COVID-19: Uwezo Dhaifu wa Serikali

introvert

JF-Expert Member
Sep 21, 2010
1,372
2,416
WanaJF,

Tanzania, kama nchi nyingine zote duniani zinapitia changamoto ya Coronavirus.

Hapa kwetu, kwa bahati ya pekee kabisa, tumepata nafasi ya takribani miezi miwili mitatu kujiandaa. Unategemea Serikali yenye wasomi kuwa na mpango wa kudhibiti tatizo hili na kulinda maisha ya raia wake na uchumi na nchi.

Lakini Serikali hii, kuanzia Raisi, wameonyesha uwezo mdogo sana. Raisi amewaambia watu waendelee kwenda kanisani na misikitini kwani Mwenyezi Mungu atatuokoa. Kasi ya ugonjwa imeongezeka Rais wala hatoi hotuba yoyote zaidi ya kutoa tweet akituomba tufanye maombi ya siku tatu.

MaRaisi wenzake wapo busy wakihutubia na kusema hatua walizochukua na wanazotegemea kuchukua. Yeye yupo Chato zaidi ya wiki mbili sasa hakuna any press conference kusema mipango ya Serikali.

Raisi amesema huu si ugonjwa wa kutisha kama Malaria na magonjwa mengine. Hii inaonyesha ni jinsi gani Rais hana uelewa wa athari za huu ugonjwa kwa sekta nzima ya afya, uchumi na uhai wa wale anaowaongoza. Ignorance ya hali ya juu kutoka ofisi ya Rais na Rais mwenyewe.

Lakini ignorance hii si tatizo kwa sababu wengi anaowaongoza ni ignorant wa hali ya juu. Leo wapo siku ya tatu kwenye maombi na wanaona ni sawa kabisa.

Ugonjwa huu unaweza kupelekea sekta nzima ya afya kusimama na kuua uchumi wa nchi. Kudharau huu ugonjwa na kuufananisha na magonjwa mengine ni kuonyesha ignorance.

Ndani ya hiyo miezi miwili mitatu ya kujiandaa tumeshindwa kuweka protocol za kutambua risky visitors na hata kutenga sehemu nzuri na maalumu ya kupokea wageni na kufanya isolation ili kupunguza imported cases.

Mara mahoteli. Mara maporini na vichakani huko. Mara mabweni ya wanafunzi. Hizo sehemu hazina basics za kumsaidia mtu mzima au mgonjwa aishi kwa usalama.

Tatizo lingine kubwa ni testing/upimaji wa watu. Process hii imekuwa centralized. Mpaka samples zitumwe maabara kuu halafu ndo majibu yatumwe kwenye hospitali husika na mikoani. Kwa njia hii ni watu wangapi unaweza ukapima kwa siku moja? Hatupewi majibu.

Mass testing inasaidia kutambua sehemu zenye athari kubwa na kuweza kuzuia na kupunguza idadi ya wagonjwa. Leo hii japokuwa Dar ina wagonjwa wengi “officially” lakini hakuna restriction yoyote ya kumzuia mtu kwenda mkoa mwingine. Watu wakianza kukimbilia mikoani tatizo litaongezeka.

Ukija kwenye uchumi hakuna kitu Serikali imefanya kusaidia private sector mpaka sasa. Wapo business as usual mode. Nchi nyingine wanapunguza kodi, wanatoa muda zaidi wa kufanya malipo, wanatoa misamaha ya tozo n.k. lakini hapa kwetu ni kama vile biashara zinaenda sawa tu.

Biashara zinafungwa na watu wanapoteza ajira lakini Serikali imenyamaza kimya kama vile hakuna tatizo. Hii yote ni kukusanya kodi iende kwenye miradi mfu ya SGR, ATCL na Nyerere Hydropower. Kuna wabishi hawatambui hii miradi ni white elephant projects lakini muda utasema.

Mwisho ni namna hili suala limegeuzwa kuwa uwanja wa mahubiri na siasa. Wachungaji na wanasiasa aina ya Paul Makonda ambao kichwani hawana kitu ndiyo wasemaji na wanaotoa maelezo.

Huyu Mkuu wa Mkoa wiki moja anawaambia watu watoke majumbani na kazi ziendelee kama kawaida kwani huu ugonjwa si kitu. Wiki ijayo anasema watu wasitoke kama hawana jambo la maana. Uongozi katika dharura unahitaji consistency.

Muhimu zaidi unahitaji sauti inayoaminika na yenye authority. Where is The President? Where is the VP?

Ukija kwa Waziri wa Afya anasema ameanza kusema ukweli. Hivi mpaka sasa yupo ofisini hajajizulu wala kufukuzwa kazi kwa kuwa alikuwa anasema uongo. Nani atamwamini tena huyu? Halafu mnaomba michango, nani atatoa pesa kama hamsemi ukweli?

Waziri anasoma takwimu anaondoka. Hamna mtaalamu wa sekta husika ya Afya anayeongea kutoa maelezo na mwelekeo. Ni kama tunasubiri maajabu tu yatuokoe.
 
Kiranja mkuu alishakimbia siku nyingi tokea 18/ March yuko Chat* huko. Marais na viongozi wote duniani hawalali wanahaha kuokoa uchumi na kulinda nchi zao na afya watu wao.
 
WanaJF,
Tanzania, kama nchi nyingine zote duniani zinapitia changamoto ya Coronavirus.

Waziri anasoma takwimu anaondoka. Hamna mtaalamu wa sekta husika ya Afya anayeongea kutoa maelezo na mwelekeo. Ni kama tunasubiri maajabu tu yatuokoe.
Duh...!.
P
 
Uganda wanapambana na Corona vizuri kuliko wazungu!
_20200419_204024.JPG
 
Huwezi jua mkuu wenda na yeye ana korona anauguzwa kimya kimya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom