CoW yazidi kusambaratika

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
19,931
34,408
Ule muungano haramu baina ya nchi za Uganda,Kenya & Rwanda umezidi kusambaratika baada ya majeshi ya Uganda kuwakamata maafisa wa Kenya waliokuwa wakiandikisha zoezi la wapiga kura nchi Kenya.Majeshi ya Uganda yaliwatia mbaroni maafisa wa Kenya kwa kile wanachodai Kisiwa cha Migingo ni sehemu ya ardhi ya Uganda.

Ikumbukwe muungano wa CoW ulipata kipigo kingine wiki chahche zilizopita baada ya Uganda kuamua kupitisha bomba la kusafirisha mafuta Tanzania badala ya Kenya.Kama hiyo haitoshi Tanzania ilisimamia kikamilifu kuhakikisha raia wa Burundi anachukua wadhifa wa katibu mkuu wa jumuiya kuanzia mwezi April 2016.Rwanda ikitumiwa na Kenya zilifanya kampeni iliyokuwa na lengo la kuongeza muda wa Katibu Mkuu wa sasa raia wa Rwanda au achaguliwe katibu mkuu kutoka Kenya kwa kisingizio eti hali ya machafuko Burundi isingefaa kutoa katibu mkuu wa EAC.Nidhahiri CoW iliyokuwa na nguvu kipindi cha utawala wa Kikwete sasa unaelekea kufa na kuzikwa rasmi.

Voter listing resumes in disputed Migingo Island
 
Picha linaendelea, kinachofurahisha zaidi administration ya magogoni mpya, kama vile EXPENDABLES, Lazima uwapende tu...
 
Dah mkuu Ngongo hili suala la katibu mkuu wa EAC kutokea Burundi na figisu alizofanyiwa inaonekana ni jambo nyeti sana na halikuvuma kabisa kwenye media.

Kama una nyama vizuri ni bora tuanzishe uzi mzuri kabisa hapa tulijadili kwa mapana yake, maana ile clip iliyorushwa na TBC ikimuonesha Magufuli na Kenyatta wakihojiwa ni kama Kenyatta alikua anajichekesha kinafiki nafiki fulani hivi mpaka mie nikastuka.

Seems kuna ishu kubwa sana inaendelea aiseee
 
Mkuu asigwa unajua nafasi ya Secretary General EAC ni nyeti sana.Kipindi cha utawala wa Dr Sezibera raia wa Rwanda ambaye alikuwa Dr binafsi na Aide de camp wa General Kagame kabla na baada ya vita vya uvamizi (RPF) ndio tulishuhudia EAC ikiyumba sana kwakuwa alikuwa akitekeleza ajenda za CoW.Zipo taarifa kwamba kuna baadhi ya funds zilikuwa zikitoka EAC kugharamia na kuratibu mikutano ya CoW mfano EAC defence protocal & Northern Corridor Intergration Projects.

Muda wa Dr Richard Sezibera ulipoanza kukaribia kumalizika zikaanzishwa propaganda aendelee kwakuwa chini ya uongozi wake protocals nyingi zilikuwa signed lakini wakasahau audit reports zilikuwa zikimuumbua sana.Burundi ndio walikuwa na zamu ya kumtoa katibu mkuu wa EAC baada ya nchi zote wanachama Kenya,Uganda,Tanzania na Rwanda kuwahi kushika wadhifa huo mkubwa katika jumuiya.Ilikuwa ni dhahiri Rais wa Burundi asingefka katika mkutano kutokana na hali ya kiusalama nchini mwake,tayari makundi ya kimkakati yalishaundwa na waTutsi wa Burundi wakidai eti nchi yao haina haki ya kushika wadhifa huo kutokana na hali ya usalama kwakuwa Tanzania ilishabaini janja ya CoW Dr Magufuli akatumia wadhifa wake wa Mwenyekiti kufanya kikao cha faragha na viongozi wenzake na kujenga hoja matatizo ya Burundi hayawezi kuzuia au kuinyima nafasi ya uongozi ndani ya jumuiya.Rwanda ilikuwa na wasiwasi iwapo wadhifa huo utaangukia kwa raia wa Burundi kutaipataia nafasi kubwa serekali ya Nkurunzinza katika siasa za EAC.

Baada ya CoW kutamba kwa muda mrefu ni dhahiri hali ya mambo imeanza kubadilika sana huku mikakati yao ikizidi kuharibika kabisa.
 
Dah Thanks sana mkuu, umenifungua sana macho.

Nachoshindwa kuelewa ni kwa nini Museveni ambaye anaonekana mshirika wa karibu sana wa Tanzania anajiingiza kichwa kichwa kwenye ishu ambazo ziko enginered na Kenya kupitia Rwanda au ndio ile slogan kuwa Museveni ni mzee wa kung'ata na kupuliza??.

CoW mtu yeyote mwenye akili alikua anajua kuwa haiwezi kufika popote, kifupi ilikua imeshabuma kabla haijaanza.
Na sasa Sudani Kusini anavutwa kuingizwa ndani ya EAC ili kuwapa nguvu Kenya na Rwanda ila soon naona mchezo utawageukia pia.

Nilicheka sana juzi kati kusikia kuwa Kenya na Ethiopia walikua wamefungiana mipaka "wamenuniana", upande wa Somalia nako mipaka yao ni hatari tupu, palipo na unafuu ni huku kwetu Tanzania sasa nachojiuliza kwa nini hawa jamaa wanatufanyia "unyang'au"??
 
Mkuu asigwa unajua M7 ana ndoto za urais wa EAC kila akipiga hesabu zake Tanzania imekuwa kikwazo kwake haitaki mambo ya haraka haraka hii ndio sababu kuu ya Uganda kupendelea CoW yenye malengo ya kupeleka mambo haraka haraka kabla M7 ajatwaliwa na Mungu hasa tukizingatia umri wake umekwenda kilometa nyingi sana.

Kenyatta na Kenya wanataka kutawala biashara ya bidhaa za viwandani kwakuwa wana viwanda vingi ukilinganisha na nchi nyingine za EA hawajali nani atakuwa kiongozi mradi mambo yao yanakwenda vizuri

Rwanda inataka ardhi na usalama katika jumuiya.Mambo hayo yanakinzwa na katazo la Tanzania kukatalia ardhi yake huku Rwanda ikilemewa na wingi wa watu na uhaba mkubwa wa ardhi.Kitendo cha Tanzania kupeleka majeshi yake Congo DRC kulikata mirija yake ya wizi wa rasilimali za Congo mambo yote haya yalichangia Kagame kuichukia Tanzania na hasa Kikwete.
 
Mkuu kwanini ni Rwanda tu iwe na ardhi ndogo na sio Burundi na Uganda kwa pamoja? Je wanakabiliana vipi na hali hiyo ya ukosefu wa ardhi, au ndio kuwahamisha raia wao kuja kwetu Tanzania kwa mwamvuli wa wakimbizi?
 
Mkuu Uganda sidhani kama ina matatizo ya ardhi, kinachoikabili Uganda ni uchumi mbovu na waasi kaskazini mwa nchi.

Burundi tatizo la ardhi analo lakini ameshajiridhikia na matatizo yake na Rais wao ni Mlokole mzuri tu, kifupi keshajijua yeye ni mnyonge na amekubali unyonge wake.

Rwanda yeye ni kichwa ngumu, tatizo la ardhi analo kubwa mno na anatafuta njia mbadala wa ardhi, mkakati ulikua ni kuimega Congo na ukabuma, Tanzania ni pamoto sana huu mkakati wa kuimega hauwezekani.
 
Mkuu kwanini ni Rwanda tu iwe na ardhi ndogo na sio Burundi na Uganda kwa pamoja? Je wanakabiliana vipi na hali hiyo ya ukosefu wa ardhi, au ndio kuwahamisha raia wao kuja kwetu Tanzania kwa mwamvuli wa wakimbizi?

Mkuu @Konda wa bodabado nchi zote za EA zina uhaba wa ardhi lakini pia zinazidiana kiwango na nyingine ni ugawaji mbovu.
a) Kenya ina ukubwa wa eneo 581,309 sq km na idadi ya watu 46 million
b) Uganda ina ukubwa wa eneo 241,038 sq km na idadi ya watu 36 million
c) Rwanda ina ukubwa wa eneo 26,338 sq km na idadi ya watu 12 million
d) Burundi ina ukubwa wa eneo 27,816 sq km na idadi ya watu 10 million

Tanzania bado ni kubwa kuliko nchi zote kwa pamoja ukubwa wa eneo 945,087 sq km na idadi ya watu 47 million.Ukitazama ukubwa wa eneo na idadi ya watu Rwanda ndio inaongoza huku ikiwa na mgogoro wa chini kwa chini wa kikabila.Watutsi wengi waliorejea baada ya RPF kushika madaraka waliwapora ardhi wahutu hilo pekee ni tatizo kubwa ambalo jawabu lake pengine lingekuwa Tanzania.Upande wa Kenya lipo tatizo la ugawaji wa ardhi mbovu wanasiasa hasa Kenyetta na matajiri wachahche wanamiliki ardhi kubwa huku idadi kubwa ya raia wakiachwa bila ardhi.Tatizo la ardhi lilikuwa moja ya sababu za muungano wa CoW.
 
Upi msimamo wa Tanzania kwenye suala la ardhi yake dhidi ya nchi jirani?
 
Msimamo wa ardhi uko wazi wana EAC ni wageni wakitaka ardhi wafuate utaratibu wa kuimiliki na si kama wazawa (Tanzania) utaratibu wao wa kumiliki ardhi ni rahisi sana.
Mkuu Ngongo una maanisha kwamba utaratibu wa Tanzania kumiliki ardhi ni rahisi au utaratibu wa EAC ndio wenye utaratibu rahisi sana hadi Tanzania kukataa utaratibu wao?
 
Utaratibu wa kumiliki ardhi mtanzania uko wazi na umerahisishwa.Wageni wanautaratibu wao tofauti na wazawa kinachogombaniwa Kenya,Uganda,Rwanda wanataka wananchi wao wakija Tanzania wapewe fursa sawa na waTanzania na si wageni.
 
Wanachekesha kweli hao majirani, yaani watu wameshindwa kuishi kwa umoja kwenye nchi zao, tena zenye idadi ndogo ya makabila tofauti na Tanzania ila hawaoni aibu kutaka kujichanganya kuishi Tanzania kama kwao!
 
Konda wa bodaboda Asante kwa kuniita huku japo naona kama ni mipasho tu na hamna chochote humu mnachojadili kinachohitaji matumizi ya akili. Kuna mambo kadhaa nafaa kuyaweka bayana hapa.
- Mgogoro baina ya Kenya na Uganda kuhusu hilo eneo la Migingo haujaanza jana, ni jambo ambalo huwa linaendelea kutatuliwa, uhusiano wetu na Uganda upo thabiti haswa kibiashara.

- Hilo la bomba, Waganda wana haki ya kuchagua eneo ambalo halitawapa wasiwasi kwenye gharama na usalama. Hivyo tunahitaji kuwahakikishia hayo au waende kwingine. Hii ni biashara na kama nisemavyo kila siku humu, hamna cha undugu kwenye biashara ila maslahi. Ujio wa Waganda huko Tanzania ni kwa sababu ya mahesabu yao na ikitokea sisi Wakenya tumeshindwa kuwadhihirishia matakwa yao, basi wapo radhi kuchagua wanakotaka.
Kuna kikao kitafanyika ndani ya siku kumi baina ya Waganda na Wakenya kujaribu kuona kama tunaweza afikiana kwenye hili, sasa hivi tayari tuna bomba kuanzia Eldoret hadi Mombasa, hivyo tunaweza waambia Waganda kwamba tutengeneze bomba la kuunga hili ambalo lipo tayari, kimsingi tutajaribu kuwahakikishia na kurekebisha kilicho wafanya watelekeze mkataba wa hapo awali baina yetu. Lakini ikishindikana basi tunaachia bila majungu, nothing personal, hii ni biashara tu.

- Muungano wa CoW upo kwa ajili ya maslahi, hamna cha undugu wala nini, dunia ya sasa haitaki maisha ya kusuasua na uwoga uwoga, maamuzi lazima ufanye kwa haraka maana hamna muda tena. Miaka ya hapo awali ilikua rahisi kuwa wavivu na kulalia maskio, lakini huo muda haupo tena.

Na ndio unaona hata rais wenu Magufuli hilo ameshalijua na hazubai tena, uchaguzi uliofanyika huko kwenu uliwadhihirishia viongozi wa CCM kwamba wananchi wamechoka na maisha ya umaskini wakati wana raslimali za kila aina. Kila siku wimbo ni ule ule, Tanzania ina ardhi nyingi zaidi ya mataifa yote EAC, ina madini, ina vivutio bora, ina bandari kubwa, maziwa na bahari n.k lakini bado inatajwa kwenye orodha ya nchi maskini wa kutupwa, huku ikihangaika kushindana na nchi ndogo ndogo kama Kenya.

CCM waliponea kwenye tundu la sindano maana walitumia nguvu nyingi sana kurejea kwenye madaraka. Hata kule Zanzibar bado wanayumba tu, wamelazimika kuwajaza wanajeshi kila kona.

Cha msingi, ifahamike muungano wa CoW upo kwa ajili ya kuharakisha yale tunayoyaweza na kuachia yale magumu hadi baadaye. Na sio lazima kila tutakachoanzisha kifaulu kwa mpigo mmoja tu, patakua na changamoto kadhaa mwanzoni, lakini taratibu tutazirekebisha tu. Hivi sasa DRC na Ethiopia tayari wameanza mikakati ya kujiunga na huu muungano, maana kila yeyote amekaribishwa na kujiunga na chochote humo atakacho ona kinamfaa, sio lazima uratibishe kila kitu, tunakuachia ujiunge na kitakachokufaidi, humu hatuna mambo ya undugu, hata Magufuli mwenyewe alishasema yupo tayari kuihusisha nchi yake kwenye hii miradi ya CoW.

Sasa hivi tupo mbioni kumfikishia Kagame reli ya SGR itakayowezesha mizigo kufika Kigali ndani ya masaa 24. ujenzi tayari unafanywa kwa spidi ya kufa mtu. Hiyo reli hatimaye itaunga hadi kule Burundi na DRC, na pia itakua ya msaada sana kwa wajasiria wa Tanzania Kaskazini. Hatuna muda wa kupoteza.
 
Back
Top Bottom