Corona: Siri ya mafanikio yetu katika hii vita

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,823
35,829
Mabibi na mabwana moja kwa moja kwenye mada.

Kwa mwendelezo wa updates kuhusiana na huu ugonjwa hapa nchini Tanzania, watake wasitake (wakiwamo mabeberu) wanacho cha kujifunza tokea katika mafanikio yetu.

Maeneo matatu muhimu kwenye mafanikio hayo wakiyadharau itakuwa imekula kwao vilivyo:

1. Ukomavu. Hapana kusikiliza kelele za vyura. Kukomaa kiutu uzima tu. Haipo Corona hapa. Kwisha!

2. Kuweka msitari wa mbele vitani, wasiokuwa wataalamu wabobezi wa fani husika. Mfano madaktari siyo wa kutanguliza mbele kwa ajili ya vita kali hii yenye kuhusiana na masuala ya afya!

3. Hawa wanaotumiwa na mabeberu muhimu wakatambuliwa na kupewa maelekezo. Mwenye Corona hana utaifa. Tanzania ikuhusishwa na Corona uraia au utambulisho hugeuka mara moja kuwa nchi ya kigeni au walau kuwa raia tokea nchi jirani!

Huyu hapa bado hajaelewa somo:

Sad News For Uganda, Kenya And Tanzania After More Cases of Covid-19 Keep Increasing

Huyu some analijua:

Rwanda registers first Covid-19 death

Vita ni vita mura!
 
Hizi ndio sababu za binaadamu ukiwa masikini wa fikra
1 Kumsingizia shetani/ibilisi ukifanya dhambi.
2 Mabeberu ukiwa huna uwezo wa kutengeneza ajira kwa wananchi wako.
3 Kuwatesa wapinzani wako kwa kusema wanatumika na mabeberu.

Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Hatujafanikiwa lolote. Tumeamua kuishi nao. Wa kufa watakufa uzuri hatutaisha.
 
Hakuna corona, mabeberu yanalazimisha Tanzania kuna corona,
Corona ipo wapi mbona hatuone wanaokufa au haya mafua tu ya kawaida ndio corona?
Kama ndio hivyo basi corona haina nguvu kama tunavyoaminishwa
 
Pana mtu alisema: "usingoje igonge mlangoni kwako ndipo ujue kuwa ipo". Mwisho wa kumnukuu.
 
Je unakula kitimoto🐷🐖🐽? Je wewe ni Msabato Safi na hauvuti sigara, hunywi pombe, na huli haramu?
Je wewe ni Muislam Safi na huli najisi yoyote, Wala hunywi 🥃🍻?
Je wewe unavuta sigara, unakula K na kitimoto 🐷🐖🐽?
Amini nawaamboa life span yet wote sawa.
Wengi hufa kuanzia miaka 60.
Wee jiachie tu.
Kuna mzee mmoja alipigwa ngwala kimo Cha mbuzi na BASHITE, anakunywaga ngumu kumeza.... Mzimaaa wa Afya njema.
Salim A. Salim havuti, hanywi yaani Safi lakini afya ndio spana mkononi.
Hebu tusitishane sijui usinywe soda, usile chumvi, usile kitimoto 🐷 🐖🐽, usile K, sijui usile Nini..... Wee kula tu.
 
Yule Mzee aliyepigwa na bashite anavuta cigar hadi anapoteza pumzi.
Na kuhusu corona ni kwamba sisi hatupimi hio ndio siri ya mafanikio yetu
 
Hakuna kweli corona, nilipo huku kuna vikongwe wengi kweli miaka 80+,k
Corona ilipopamba moto nikawa nawaona na mfua tu nikadhani hapa tuwepoteza lakin wapi
Wapo wanadunda tu hakuna cha barakoa Wa mini,hata hivyo Mimi mwenyewe sijawahi kuvaa barakoa Wa kuona mgonjwa amekufa na corona.Isipokuwa matajiri ndio wanakufa tu
Pana mtu alisema: "usingoje igonge mlangoni kwako ndipo ujue kuwa ipo". Mwisho wa kumnukuu.
 
Hakuna kweli corona, nilipo huku kuna vikongwe wengi kweli miaka 80+,k
Corona ilipopamba moto nikawa nawaona na mfua tu nikadhani hapa tuwepoteza lakin wapi
Wapo wanadunda tu hakuna cha barakoa Wa mini,hata hivyo Mimi mwenyewe sijawahi kuvaa barakoa Wa kuona mgonjwa amekufa na corona.Isipokuwa matajiri ndio wanakufa tu

Mkuu ipo taabu moja kuhusu Corona. Kama upimaji makini haupo ni rahisi sana kutodhani kuwa Corona ipo na kuwa inauwa.

Kwa msimamo tuliouchukuwa kama nchi katika moja ya hatua kunapo mafanikio yetu, tuna discourage upimaji na haswa wa maiti.

Mtu alikuwa na ukimwi au kisukari kwa miaka 20 iliopita anakufa ghafla. Si lazima kuwa kafa kwa ukimwi au kisukari. Anaweza kuwa kachomwa kisu au hata kafa kwa malaria.

Ilikuwa muhimu kupima kama nia ingekuwapo kujiridhisha.

Hatari moja katika huu muarobaini wetu ni kuwa watu wanabweteka na umuhimu wa tahadhari unakuwa haupo tena.

Ni wazi kuwa pana watu tunaweza kuwa tumewapoteza kwenye hii puuziaji ambapo wangali kuwa wamechukua tahadhari zaidi kama ukubwa wa tatizo ungelikuwa umewekwa wazi kwao.
 
With this global village we living in, it is going to be so difficult to say goodbye to corona at least for now.
International travel was the main reason why corona spread so fast from one country to another. Exponential increase in corona cases is what scares me the most bearing in mind the fact that our boarders are so porous and the task to defend them is monumental. That's why there are still some lingering corona virus cases in China to date although tremendous success has been realized in combating corona virus.
So, with that said, we should continue taking necessary precautions as advised by health officials as the pandemic is winding down. For our case, we have fared very well compare to other countries due multiple strategies used one being prayers. I can't thank God enough for making this possible because the earlier predictions of Africans dying like locusts didn't materialized. It's not over until it's over.
Be safe.
 
Jambo moja kubwa na la msingi sanaa kwa Tanzania ni kwamba tumepata Rais shupavu na mwenye akili kubwa.
 
Mabibi na mabwana moja kwa moja kwenye mada.

Kwa mwendelezo wa updates kuhusiana na huu ugonjwa hapa nchini Tanzania, watake wasitake (wakiwamo mabeberu) wanacho cha kujifunza tokea katika mafanikio yetu.

Maeneo matatu muhimu kwenye mafanikio hayo wakiyadharau itakuwa imekula kwao vilivyo:

1. Ukomavu. Hapana kusikiliza kelele za vyura. Kukomaa kiutu uzima tu. Haipo Corona hapa. Kwisha!

2. Kuweka msitari wa mbele vitani, wasiokuwa wataalamu wabobezi wa fani husika. Mfano madaktari siyo wa kutanguliza mbele kwa ajili ya vita kali hii yenye kuhusiana na masuala ya afya!

3. Hawa wanaotumiwa na mabeberu muhimu wakatambuliwa na kupewa maelekezo. Mwenye Corona hana utaifa. Tanzania ikuhusishwa na Corona uraia au utambulisho hugeuka mara moja kuwa nchi ya kigeni au walau kuwa raia tokea nchi jirani!

Huyu hapa bado hajaelewa somo:

Sad News For Uganda, Kenya And Tanzania After More Cases of Covid-19 Keep Increasing

Huyu some analijua:

Rwanda registers first Covid-19 death

Vita ni vita mura!
Wewe unajua wazi kwamba Tanzania tumefanya kituko kwa namna tulivyoikabili corona; takwimu hakuna, usiri mkubwa, kuzika usiku, kutokufanya mambo kwa weledi, n.k halafu ndio unasema tumefanya mambo kwa ukomavu?...Unafanana sana na boss wako kwenye ile suti yake maarufu.0
 
Mkuu nakuelewa kabisa machungu uliyokuwa nayo.

Lakini tuko hapa mkuu. Nyomi kila mahali na hata kanisani alikokuwa mzee baba jana kulikuwa hata nafasi ya kupenyeza mguu ilikuwa hamna. Hakuna barakoa wala nini.

Hali kama ile huoni kuwa kuna point kuwa ugonjwa huu kwishney!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom