Cost of living in Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Cost of living in Tanzania

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by stringerbell, Jun 25, 2010.

 1. stringerbell

  stringerbell Member

  #1
  Jun 25, 2010
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wanajamii habari zenu
  jamani naomba kuwauliza kuhusu cost of living sasahivi hapo bongo,mimi nipo state natarijia kuja hapo kukaa kwa muda wa miezi 4.
  bei ya vyakula kama mchele ,maharage,vitunguu,mbatata n.k ni kisai gani
  vinwaji kama bia na soda kiasi gani?
  petrol kwa litre kiasi gani
  nyama na kuku kilo kiasi gani
  mobile phone rate

  pamoja na gharama nyengine muhimu ambazo nimesahau kuzitaja.
   
 2. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #2
  Jun 25, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 362
  Trophy Points: 180
  pamoja na kukaa state kote huko bado tu hujaacha ku-convert!
   
 3. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #3
  Jun 25, 2010
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  We nenda tu bongo, Maisha laini, hasa kama una hizo USD, tatizo ni sisi tunaopata pesa za madafu hapa Bongo,
  Just fyi, kilo ya mchele is almost 1 usd kwa sasa, Mobile charges are resonable (kila provider na mtindo wake) we njoo na hizo dollar angalau ukuze uchumi bwana
   
 4. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #4
  Jun 25, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Sasa hiyo ni swali gani? Kwani ati unataka kuja na kijiji kizima?
   
 5. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #5
  Jun 25, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Duh....afadhali unarudi.......Tuletee zawadi.....Huku si hali mbaya kaka.......Si unakuja nazo??? I mean USD????? Kama vp nifanyie ka laptop wangu unipunguzie ghadhabu za kubanana cafe,,,,,,,,,

  Hope mpk hapo ushajua Bongo ipo vp......

  Huwezi kwepa MIZINGA...

  KARIBU
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Jun 25, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Maisha Bongo ni ya kawaida tu Broda, si unaona tunaishi na tunakomaa?...Kimsingi ni kwamba kama percent kubwa ya wabongo wanaishi chini ya 1$ kwa siku, wewe utashindwa?..Ni kweli kuna vitu vya gharama, kuna viwanja vya starehe vya ghali, lakini kwa mtu aina yako huwezi shindwa bana, we njoo..nadhani huku ni kwenu!
   
 7. AK-47

  AK-47 JF-Expert Member

  #7
  Jun 25, 2010
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  We come tu usiogope kama umeweza kuishi ng'ambo utashindwa bongo tena kwa miezi minne tu huku ukichacha kama una ndugu ama marafiki utakula tu. kuhusu bia na soda bei zinatofautiana kuna za ki Mlimani City, ki Rose Garden, Break Point na hata za Maryland wewe ni kupima nguvu yako ya kiuchumi.
   
 8. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #8
  Jun 25, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,947
  Likes Received: 2,093
  Trophy Points: 280
  Tembelea tovuti hii labda utapata msaada www.nbs.go.tz Lakini wewe njoo tu bongo na kiasi ulichonacho - kama kitaisha siutapunguza muda wa kukaa bongo, badala ya miezi yako 4 utakaa hata wiki 2. Pia kama unatumia visa au kadi za benki za namna hii hakuna shida kwani ukipungukiwa unavuta tu. Globalisation phase III imeifanya bongo kuwa kama huko USA, hivyo wewe njoo tu. Kama unafikia hotel kuna za manzese za bei chini na zile kama 5 star (zina websites). Hivi toka uondoke huku bongo ndio unarudi kwa mara ya kwanza?
   
 9. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #9
  Jun 25, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  Kwani ukija unatafuta nyumba ya kupanga kwa miezi hiyo minne ..

  Life Bongo ndo kama ulivyoliacha hakuna mabadiliko zaidi ya mfumuko wa bei kuendelea kuongezeka
   
 10. R

  Renegade JF-Expert Member

  #10
  Jun 25, 2010
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 3,770
  Likes Received: 1,075
  Trophy Points: 280
  Karibu, kwani unakuja kwa mara ya kwanza? au? kama ni nyumbani una haja ya kuuliza bei , kwa maana Pamoja na ukali wa maisha Bongo bado tu wakarimu, ukitaka kufikia kwa mjomba sawa, au la kuna full furnished apartments kwa bei tofauti tofauti, lakini pia Guest za uswahilini ni nyingi sana, lakini zinataka uwe macho unaweza kuibiwa Vijisenti vyako, Kama una Visa Card ndo usiseme, Pia usiogope bei ya simu TIGO wako pia sana tu.
   
 11. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #11
  Jun 25, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,710
  Trophy Points: 280
  Kama umeweza kuishi kwa huyo mjaluo Obama utashindwa kuishi Bongo? We nenda tu maisha yaleyale tangu uhuru mabadiliko ni kidogo sana. Sema tu gap kati ya matajiri na masikini inazidi kuongezeka!
   
 12. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #12
  Jun 25, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  wakulu, mnamsimanga au mnamshauri?
   
 13. Who Cares?

  Who Cares? JF-Expert Member

  #13
  Jun 25, 2010
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 3,465
  Likes Received: 1,951
  Trophy Points: 280
  duuuh...yani mzee umekaa huko mpaka hujui hata ndugu zako tunaishije?...anyway...njoo na kama dola za kimarekani 500 kwa siku maisha yanaenda fresh tu...maana hata mie ndio nazotumia kila siku...ukitaka mchanganua sema nikupatie...kwa miezi 4 likely siku 120 X500= usd 60,000.. ila ukitaka ku-save au kubana matumizi itabidi tukuonyeshe maeneo ambayo hasheem thabit alikuwa anajificha kukwepa gharama za u-supa staa wake....

  Pia mkuu ukija na hilo range rover lako sport utakuwa umepunguza gharama za kutumia haya magari ya avis...ila ujuee mafuta yetu aka gasoline ime-chakachuliwa mbayaaaa...itaua engine ya gari lako...sikushauri kabsaa upande daladala...ni bora upande bajaj na bodaboda...ila ajali kibao mzee....hope pia hutopenda kukaa manzese ila kuna hotel kali kuliko hiyo kempinski....unaulizia pia bei ya mchele..kwani utakuja na wife apike?...ujue umeme hakuna na hotel hawaruhusu kujipikilisha vyumbani utawaunguzia jengo lao...usije na wife bana..utawanyima shavu dada zetu ...hao sikuhizi goli moja dola 100...sema wapo hata wa tshs 200 mitaa ya sewa buguruni pale...anyway...kuna sheraton out..msosi plate ya wali kuku kitu cha tshs 3000, soda tshs 500, ndizi mbivu tshs 200, maji yapo hata ya viroba tshs 100...

  KAKA WEE NJOO TU BANAAA...washkaji zako pia si unajua tumechoka...so kila jioni wewe ndio unakuwa pedeshee wetu full kuzungusha mi-bia pale mliman city....ohhh..kipo kijiwe kingine mitaa ya city centre pale gorofani kinaitwa sijui savana au...nimesahau sikuhisi kule huwa hata siendagi tena
   
 14. stringerbell

  stringerbell Member

  #14
  Jun 25, 2010
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ndio nikija natafuta nyumba ya kupanga ,sitaki kukaa kwa ndugu zangu kwasababu mimi very independent.
  naona jamani badala ya kunijibu maswali yangu mnanishambulia na kunirejeshea maswali mimi instead of giving me the idea hiyo cost of living .
  sababu ya kuuliza hivyo kwasababu mimi ni mtu wa budget sasa nataka kujua nichukue kiasi gani ili nipate kuwasaidia ndugu zangu pamoja na expenditure zangu mwenyewe.kuna mtu kaniambia nichukua 500 dollar lakini nahisi haitatosha kwa miezi 4 maybe one month is enouph.
  nawasikia watu kwamba maisha ni expensive siku hizi huko.
   
 15. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #15
  Jun 25, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,955
  Likes Received: 21,117
  Trophy Points: 280
  wabongo kama kawaida badala ya kukujibu wanaanza longolongo,jamaa anakuja anakaa miezi 4 anataka kujua aje na kiasi gani kwa muda huo,mwambieni vitu vya kueleweka sio we njoo tu maisha poa tu........
   
 16. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #16
  Jun 25, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,955
  Likes Received: 21,117
  Trophy Points: 280
  duh wewe sasa unataka asije kabisa..........
   
 17. AK-47

  AK-47 JF-Expert Member

  #17
  Jun 25, 2010
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kuna apartment hadi za dola 180 kwa mwezi zidisha mwenyewe mara miezi 4......gharama nyingine ni kama Tsh 150,000/= kwa siku kama hutaki makuu saana hivyo andaa kama USD 3000/=. Za kuwagawia ndugu zako zawadi na asante kwangu kwa kukupatia mchanganuo huu utajua mwenyewe. USD 1 ni sawa na tsh 1,400/= hivi.... I hope nimekusaidia.
   
 18. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #18
  Jun 25, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  Jamani wale wataala wa bajeti msaidieni si vibaya kuwa kuplan kila kitu ...

  Mie nashindwa pa kuanzia ..Nikianza na sukari mie napenda chai nadhani wakatu unaondoka uliacha kili sh 500 sasa ni 2000...
  Nyama sasa nadhani kilo 4000-5000 kwa kg
  Mchele huu kwa vile unapanda na kushuka nashindwa kusema
  endeleeeni
   
 19. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #19
  Jun 25, 2010
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  sema unakujaje utasaidiwa zaidi

  unakuja na familia yako
  utahitaji nyumba ya vyumba vingapi na maeneo gani
  utapenda kukodisha usafiri au haumind kupanda basi/ pia kuna bajaji which is very cheap
  mji gani unataka kufikia maana yake hata mwanza ni babu kubwa siku hizi
  je wewe unapenda ku socialize kiani gani 1. billicanas/ au beach/ au bar/ kwenda sehemu kama znz/ wewe ni mtu wa kula starehe sana au wastani

  ukijieleza zaidi utapewa ushauri mzuri zaidi
  utani na matusi visikukimbize

  bia 1400 kama ukinunua na kwenda kunywea nyumbani otherwise billicanas ni 5000
  soda 500 sehemu zingine wana bei zao
  nyama ukinunua kwenye butcher 4500
  kuku ni 7000
  mchele ukienda kununua gunia sokoni utapata cheap zaidi
  petrol 1650 per litre
  simu tigo thumni tu
  ukitaka kuenjoy miezi 4 njoo na 8000 usd
   
 20. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #20
  Jun 26, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  duu mkuu hiyo kwa miezi minne inatosha bambuuuuucha tu.
   
Loading...