CORONA: Madereva wa Tanzania bado wanazuiwa mpakani, TATOA Watoa tamko

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,293
24,177
June 8, 2020

Chama cha wamiliki wa Malori Tanzania (TATOA) Tanzania Truck Owners Association :: Home wameonesha masikitiko yao kwa nchi jirani na Tanzania kufuatia muendelezo wa kuzuiliwa madereva wa malori wanaotoka Tanzania kuvuka mipaka kwa madai ya kuwa madereva hao wana maambukizi ya virusi vya Corona.

TATOA inasema kuwa hili suala la changamoto mipakani na nchi jirani issue siyo Covid-19 bali kuna kitu nyuma ya pazia.
Maana hakuna dereva anayeingia bandarini bila cheti cha kupimwa Covid-19 lakini madereva wa malori wakifika mpakani na nchi jirani vyeti hivyo vya afya njema havitambuliwi na serikali ya nchi jirani.

Chanzo: Global TV Online
 
June 8 , 2020

Hali tete kwa wamiliki wa malori yaliyokwama Namanga/watakiwa kulipa fidia

Wenye magari waingia hofu baada ya wenye mizigo kuonesha watawadai. Wamiliki hao wa malori ya Tanzania wamesema mizigo iliyokwama mingine ni ya viwandani kama viwanda vya soda, bia, baruti za migodini n.k ambao wamesema kutokana na masuala mtambuka vinaweza kufungwa, ajira kupunguzwa kutokana na mizigo hiyo kukwama.

Source : ITV Tanzania
 
Tanzania tumeshasema hakuna Corona. Wenzetu wanaamini Corona ipo. Kwa hiyo ni haki yao kuwalinda raia wao. Kila anaekwenda kwao lazima wampime wenyewe. Nawaunga mkono. Hawataki mambo ya kipuuzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nao wanasubiri serikali itoe tamko!? Cut the supply kila mtu ashinde mechi zake!
 
June 8, 2020

Chama cha wamiliki wa Malori Tanzania (TATOA) Tanzania Truck Owners Association :: Home wameonesha masikitiko yao kwa nchi jirani na Tanzania kufuatia muendelezo wa kuzuiliwa madereva wa malori wanaotoka Tanzania kuvuka mipaka kwa madai ya kuwa madereva hao wana maambukizi ya virusi vya Corona.

TATOA inasema kuwa hili suala la changamoto mipakani na nchi jirani issue siyo Covid-19 bali kuna kitu nyuma ya pazia.
Maana hakuna dereva anayeingia bandarini bila cheti cha kupimwa Covid-19 lakini madereva wa malori wakifika mpakani na nchi jirani vyeti hivyo vya afya njema havitambuliwi na serikali ya nchi jirani.

Chanzo: Global TV Online

TUMECHOKA NA HIZO NGONJERA.UKITAKA KUINGIA KWENYE NYUMBA YA MTU FUATA MASHARTI YAKE.MBONA WATZ TUNAOGOPA SANA VIPIMO VYA MAJIRANI ZETU?KAMA WEWE HUNA COVID HUNA TU NA KAMA UNAYO UNAYO TU
 
TUMECHOKA NA HIZO NGONJERA.UKITAKA KUINGIA KWENYE NYUMBA YA MTU FUATA MASHARTI YAKE.MBONA WATZ TUNAOGOPA SANA VIPIMO VYA MAJIRANI ZETU?KAMA WEWE HUNA COVID HUNA TU NA KAMA UNAYO UNAYO TU

Tusiburi Diplomasia ya kujinafasi (geopolitics) inayoongozwa na mwanadiplomasia namba 2 wa serikali ya Tanzania chini ya CCM Mpya Mh. Prof. Palamagamba Kabudi kama ataweza kuwa na ushawishi wa kuwaaminisha Rwanda , Kenya na Uganda kuwa Tanzania ni salama salmini na hakuna visa vya Covid-19 kama nchi beberu za Ulaya na Marekani ya Kaskazini zinazodai kuwa ipo na lazima uwazi wa taarifa uwepo kuhusu hali ya maambukizi Tanzania.
 
Kama wamepimwa hapa nyumbani na kukutwa hawana COVID19 kisha wakapewa certificates zinazoisha muda wake kwa siku 14 kwa nini wasipimwe tena wakitakiwa kupimwa ili waruhusiwe kuingia nchi jirani?
Malumbano na malalamiko ni ya nini? Wakitaka kupeleka uswahili wa serikali yetu huko Kenya wataumia kwa kuwa wenzetu huko wako serious na vipimo, kisayansi siyo ki-Madagascarian.
 
June 9 , 2020

Waziri wa Uchukuzi - Kuna changamoto mipaka ya Rwanda, Kenya, Zambia ila siyo Burundi

Hayo yamesemwa na waziri wa uchukuzi, mawasiliano Injinia Isack Kamwelwe pamoja na kuwa nchi za EAC na SADC zilikubaliana kuwezesha mizigo inayobebwa na malori lakini kuna changamoto za kurahishisha malori na madereva kuvuka mipaka bila vikwazo sharti wawe na vyeti safi vya kutokuwa na virus vya Corona lakini mambo yanakwenda ndivyo sivyo.

Hivyo waziri wa mambo ya nje Prof. Palamagamba Kabudi atasimamia kuitisha nchi za Rwanda, Zambia na Kenya kutatua sintofahamu inayoendelea mipakani.
 
Back
Top Bottom