CPJ: Idadi ya waandishi wa habari waliofungwa duniani yaongezeka

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Kamati ya kutetea waandishi habari CPJ imesema idadi ya waandishi habari waliofungwa duniani mwaka huu imefikia kiwango cha juu huku China na Myanmar zikiropotiwa kuwaweka gerezani wanahabari 293.

Katika ripoti yake ya kila mwaka, kamati hiyo ya kutetea waandishi habari imesema waandishi habari 50 bado wanaendelea kuwepo gerezani nchini China, 26 Burma, 25 nchini Misri, 23 Vietnam na wengine 19 nchini Belarus.

Imeongeza kuwa wengine waliofungiwa nchini Saudi Arabia, Iran, Uturuki, Urusi, Ethiopia na Eritrea inafikisha idadi Jumla ya wafanyakazi wa vyombo vya habari walio korokoroni kufikia 293 kote duniani kufikia Disemba mosi. Idadi hii ni kubwa ikilinganishwa na mwaka uliyopita ya 280.

Joel Simon, Mkurugenzi mtendaji wa kamati hiyo amesema hii ni mara ya sita mfululizo CPJ inaweka rikodi ya waandishi waliofungwa gerezani kote duniani, akisema kuwafungia waandishi hao kwa kufanya kazi yao ni ishara tosha ya tawala zinazoongoza kimabavu.

Kwa miaka 40 CPJ imekuwa ikikosoa mauaji, kufungwa kiholela, kunyamazishwa, kupigwa na kutishwa kwa waandishi habari.

Katika ripoti yake kamati hiyo imesema inasikitisha na kuumiza kuona mataifa mengi zaidi kila mwaka katika orodha inayowahangaisha waandishi habari hasa nchini Myanmmar na Ethiopia ambako uhuru wa vyombo vya habari umekiukwa. CPJ imesema mwaka huu pekee waandishi 24 wameuwawa duniani kote.

Mexico imebakia kuwa taifa lililo hatari mno kwa waandishi habari ambako watatu tayari wameshauwawa kutokana na kazi yao huku kiini cha mauaji ya wengine sita kikiendelea kuchunguzwa.

India pia imetajwa kuwa katika hali mbaya, waandishi 4 wameuwawa huko mwaka huu. CPJ imesema idadi kubwa ya waandishi habari wamekatamwa kutfuatia kuendelea kukandamizwa kwa uhuru kwa kuripoti kwa uwazi duniani.

Ripoti hiyo imezungumzia pia hali mbaya kwa waandishi habari duniani ikiwemo sheria zinazowalenga waandishi habari mjini Hong Kong na Xinjiang, mapinduzi ya kijeshi Myanmar, vita vya Kaskazini mwa Ethiopia na kamata kamata inayofanywa dhidi ya upinzani nchini Belarus.

Chanzo: DW Swahili
 
Back
Top Bottom