Mkuu nimecheka hadi machozi.Dah ilikua form 2 nilisema kwa cube members wangu kuna kiatu cha jamaa mmoja Wa form six kinanuka ,wakaenda kunisemea ,kumbe jamaa alikua mtabe na anaheshimika kindakindaki ,muda Wa jioni unaingia kaanza kunitafuta dormitory ,nlienda kulala juu ya mti mpaka asubuhi nikanyoosha kwa headmaster kwa usalama wangu ,asubuhi naona jamaa anakuja kwenye office ya headmaster huku anapiga mluzi halafu katabasamu
Headmaster mwenyewe anazima fegi kwa jamaa akaniombea msamaha ,kweli jamaa akawa kaka wangu Wa shule hakuna aliyenionea Tena ,sema ndio hivyo kumfulia, anakupa sh 50 umletee mkate,soda na change ibaki ,ukiletewa nido sijui na blueband unanyoosha moja kwa moja kwake
nakumbuka mwaka 2005 wkt npo kidato cha 4 ktk shule inaitwa Bismarck ipo mkoan Mwanza nlizushiwaga natembea na mwalim wang wa masomo ya biashara eti kisa kila pepa ya Book keeping na Commerce nlikua naongoza mim, pia nakumbuka mwaka 2007 wkt npo kidato cha 6 ktk shule ya wavulana ya Azania nlimpgaga ngum dereva wa daladala ya Temeke/Muhimbil baada ya mwanafunz wa kidato cha kwanza kusukumwa na kufarik, yan iyo fujo yake haikua ndogo kwa maana wanafunz wa Azania 2lizagaa ktk vitua shaz kufanya fujo
Azania nadhani 2009 kuna dogo wa o level aligongwa akafa sasa zilikuwa zikipita daladala za tandika - muhimbili konda anashushwa ana kula kichapo basi ikawa fujo balaa sasa o level wanavaa suruali za blue kama za makondakta kuna dogo mmoja katika purukushani akachukua koti la konda akalivaa bila kujua katokelezea kama konda na suruali yake basi ile kajichanganya wakashindwa kumtambua ndani ya muda mfupi akale krebu za kutosha ile kaja kuvua kabaki na t shirt ya shule tayari ana nundu za kutosha
Kuna jamaa alikua kani udi kidato Shule moja kule iringa, maarufu kama Nyomo guy yani ni mtemiiii balaaa, pande moja la mtu, na mm that time ndo kwanza Nipo form 1 alinishika kola ya shirt yangu, mm bila kumfaham nkampayukiaa “we kaka vipii” aisee alinikata jicho balaaa. Nkanyweaa bas kuja kufatiliaa kumbe alikua anantafuta anifahamu kisa bwenini kwao huko natajwaa na wahuni kila leoo
Nilkua na matatzo ya kusikia, bas siku wkt natembea DH npo stejini kule juu akatokea mvulana mmoja maskini aliniita akachokaa mm sina Habar. Nxt day naingia class nasikia naitwa Binti kiziwi nilmtafuta alientunga hilo Jina kuja kumpataaa 🤣🤣🤣 namkuta jamaa mwenyewe mweusi tiiii nkamwambia acha dharau we black mambo, alinuna mwaka mzima but tukaja kua good friends ad sasa hivi.
A level Nilhama Shule from Moshi to Zoo (iringa girls) siku ya kwanza nareport dadeki nakuta form6 wanachapwaa stick za maana Yan wadada wanagalagala chini aisee nilmshka mama mkono nakazana kuhama na hii Shule, aiseee cjawah kuenjoy life ya pale zoo hata kduchuu.
Kuna siku kipindi cha mfungo wa ramadhan pale zoo Muslims huwa tunajipikia viaz. Ss hyo week kukawa na kamata kamata ya simu by this time Nipo form6. Kumbe form 5 wakishirikiana na baadh ya form6 walikuwa na mpango wa chnchn kumcharaza mwl yyte atakae kuja kukamata simu aisee Mwl Nazareth alicharazwaa gizani 😂😂🙌🏽 Ile kapata upenyo katorokaa basi nusu saa hii Polisi cjuiii ffu hawa hapa wakwanza kubondwa virungu ni sie Muslims maana tulkua karbu tu jmn nililiaaa mm dah hii shulee sutaisahauuu
Big up hii nimeifanya sana Kahororo Secondary Bukoba, nadhani tulikuwa wote! sufuria inapigwa juu kwa juu! punje za Dona zinamwagika lkn zinadakwa zote kijanja, iliitwa ''scrumble'' ilikuwa inatokea km wapishi wameiba sana Unga waugali na kupikia maandazi maarufu bukoba ''Vibaragara''Na siku ya kula wali unavaa nguo za mapigano. Uji ukiwa hauna sukari na maharage yamejaa wadudu lakini mnagombania!
Msocha hakuwakamata kweli?Nakumbuka galanos sec tanga tulitotoka Na washkaji watatu,tukazamia kwenye harusi mtaani ,watu kibao wa ukwel plus totoz za kifa mtu bhas kwenye msosi kila mtu Na kadi yake(kumbuka tulizamia,),tukasema kwenye foleni tukae mbalimbali means mmoja nyumba mwingine katikati Na mwingine mbele(kumbuka hatuna kadi),Kwa kiherehere changu cha msosi nilikuwa wa mbele.
Nafika pale naulizwa kadi ipo wap najidai bubu af msosi unanukia kinyama(mambo ya kitanga,nikawekwa pembeni
Washkaji wakashtuka lkn hawawez kutoka coz geti zote zimefungwa ili wazamiaji wasiingie(sherehe za uswahilini kimtindo)
Baada ya dkka 5 msela wangu nae kapigwa ban ,hapo siongei wa kucheka coz mm ni bubu Ila kicheko kinakuja hadi machozi yanakaribia kutoka
Baada tena ya dkika5 msela nae kapigwa pembeni.
Wenye harusi wakaanza oh oh mnatutia aibu sijui nini Na nini ,mwishowe wakasema tukiendelea kusimama pale ndio tunawatia aibu mara dufu so tupitishwe Kwa mlango wa nyuma ambapo huku kuna masufuria.
Kufika huko tukakuta vitu vya kumwaga(misosi)
Dah huwez amini ububu ukaisha ,piga kinyama then tukaweka kwenye mifuko had skonga tukaingia prepo kila mtu alionja ,nikikumbuka mbavu sina
Sahihi Usangira HM na Maguhu Second Master mwanzoni mwa 2000s huko enzi za akina Chid Boy!...mkuu ulikuwepo nin au we ndo Nebo mwenyewe!duuuu...hiki kipindi cha headmaster usangira nn....
Enzi hizi acha kbsa aiseee.Ila nilipita juzikati pale sio kama miaka yetu ileSahihi Usangira HM na Maguhu Second Master mwanzoni mwa 2000s huko enzi za akina Chid Boy!...mkuu ulikuwepo nin au we ndo Nebo mwenyewe!
nilitumwa ofisini kwa mkuu nkakuta mikate imepakwa brubend kabsa nkaificha ndan ya sweta langu kumbe ilikua ya wasimamizi wa mitihan ya kidato cha sita duu ilikua nongwa kweli
Umenikumbusha mbali saaana.hahahaaa mm nakumbuka mwaka 2008 niko form 4 galanos tanga, kuna mwalim mmoja alikuwa anaitwa macmaster Luziro, alinidaka mtaani..., Sasa akajifanya mjanja et ananiita ananiuliza kijana unasoma wapi, nikamwambia nguvumali sec. Akasema bas nimekufananisha na mwanafunz wang nilimfundisha Ecknford.., Nikamuambia umenifababisha... Sasa hapo wote tukawa tumedanganyana wakat mm nilikuwa namsoma...
Ila alikuja akajua akaniambia we dogo ulinichezea sana akili