rkgx
Senior Member
- Nov 30, 2013
- 100
- 80
Natumia huduma ya kadi kufanya manunuzi online na kwa muda mrefu nimekuwa nikinunua vitu online kupitia paypal (gateway) lakini huwa inatokea muda mwingine nikanunua kitu halafu seller akashindwa kuleta nafungu kesi paypal na baadaye seller anaamua kunilipa (refund) lakini cha ajabu nikishalipwa na seller hela yangu huwa hairudi kwenye akaunti. Na mara nyingi nikirudishiwa hela paypal nao huwa wananitumia email kwamba nimerudishiwa hela na kwakuwa huwa nanunua kwa kutumia CRDB Visa Card hela yangu huwa inarudi kwenye akaunti yangu.
Hivi karibuni yapata kama mwezi mmoja na siku kadhaa hivi nilifanya transaction online ya $139.99 ambayo kwa hela ya kibongo ni kama 316,632 Tsh. Baadaye seller akasema kwamba ameishiwa na stock kwahiyo atarudisha hela yangu ili baadaye akiwa na bidhaa stock atanitaarifu nilipie tena. Baada ya siku tatu seller akanitumia meseji kwamba ameni-refund tayari na baadaye paypal wakathibitisha kwamba nimerudishiwa hela na imerudi kwenye akaunti yangu. Niliwasiliana na watu wa customercare kwa email nikawaambia juu ya suala hilo nao wakawasilisha kwenye Idara ya Refunds, baada ya hapo nikapokea email kutoka kwao kwamba niwatumie receipt ya refund hiyo kwa pdf nikafanya hivyo na nikawatumia na refunds zangu za nyuma ambazo kwa kipindi chote sikuwahi ziona kwenye bank statement yangu kama zimerudi.
Sasa cha ajabu tangu niwatumie hizo receipt hadi leo ni mwezi mzima hakuna mtu yeyote aliyetoa jibu kwamba nini kinaendelea, nimewaandikia emails zaidi ya saba hawajibu na nimewasiliana na watu wa customercare wanasema tatizo lako tumeliwasilisha wanalishughulikia. Lakini cha ajabu kwa kipindi hiki chote ninachosubiri kupata majibu kutoka kwao kuna harufu ya wizi naiona. Kuna thread kama hii niliisoma hapa kwenye jukwaa inaelezea jinsi wanavyoshirikiana kuzila hizo pesa za refunds kwa kugawana kuanzia kwa wakubwa wa vitengo hivyo ndio maana kwenye suala langu la kudai refunds zangu kuna kigugumizi kikubwa.
Najua kuna wengine wanaweza kuwa na experience kama hii nawaombeni mjitokeze hapa maana nafikiri hii siyo misingi bora ya utoaji huduma especially kwa Benki kubwa kama CRDB ambayo wateja wengi tunaiamini. Inaweza kuwa kuna watu wachache wanafanya hizo mambo na kuichafua Bank lakini nashangaa hata watu wa customer service nao kutojibu querry za wateja ni maadili ya kazi zao?