Serikali ya Tanzania na hasa kiongozi wetu mkuu amerudia mara nyingi kuwa hatuna ugonjwa wa Covid-19 na wote tumeshuhudia ya kuwa kambi na wodi zilizokuwa zimetengwa zilifungwa tangu mwaka jana.Hili ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu.
Jambo moja ambalo binafsi sikubaliani nalo ni hili la kuweka matumaini makubwa katika dua na maombi na kuanza kulegeza taratibu zingine za kujikinga. Duniani wanaoathirika na Covid wengine ni wacha Mungu kuliko hata sisi na hatuna ubora wa kiimani kuliko wao.
Naamini ya kuwa mafanikio makubwa tuliyopata mwaka jana pamoja na hizo dua na maombi ni kuanza kuchukua hatua mapema kuhamasisha watu kwa kupitia njia mbalimbali.
Ugonjwa upo South Africa, Malawi, Kenya na Uganda achilia mbali Burundi na Rwanda na kwa mantiki hiyo ni suala la muda tu.
Serikali iendelee kutangaza kuwa hakuna Covid-19 lakini irudishe uhamasishaji wa kujikinga. Barakoa katika public places (hasa daladala) iwe lazima, vifaa vya kunawia mikono sehemu za biashara virudishwe, shule zote taratibu za awali ziwekewe mkazo.
Kwa kuwa ugoNjwa umeonyesha kuwa na athari kubwa kwa watu walio na magonjwa mengine (co morbidity kama kisukari, Pressure na HIV), kliniki za magonja haya ziwekewe utaratibu mzuri.
TANZANIA KORONA HAKUNA ILA KWA JIRANI IPO!