#COVID19 Serikali yatoa angalizo maambukizi mapya ya Corona

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Serikali ya Tanzania imesema kuna viashiria vya wimbi la tatu la ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona kuingia nchini kutokana na nchi jirani wananchi wake kuzidi kupata maambukizi ya ugonjwa huo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi Juni 19, 2021 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) mkurugenzi wa kinga wa Wizara ya Afya, Dk Leonard Subi ametoa maagizo kadhaa likiwemo la kuwataka wananchi kuvaa barakoa.

“Wizara inawakumbusha wananchi wote kutopuuza ugonjwa wa Covid-19. Wizara imeanza kuona viashiria vya kutokea kwa wimbi la tatu la mlipuko wa ugonjwa huu katika nchi yetu.”

“Hii ni kutokana na taarifa za ufuatiliaji wa mwenendo wa ugonjwa huu zinazofanywa na wizara na mwingiliano kati ya watu wetu na mataifa mengine,” amesema Dk Subi.

Amesema idadi ya wagonjwa wanaokutwa na vizuri vya corona barani Afrika imeongezeka ndani ya wiki tano mfululizo zikiwemo nchi jirani na Tanzania, “maambukizi yanaongezeka maradufu kuliko ilivyokuwa wimbi la pili.”

Katika maelezo yake amewataka wananchi kuchukua tahadhari kwa kuvaa barakoa, kutumia vitakasa mikono na kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni.

Chanzo: Mwananchi
 
FB_IMG_1624005081350.jpg
 
MAGUFULI NA WACHUNGAJI FEKI walisema mungu wao kaiponya Tanzania wakati huo huo wanaficha data.

Pimeni watu tujue kama tumeponywa au lah!
Pale Mwananyamala kuna wodi maalum ya changamoto ya upumuaji/Corona/Covid19 na ipo full hadi sasa hivi.
 
Uganda walichanjwa lakini wapi, hii Corona dawa ni kutoipa attention tu, kuvaa barakoa nako ni kama bahati nasibu, mimi nikivaa majirani zangu hawana habari nayo, na sidhani kama barakoa zinazuia 100% nyungu nayo haijathibitishwa popote, maombi?! kwani waganda hawamjui Mungu!, au Mungu ana upendeleo!, sijui tunahitaji kitu gani zaidi kuhusu huu ugonjwa ili tujikinge.
 
Uganda walichanjwa lakini wapi, hii Corona dawa ni kutoipa attention tu, kuvaa barakoa nako ni kama bahati nasibu, mimi nikivaa majirani zangu hawana habari nayo, na sidhani kama barakoa zinazuia 100% nyungu nayo haijathibitishwa popote, sijui tunahitaji kitu gani zaidi kuhusu huu ugonjwa ili tujikinge.
Tumia bupiji, corona haikatizi ukipiga hii kutwa mara tatu🤣🐒🤸
20210214_210803.jpg
 
Amefariki?
asee nna ndugu yangu alitembelea pande hizo siku za karibuni..
amefika juzi hapa anaumwa akachukua tax imkimbize hospital hata hakufika maana mbavu zilimbana akihema unasikia miruzi tuu
 
Back
Top Bottom