CoW yazidi kusambaratika

Unazungumziaje kuhusu suala la ardhi kwenye shirikisho ukizingatia kwamba ni Tanzania na Kenya pekee ndizo nchi zenye ardhi kubwa kuliko zote ndani ya shirikisho. Mkuu Ngongo amesema kwamba kuna baadhi ya nchi zinataka raia wao wawe na haki sawa ya kumiliki ardhi sawa na raia wa nchi yenye ardhi kubwa, nini maoni yako?
 
Mambo yapo mengi ya kuungana na sio lazima tuungane kwenye ardhi, fahamu kwenye CoW kila mshirika ana uhuru wa kuchagua asichotaka kuhusishwa nacho, na kuunga kwenye kinachomfaidi. Huwezi kununa kwa kila kitu kisa ardhi, kila ukiombwa na kuagizwa tuungane kwenye mengine kama elimu, miundo mbinu, biashara n.k. unanuna eti ardhi ardhi.

Cha msingi na muhimu ni kuwa na sera nzuri za ardhi, hata usipoungana na wenzio lakini uwe na sera mbovu, bado hiyo ardhi yako italiwa na kutafunwa tu. Hapo Tanzania nimeona jinsi wageni kutoka mbali wanavyomega ardhi, ilmradi wana hela za kumwaga. Wawekezaji wageni kutoka mbali wamenunua ardhi nyingi sana halafu badala ya kuwekeza, wanatumia kupata mikopo, huo ni mfano mmoja tu, ila kuna mengi yanafanyika.

Hivyo, ukigoma kuungana na wenzio kisa unataka kuwabana kwenye masuala ya ardhi halafu mwenyewe una sera mbovu na ufisadi kiasi kwamba Mwarabu na Muhindi anatua na mkoba wake na kufanya yake, utakua hujafanya chochote.
 
Vipi Kenya mkuu, nasikia kuna matajiri wakubwa wanamiliki ardhi kubwa huku wananchi wakikosa ardhi ya kilimo na shughuli za makazi
 
Vipi Kenya mkuu, nasikia kuna matajiri wakubwa wanamiliki ardhi kubwa huku wananchi wakikosa ardhi ya kilimo na shughuli za makazi

Kenya tulishakubali tuna matatizo ya kihistoria ya ardhi na tumeboresha sera haswa kwenye katiba mpya.
Mambo mengi yamefanyika na tunaendelea kuboresha. Serikali inanunua ardhi na kuwagawia raia. Mfano ni ile ardhi ya Waitiki.
 
Kachukueni ardhi kwa Kenyatta.
 
Kachukueni ardhi kwa Kenyatta.

Kama wewe mfuatiliaji wa taarifa za Kenya utaona kwamba tayari na hiyo pia tunaimega japo taratibu. Kadiri muda unavyoenda na changamoto zinavyozidi kuongezeka, familia ya Kenyatta watajikuta wameachia pia. Rais Uhuru alishasema mwenyewe hana usemi kuhusu hiyo ardhi maana ni ya familia na yeye kama mmojawapo wa wana wa hiyo familia hawezi fanya maamuzi binafsi bila kuwaomba wengine.

Kwa mfano leo hii haiwezekani mwana mmoja wa aliyekua rais Mkapa au Mwinyi akafanya maamuzi juu ya mali ya familia yote ya Mkapa. Hapa kwetu Uhuru anabanwa na sheria na mfumo, lakini taratibu hiyo ardhi itatwaliwa tu, vijana wanazaliwa kila siku wasiokua na subira na ambao hawajui wala kufahamu michango ya hayati marehemu Kenyatta, hivyo hawataendelea kuvumilia umaskini wakati wanaona kuna familia zenye ardhi kubwa kubwa.

Cha msingi ni kwamba, imetuchukua muda mrefu kuboresha sera za mambo ya ardhi. Tumeweka nguzo zote muhimu na kuhakikisha jamii itanufaika pakubwa na mifumo yetu ya ardhi. Na kama nilivyotaja, serikali tayari inanunua ardhi kubwa kubwa na kuwagawia raia maskini.
 
Kenya bado sana. Serikali haina sauti kwenye ardhi za watu binafsi.
 
Ifahamike rasmi Burundi ni mshirika mtiifu kwa Tanzania yanapokuja maswala ya EAC.Hivyo Katibu Mkuu raia wa Burundi ni pigo kubwa sana kwa muungano wa CoW

Mkuu Ngongo kuna wakati nilifikiria Burundi ikiungana na Tanzania lingekuwa jambo jema sana, actually Burundi na Tanzania gotta lot in common, tuungane kama ilivyo Zanzibar wao wawe na Serikali yao na kujihamlia mambo yao. Hayo ni maoni yangu.
 
Mkuu Bukyanagandi muungano na Tanzania unaweza kumaliza matatizo yao ya kikabila.Zanzibar bila Tanganyika hali ingekuwa mbaya kuliko Burundi ya leo.
 
Walikuwa Na Muunga no wa kinafiki
Tanzania nimtakuja tu
Na kujibaragqzua koote lakini watatulia
MK254
 
MK254
 
Mkuu kwanini ni Rwanda tu iwe na ardhi ndogo na sio Burundi na Uganda kwa pamoja? Je wanakabiliana vipi na hali hiyo ya ukosefu wa ardhi, au ndio kuwahamisha raia wao kuja kwetu Tanzania kwa mwamvuli wa wakimbizi?
Wanataka kujitanua kama Israel
Kitu ambacho hakiwezekani
 
Tena asije kurogwa kujaribu upuzi huo
Naamini itakuwa kiama kwake
 
Mkuu Ngongo kuna wakati nilifikiria Burundi ikiungana na Tanzania lingekuwa jambo jema sana, actually Burundi na Tanzania gotta lot in common, tuungane kama ilivyo Zanzibar wao wawe na Serikali yao na kujihamlia mambo yao. Hayo ni maoni yangu.
Mkuu huo muungano unadhani ungekuwa na makubaliano gani kwa sababu tayari umesema watakuwa na serikali yao?
 
mada tamu sana napenda sana wakuu mnavyotingishana kwa hoja
 
Mkuu huo muungano unadhani ungekuwa na makubaliano gani kwa sababu tayari umesema watakuwa na serikali yao?

Mkuu kwani muungano wa sisi na Zanzibar huko je, mbano wana Serikali yao? Burundi wanaweza kufuata mkondo huo huo, muugano utawapa bonasi ya ziada in terms of usalama, ulinzi, kupunguza msuguano wa kikabila unao chochewa na majirani zao etc.
 
Hilo linawezekana mkuu, lakini kumbuka population ya Zanzibar ni 1.5Millions wakati warundi ni almost 12Millions ambao ni kama robo ya Watanzania wote millioni 48.
Tukiwabeba warundi kuwaingiza huku kwetu tunakua tumebebamzigo mkubwa sana wa watu ambao sidhani kama ardhi yetu inaweza kuwa accomodate.

Kumbuka hawa jamaa ni wafugaji kama walivyo wamasai, sasa kama wamasai wasiofika millioni 2 tu wanatupa headache kwa migogoro ya wakulima na wafugaji kila siku Morogoro huko, tukibeba load ya 12Millions inkuwaje??
Maana yake ni kuwa tutakuwa tumekuza migogoro ya wakulima na wafugaji kama mara 6 hivi
 
Mkuu asigwa ni kweli tukiungana na Burundi zipo athari zake lakini pia zipo faida zake.Yafaa wataalam wa uchumi,jamii na siasa wakafanya uchambuzi wa kina kupima hizo faida na hasara lakini kubwa zaidi ni utayari wa warundi na wataganyika wenyewe kuungana na si kulazimisha kama ilivyo Zanzibar.Mwaka 2011 tulitoa uraia kwa wakimbizi 8000 wa Rwanda na Burundi,Mwaka juzi tulitoa uraia 1,500 wakimbizi wa kisomali wapo kule Handeni Tanga mwaka jana tulitoa uraia kwa warundi 162 na bado zipo dalili ya kuendelea na zoezi la kugawa uraia kila mwaka hasa nchi zenye matatizo ya usalama kama Burundi na Congo DRC.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…