule, lakini ninachojua, hakuna sehemu wala taasisi ya fedha inayolipisha deposits.
Umejibu vizuri ahsante pia.
1. Kwa kawaida, shule ambazo ni credible huingia mikataba na benki husika kupokea pesa za ada kutoka kwa wazazi/walezi. Actually, CRDB wana software mahsusi kwa kila shule mshirika wake kiasi kwamba mzazi halipi pesa za karo tu bali pia na kuonesha sababu ya malipo, jina la mtoto na darasa analosoma. Kumbukumbu zote hizo zinakuwa kiganjani mwako ukifuata utaratibu (software).
2. Dhana ya ku-deposit pesa ni pale unapoweka kiasi husika kwenye akaunti yako. Siyo pale unapotafuta huduma ya kusafirisha malipo/pesa zako kupitia benki kwa sababu yoyoyte ile. Ulichotaka kufanya siyo deposit bali ni kupata huduma ya kutuma malipo ya karo ya shule kwa ajili ya mtoto wako kupitia benki (CRDB-Bank PLC). Kupata huduma za kila aina, mahali popote pale, sharti kulipiwa.
 
JPM afukuzeaziri wa fedha, kwani hajui hayo yanatendeka?

Habari wakuu,
Nimetafuta jukwaa la fedha au malalamiko sijaliona, so kama haifit hapa mnisamehe.

Iko hivi, jananimekwenda kulipa ada kwaajili ya kijana wangu anaanza Kidato cha kwanza (shule ipo Dodoma). Sakata lilianzia shuleni, hawataki malipo ambayo hayajapitia dirishani kwa benki. Yaani lazima uwe na pay slip ya bank. So, hauwezi kufanya mobile payment wala internet banking. Hii ikawa kero kubwa sana maana kwa ulimwengu huu ulivyo sipiiiidiiii haifai watu hasa taasisi kubaki analojia.
Kufika bank (CRDB tawi lipo Moro), nikaambiwa, kila transaction ya kuweka pesa kwenye akaounti ya hiyo shule natakiwa nilipie charge ya Tshs 1,180.00 Hii kwangu ilikuwa na mpya, ya ajabu na wizi. Unaanzaje kutozwa fedha kwa kudeposit? Sijawahi kuiona popote dunia nzima
CRDB acheni hizi mambo, mnatuibia, hakuna gharama ya kudeposit
Ni hayo tu
 
Back
Top Bottom