PA Nimejipendekeza kua Mkarimani.... Naomba lile deni ambalo nakudai uniongezee walau 30 ya soda.....:wink2: (ila story yako nimeruka.... na sio kwamba ipo sawa naweza nikawa nimekosea ila have tried my best)
Mapenzi… Mapenzi… Mapenzi….
Mapenzi ni hisia za ajabu… Kama umewahi bahatika kupenda Kimapenzi ama kuna mtu wampenda kimapenzi unaelewa hasa nini namaanisha kua ni hisia za ajabu. Kuna mtu Alisha wahi sema "Nimependa hadi kikomo cha Ukichaa, Jinsi ambayo kwangu ni njia pekee ya jinsi ya kupenda" na nakubaliana nae. Mara nyingi kwa sie wanaume kukubali kua twapenda kwa dhati wapenzi wetu ni kazi ILA Amini nakuambia nasie wanaume hua twapenda kiasi cha kuchanganikiwa mara moja moja. Upande wa wanawake hakuna ubishi kua wao wapo wazi zaidi kuonesha upendo wao hadi kikomo cha ukichaa. Wapo bora sana katika kutuonesha hasa ni namna na Kiasi gani watupenda… Much Love kwa akina dada/mama wote!
Kuna mambo ambayo waweza fanya yalo ya ukichaa yakawa ndani ya uelewa wa mwanadamu ukiwa uko ndani na dimbwi la Mapenzi. Lakini kuna mara nyingine watu hufanya hadi kuvuka mpaka ama niseme kua zaidi kuliko. Wengine hufanya ya ajabu/sio kawaida na kutengeneza kumbu kumbu nzuri na za kufurahisha. Lakini kuna wale hufanya yale ambayo yamevuka mpaka hadi yaweza badilisha maisha ya wahusika daima!
Leo nipo interested katika kukumbushiana ni mambo gani ya Ukichaa tumefanya kwa ajili ya Penzi… iwe sasa, karibuni ama zamani. Kitu gani cha ukichaa zaidi usha wahi fanya? Kiasi kwamba hata ukikumbuka sasa wajiuliza "hivi kweli ni mimi Yule alofanya yale?"