Ngongo
Platinum Member
- Sep 20, 2008
- 21,370
- 37,908
- Thread starter
- #41
Konda wa bodaboda Asante kwa kuniita huku japo naona kama ni mipasho tu na hamna chochote humu mnachojadili kinachohitaji matumizi ya akili. Kuna mambo kadhaa nafaa kuyaweka bayana hapa.
- Mgogoro baina ya Kenya na Uganda kuhusu hilo eneo la Migingo haujaanza jana, ni jambo ambalo huwa linaendelea kutatuliwa, uhusiano wetu na Uganda upo thabiti haswa kibiashara.
- Hilo la bomba, Waganda wana haki ya kuchagua eneo ambalo halitawapa wasiwasi kwenye gharama na usalama. Hivyo tunahitaji kuwahakikishia hayo au waende kwingine. Hii ni biashara na kama nisemavyo kila siku humu, hamna cha undugu kwenye biashara ila maslahi. Ujio wa Waganda huko Tanzania ni kwa sababu ya mahesabu yao na ikitokea sisi Wakenya tumeshindwa kuwadhihirishia matakwa yao, basi wapo radhi kuchagua wanakotaka.
Kuna kikao kitafanyika ndani ya siku kumi baina ya Waganda na Wakenya kujaribu kuona kama tunaweza afikiana kwenye hili, sasa hivi tayari tuna bomba kuanzia Eldoret hadi Mombasa, hivyo tunaweza waambia Waganda kwamba tutengeneze bomba la kuunga hili ambalo lipo tayari, kimsingi tutajaribu kuwahakikishia na kurekebisha kilicho wafanya watelekeze mkataba wa hapo awali baina yetu. Lakini ikishindikana basi tunaachia bila majungu, nothing personal, hii ni biashara tu.
- Muungano wa CoW upo kwa ajili ya maslahi, hamna cha undugu wala nini, dunia ya sasa haitaki maisha ya kusuasua na uwoga uwoga, maamuzi lazima ufanye kwa haraka maana hamna muda tena. Miaka ya hapo awali ilikua rahisi kuwa wavivu na kulalia maskio, lakini huo muda haupo tena.
Na ndio unaona hata rais wenu Magufuli hilo ameshalijua na hazubai tena, uchaguzi uliofanyika huko kwenu uliwadhihirishia viongozi wa CCM kwamba wananchi wamechoka na maisha ya umaskini wakati wana raslimali za kila aina. Kila siku wimbo ni ule ule, Tanzania ina ardhi nyingi zaidi ya mataifa yote EAC, ina madini, ina vivutio bora, ina bandari kubwa, maziwa na bahari n.k lakini bado inatajwa kwenye orodha ya nchi maskini wa kutupwa, huku ikihangaika kushindana na nchi ndogo ndogo kama Kenya.
CCM waliponea kwenye tundu la sindano maana walitumia nguvu nyingi sana kurejea kwenye madaraka. Hata kule Zanzibar bado wanayumba tu, wamelazimika kuwajaza wanajeshi kila kona.
Cha msingi, ifahamike muungano wa CoW upo kwa ajili ya kuharakisha yale tunayoyaweza na kuachia yale magumu hadi baadaye. Na sio lazima kila tutakachoanzisha kifaulu kwa mpigo mmoja tu, patakua na changamoto kadhaa mwanzoni, lakini taratibu tutazirekebisha tu. Hivi sasa DRC na Ethiopia tayari wameanza mikakati ya kujiunga na huu muungano, maana kila yeyote amekaribishwa na kujiunga na chochote humo atakacho ona kinamfaa, sio lazima uratibishe kila kitu, tunakuachia ujiunge na kitakachokufaidi, humu hatuna mambo ya undugu, hata Magufuli mwenyewe alishasema yupo tayari kuihusisha nchi yake kwenye hii miradi ya CoW.
Sasa hivi tupo mbioni kumfikishia Kagame reli ya SGR itakayowezesha mizigo kufika Kigali ndani ya masaa 24. ujenzi tayari unafanywa kwa spidi ya kufa mtu. Hiyo reli hatimaye itaunga hadi kule Burundi na DRC, na pia itakua ya msaada sana kwa wajasiria wa Tanzania Kaskazini. Hatuna muda wa kupoteza.
Mkuu MK254 Mgogoro wa kisiwa kidogo cha Migingo haujalishi kama umeanza leo au jana jambo lilo wazi ni kwamba mgogoro huu unaibuka mara kwa mara kwa mameno rahisi bado haujapatiwa ufumbuzi wa kudumu.Kenya wanadai ni kisiwa chao Uganda nao vile vile wanadai ni kisiwa chao ndio maana wamezuia maafisa uchaguzi kuacha kuendesha zoezi la kuandikisha wapiga kura.
Mheshimiwa hakuna kikao kitakachofanyika baina ya Kenya na Uganda kuhusiana na ujenzi wa bomba la mafuta kama kikao kitakuwepo basi watazungumza juu ya Kisiwa cha Migingo.Kuna uzi ulianzisha kuhusiana na kikao hicho lakini baada ya kupekenyua tukagundua ni kikao kilichotarajiwa kufanyika mwaka 2015 wakati kikao cha Dr Magufuli na M7 kilifanyika mwaka huu 2016.
Nakubaliana na wewe muungano wa CoW upo kwaajili ya maslahi lakini maslahi hao mengi ni kwaajili ya kuiumiza Tanzania jambo ambalo limeshindwa na linaendelea kushindwa.