Corona: Kirusi kipya cha India kwa mujibu wa Daktari kutoka Muhimbili

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
28,085
36,063
Mabibi na mabwana taarifa mpya za kitalaamu, hizi ni muhimu sana kwetu kwenye kujilinda na hili gonjwa.

Inatia moyo madaktari wetu wanapoendelea tuhabarisha tusijisahau.

Hatuna sababu ya kudanganyana.

Huu ndiyo ulio ukweli mchungu:

====

By Herieth Makwetta

Dar es Salaam. Wataalamu wamesema aina mpya ya virusi vya corona ‘double mutant’, ambavyo vimeonekana nchini India ni hatari zaidi kutokana na uwezo wake wa kubadilika mara kwa mara.

Kirusi hicho kipya aina ya B.1.617 ndicho kinaelezwa kuwa wimbi la pili kuipiga India, ambayo imeshuhudia maambukizi kufikia zaidi ya milioni 21 huku vifo vikifikia 230,168 hadi kufikia jana mchana.

Akizungumza na Mwananchi, Mtaalamu wa maicobaolojia na virusi kutoka Chuo kikuu cha Muhimbili (Muhas), Dk Joel Manyahi alisema aina hiyo ya kirusi kina tabia ya kujibadilisha mara kwa mara.

“Kirusi hicho hicho kinajibadilisha kidogo kinachukua chembechembe nyingine ya jeni (gene) inatengeneza rangi nyeupe kidogo au hufifia na hujiweka kwa binadamu au mnyama.

“Kina tabia ya kutumia protini, kinajibadilisha kidogo ili kuwa orijino, kinajibadilisha mara mbili, kama kilikuwa A kinabadilika kuwa B halafu baadaye kinakuwa C, kikifanya mabadiliko kinakuwa kirusi kingine ili kiweze kuenea kwa urahisi zaidi,” alisema Dk Manyahi.

Wakati wanasayansi wakiwa katika uchunguzi kuhusu aina mpya ya kirusi cha Corona kinachoua nchini India, wataalamu wa afya nchini wametoa angalizo huku wakitaja mbinu mbalimbali zitakazosaidia kuepukana na kirusi hicho.

Madaktari wameiomba Serikali kupunguza mwingiliano wa watu, kuongeza upimaji na taasisi zenye uwezo ziruhusiwe kupima na nchi iandae hospitali za dharura zenye oksijeni za kutosha.

Wameonya kuwa Tanzania inapaswa kutokana na wimbi la corona nchini India. Daktari Bingwa wa magonjwa ya ndani na yanayoambukiza kutoka Hospitali ya Aga Khan, Mandela Makakala alisema virusi vya corona vinabadilika badilika sana na vinaweza kuwa hatari zaidi ya tunavyofikiria kwa kuongezeka uwezo wa kusambaa zaidi na makali ya ugonjwa.

Alisema yatupasa kujitathmini kama nchi tumejiandaa vipi kupambana na wimbi la corona litakalokuja. “Madaktari tulio wengi tunadhani ni muhimu kuanza kutoa chanjo kwa makundi yaliyo katika hatari kubwa, yaani watumishi wa afya, wazee na wagonjwa wanye matatizo ya kiafya kama sukari, shinikizo la damu, magonjwa ya moyo na uzito kupita kiasi,” alisema.

Dk Mandela alisema ni muhimu kupunguza mwingiliano wa watu katika nchi ambazo zina wagonjwa wengi wa corona.

Wataalamu: Kirusi cha India balaa, hatua zichukuliwe kuikabili corona

Ninawasilisha.
 
Kuna kitu hakiko sawa,
juzi kati hapa wakati wa mwendazake tuliambiwa Tanzania kuna Mutant ya hatari mno (mara 10 zaidi) ya virusi vyote vya corona, na wasafiri waliokuwa wanatoka tz walikua wanapimwa na kukutwa navyo, sasa najiuliza hiyo mutation ya tz imepotelea wapi, mbona tena india?

Jambo la pili, ukiangalia hyo rate ya walioambukizwa na waliokufa hamna tofauti yoyote na kile kirusi cha kwanza, maana tokea mwanzoni kabisa wanaokufa kwa corona ni chini ya 5% ya waliopata, na hata sasa hyo ya india rate iko vile vile, sasa huo ukali ukoje?
 
Civil servants wote -- utakuwa unamwunga mkono Prof. Assad. Yeye alitambua hata serikalini 60% ya viongozi ni mbumbumbu wasiokuwa na tija yoyote kwa taifa.

Very serious allegations. Kama zako tu mkuu.
Least but all. Sasa kwan' efficiency hubadilika kila regime?!
 
Mabibi na mabwana taarifa mpya za kitalaamu, hizi ni muhimu sana kwetu kwenye kujilinda na hili gonjwa.

Inatia moyo madaktari wetu wanapoendelea tuhabarisha tusijisahau.

Hatuna sababu ya kudanganyana.

Huu ndiyo ulio ukweli mchungu:

====

By Herieth Makwetta

Dar es Salaam. Wataalamu wamesema aina mpya ya virusi vya corona ‘double mutant’, ambavyo vimeonekana nchini India ni hatari zaidi kutokana na uwezo wake wa kubadilika mara kwa mara.

Kirusi hicho kipya aina ya B.1.617 ndicho kinaelezwa kuwa wimbi la pili kuipiga India, ambayo imeshuhudia maambukizi kufikia zaidi ya milioni 21 huku vifo vikifikia 230,168 hadi kufikia jana mchana.

Akizungumza na Mwananchi, Mtaalamu wa maicobaolojia na virusi kutoka Chuo kikuu cha Muhimbili (Muhas), Dk Joel Manyahi alisema aina hiyo ya kirusi kina tabia ya kujibadilisha mara kwa mara.

“Kirusi hicho hicho kinajibadilisha kidogo kinachukua chembechembe nyingine ya jeni (gene) inatengeneza rangi nyeupe kidogo au hufifia na hujiweka kwa binadamu au mnyama.

“Kina tabia ya kutumia protini, kinajibadilisha kidogo ili kuwa orijino, kinajibadilisha mara mbili, kama kilikuwa A kinabadilika kuwa B halafu baadaye kinakuwa C, kikifanya mabadiliko kinakuwa kirusi kingine ili kiweze kuenea kwa urahisi zaidi,” alisema Dk Manyahi.

Wakati wanasayansi wakiwa katika uchunguzi kuhusu aina mpya ya kirusi cha Corona kina[1] choua nchini India, wataalamu wa afya nchini wametoa angalizo huku wakitaja mbinu mbalimbali zitakazosaidia kuepukana na kirusi hicho.

ADVERTISEMENT
Madaktari wameiomba Serikali kupunguza mwingiliano wa watu, kuongeza upimaji na taasisi zenye uwezo ziruhusiwe kupima na nchi iandae hospitali za dharura zenye oksijeni za kutosha.

Wameonya kuwa Tanzania inapaswa kutokana na wimbi la corona nchini India. Daktari Bingwa wa magonjwa ya ndani na yanayoambukiza kutoka Hospitali ya Aga Khan, Mandela Makakala alisema virusi vya corona vinabadilika badilika sana na vinaweza kuwa hatari zaidi ya tunavyofikiria kwa kuongezeka uwezo wa kusambaa zaidi na makali ya ugonjwa.

Alisema yatupasa kujitathmini kama nchi tumejiandaa vipi kupambana na wimbi la corona litakalokuja. “Madaktari tulio wengi tunadhani ni muhimu kuanza kutoa chanjo kwa makundi yaliyo katika hatari kubwa, yaani watumishi wa afya, wazee na wagonjwa wanye matatizo ya kiafya kama sukari, shinikizo la damu, magonjwa ya moyo na uzito kupita kiasi,” alisema.

Dk Mandela alisema ni muhimu kupunguza mwingiliano wa watu katika nchi ambazo zina wagonjwa wengi wa corona.

Ninawasilisha.
Watetezi wa kupiga nyungu mbona kimya kabisa!
 
Tanzania tumelindwa na Mungu dhidi ya corona hadi sasa kwa kuwa viongozi walitamka hadharani kumtanguliza Mungu mbele ya mambo mengine katika vita dhidi ya çorona! Kama tukajidanganya na kutanguliza akili zetu na kuiga mataifa mengine kwa homa kuwa sisi siyo kisiwa ni kujiangamiza!
Kumbuka mataifa yanayoteseka yanavaa sana barakoa!!
 
Back
Top Bottom