CalvinPower
JF-Expert Member
- Nov 25, 2008
- 1,628
- 990
Haya ndiyo yaliyonikuta kutoka CRDB bank, wasichukie ila wajaribu kuelewa kuwa tukiandika na kuanika mabaya tunayoyapata kutoka kwa Service Desk, Customer Care teams, Customer Service Reps ndio itakayopelekea wao kujirekebisha na kutoa huduma bora hapo baadae.
Matatizo kama haya huwa tunayapata kutoka yale makampuni yenye wateja wengi kuliko yale yenye wateja wachache.
Nimekuwa na tatizo na visa card yangu ya bank kwa mda mrefu, nilikuwa nashindwa kufanya manunuzi online, nashindwa ku-link card yangu na paypal na sio kama mimi ni mgeni katika hili. hivyo usije niambia process za kulink ni hizi na hizi.
Ok nielezee tu baada ya kushindwa kuitumia card yangu online nikapiga simu kwenye number ambazo zipo kwenye card yangu ( contact customer care ) kuelezea tatizo langu nilijaribu kujielezea kwa umakini sana kuhusu tatizo langu na yeye akanijibu kuwa anachukua maelezo yangu na anayafikisha kwa idara inayohusika na nitajulishwa kwa njia ya sms punde tatizo langu litakapotatuliwa.
Nikamwambia kama anaweza akanipa namba ya hiyo idara ili niwaelezee hili tatito, akanijibu kwa ufupi tu hapana na akakata simu.
Nikapiga tena ikapolelewa na supervisor mwingine, ambae aliweza kutatua tatizo langu ndani ya dakika 3 tu, aliniambia subiri usikate simu na akaniweka on hold kidogo nafkiri labda alikuwa anawasiliana na hiyo idara, alirudi online na kuchukua maelezo ya ziada na akaniambia account yangu haina hela hivyo niongeze halafu nijaribu kufanya manunuzi tena online pamoja na ku link card yangu na paypal.
Baada ya kuweka kiasi fulani cha hela mambo yakawa sawa na nililipia service ya dola xx na ikakubali na hapohapo nikapata sms ya muamala nilioufanya kutoka crdb bank.
Nikajaribu ku link card yangu na paypal nayo ikakubali. Baada ya siku nikapata tena muamala kutoka crdb ukionyesha kuwa nimefanya muamala na kama sitambui huo muamala nipige simu ili nieleweshwe, nikapiga simu na wakanieleza kuwa ule muamala nilioufanya ndio umekamilishwa leo na wamenitumia hiyo sms kunijulisha na huo ndo mchanganuo katika Tsh, nikawaambia ok ila mbona muamala umekuja kwa mfumo wa USD na sio Tsh? wakasema hiyo ni Tsh na sio USD.
Basi nikawaelewa na kuwashukuru wakaniuliza kama nina swali lingine nikawaambia sina, Cha kushangaza nilipotaka kufanya manunuzi mengine tena card yangu ikakataliwa kama ilivyokuwa awali, japo kulikuwa na balance kubwa tu ila ilikuwa inakataliwa, nikaongeza hela, hali ikawa hivyo hivyo.
Safari hii nikaamua kwenda moja kwa moja kwenye tawi langu na kuijaribu card yangu kwenye ATM, napo ikagoma ikaleta ujumbe unaosomeka "sorry this transaction has declined", nikaingia ndani kwenye desk customer service, wakasema nijaze form halafu nilipie sh 5,900/= ili wa-reset password yangu, nikaambiwa baada ya hapo kilakitu kitakuwa sawa.
Baada ya kufanya hayo yote nikaambiwa nitapata sms kwenye simu halafu niingie kwenye ATM niweke password mpya nitakayotumiwa, sikupata sms wala nini na muda ukawa unazidi kwenda almost 2hrs, wakasema nijaribu hivyohivyo kwenye ATM na nikiulizwa password niweke 1234, nikafanya hivyo lakini bado nikawa napata ujumbe "sorry this transaction has declined".
Nikarudi tena ndani na yule alienihudumia mara ya kwanza akawa anamuhudumia mteja mwingine aliekuwa pembeni yake akaniuliza nikamwambia ujumbe ninaoupata kwenye ATM.
Akachukua card yangu na kuikagua kwenye computer yake na kunieleza kuwa card yangu imefungiwa hivyo lazima nijaze form ili waweze kuifungua,
nilifanya kama alivyonielekeza na akaniambia nimwone meneja ili aweze kuidhinisha, muda ukazidi kwenda na baada ya lisaa wakasema niende nirudi tena baada ya siku tatu.
Nilivyorudi tena baada ya siku tatu sikumkuta tena yuke meneja nikamkuta meneja mwingine, nikaanza kumwelewesha pale tulipoishia kabla ya yeye. achachukua card yangu na kuikagua tena kwenye pc yake, akasema card yangu imefungiwa walihisi ilitumika online pasipo idhini yangu tarehe zile ambazo mimi nilifanya muamala.
Nikamwambia ni mimi nilifanya huo muamala na kwanini waliifunga wakati sikulalamila?
Kwa ushauri wake akasema nijaze form ili waweze kuifungua na wakachukua namba yangu ya simu ili wanijulishe. Nikawauliza labda itachukua muda gani ili niweze kujua na nikiona siku zimepita niweze kuja tena, akaniambia we nenda tu tutakujulisha.
Cha kunishangaza wiki mbili zimepita bila kupata sms kutoka kwao, nikaamua kwenda tena kwenye tawi langu na nikamkuta yule meneja wa mwanzo kabla ya huyu alieniambia nisubiri sms kutoka crdb. Nikamkumbusha pale tulipoishia. Akasema nijaze form ili nipate card mpya, safari hii nikawa mkali nikamwambia wiki mbili zilizopita nilikuja nikakukosa ila nilimkuta meneja mwingine nae akasema nijaze form nikajaza nikaambiwa nisubiri nitatumiwa sms kutoka crdb, lakini ni wiki mbili sasa sijapata sms kutoka crdb ndo nimeamua kuja tena wewe unaniambia nijaze tena form nipate card mpya mbona kila nikija mnasema nijaze tu form hii ni safari ya tatu najaza form, na nikijaza kwaajili ya card mpya nayo nitaambiwa nisubiri tena wiki mbili, mbona siwaelewi?
Nikawauliza hivi ningekuwa na mamilioni kama Reginald Mengi ningekuwa nasumbuliwa hivi?
Nikawaambia Rais anaposema watu hawafanyi kazi hajakosea, mshahara wako unatoka kwa wateja kama sisi, sasa mimi nikifunga account yangu na mwingine kwa maudhi kama haya akafunga, huoni kuwa mtapoteza wateja na hivyo kupelekea kwenu kutoona hela? Halafu mtasema Magufuli kabana sana hakuna hela, kumbe ni ninyi hamtaki kufanya kazi.
Basi kwa maneno hayo akainua simu yake ya mezani na kuongea na idara inayohusiana na matatizo yangu na kisha kuniambia nisubiri kidogo. Kwa kuwa leo ilikuwa siku ya jmosi nikaona niwape muda, nikawaambia sina muda wa kusubiri naenda nitarudi jtatu na kama hawatakuwa na muafaka na card yangu basi nachukua fedha zangu zote nafunga account, nikaondoka.