#COVID19 Corona: Vifo vinazuilika tusijitabirie kwenye nadharia za kijinga

Serikali haina mamlaka ya kuikataa miito yetu labda kama haituwakilishi sisi.
Umesahau kauli ya Mwenyekiti kuwa madiwani hawakuchaguliwa na n=wananchi? Maana yake mwaka kura tulizopiga hazikuhesabiwa bali walipitisha watu wanaowataka kuanzia madiwani hadi rais
 
Haya yanayoongelewa humu na baadhi yetu yanasikitisha sana na bahati mbaya wenye weledi hawana nafasi ya kueleza ukweli.

Juzi kati nilikuwa kituo kimoja cha afya. Wasiwasi ya madaktari na manesi/wauguzi kuupata ugonjwa huu ilikuwa ni ya wazi kabisa na hivi ukizingatia wao wanakuwa mazingira hao muda wote.
 
Ni muda muafaka wa kujitegemea kiakili.
mkuu sio kwa hili. hizo nchi matajiri tu zinapiga kolabo.

hata hizi kampuni za kibeberu japo zina ukwasi wa hatari imebd ziungane kutengeneza hizi chanjo.

20210305_173711.jpg
 
Hujakatazwa kufuata chanjo, nenda katumie

Mijitu ya Lumumba mawazo yenu bora ya kuku.

Hakuna nchi moja iliyopata chanjo ya kutosha raia wake wote.

Achanjwe vipi nani kutoka wapi hali lengo ni kuchanja raia wote na chanjo haitoshi?

Kwa nini wanaanza watu wao walio hatarini zaidi?

Nchi ipi umesikia wewe inachanja wahedi?

Hovyoo!
 
Hizo chanjo hata mimi siziamini.

Kwa akili hii ya kuwa na fikra hasi, hutakuja kuamini chochote. Kwanini unatumia dawa ya malaria, je unaiamini kwa kuwa ulifanya utafiti au kwa kuwa hujasikia watu wakiisema ina madhara???

Kisayansi kila dawa ina madhara. Tofauti ni madhara yapi na kwa kiwango gani mtu atakuwa tayari kuyachukua!! Ikiwa hutaki madhara ya chanjo, chagua uwezekano wa kufa ukikupata!! Chagua kutumia fedha nyingi kupigana nao ukikupata! Chagua kuona biashara za utalii zikifa!!

Maisha ni kupanga na kuchagua! Na mleta mada anazungumzia sisi kupewa nafasi ya kuchagua. Kuna ubaya wowote uongozi wa nchi ukikubali chanjo na kigezo cha chanjo ikawa ni utashi?? Mbona hizi za surua, polio, pepopunda, dondakoo ni za lazima kwa watoto na mama waja wazito? Au unasema hazina madhara? Nani kakwambia hazina madhara??

Mkuu, kukana ama kukiri hakuondoi facts!!
 
Usione mtu anashinda kufungua nyuzi kila siku akililia chanjo ukadhani anahitaji kweli hizo chanjo,ni kwa sababu tu Magufuli hataki si ajabu kama serikali ingechukua chanjo ila za China pia ingekuwa maneno.
 
Back
Top Bottom