Kwako Rais wetu mpendwa, jembe letu la ukweli, mzee baba, Dr. Magufuli.
Protokali yote imezingatiwa.
Mengi yameandikwa, shauri mbalimbali zimetolewa tangia kabla sana ya ugonjwa huu kuingia nchini takribani miezi miwili sasa.
Ugonjwa uliopaswa kuzuiliwa kuingia, uliingia nchini. Pia ugonjwa uliopaswa kudhibitiwa usisambae haujadhibitiwa na unaendelea kusambaa.
Haitusaidii kuendelea kuoneana aibu. Haitusaidii kuendelea kuficha maradhi. Wala haitusaidii kuacha kuelezana ukweli wazi wazi kwa maana msema kweli ni mpenzi wa Mungu.
Hadi tulipofikia naamini tunakubaliana sote kuwa hatuna jipya tena tokea kwa watendaji wetu waliopewa jukumu la kuudhibiti na hata kuutokomeza kabisa ugonjwa huu kutoka hapa nchini.
Mengine yote ni historia au yatokanayo na historia hiyo.
Mzee baba, tunakupenda sana na ni nia yetu sisi tunaoamini kuwa tu wengi, uendelee kutuongoza ikibidi hata baada ya 2025. Ila mheshimiwa, kwa sasa tunakuomba wewe mwenyewe ulione hili pamoja nasi kwa dhati kabisa:
Mzee baba, tunakuomba tujadiliane mbinu mpya za kupigana katika vita hivi mapema kabla hatujashindwa kabisa.
Tunakuomba mzee baba, iundwe tume nyingine yenye madaraka kamili ya kuongoza vita hii kama itakavyoona yenyewe kuwa inafaa. Ufanisi wake upimwe kwa vigezo vilivyo wazi.
Ni jambo la heri tu mkuu kuwa, wapo wana wa nchi hii wengi tu na wenye uzalendo uliotukuka, wanaoweza kukusaidia kuondosha gharika hili na kulitokomeza kabisa.
Mzee baba, tunayo nafasi ya kurejea katika maisha yetu ya kawaida (na mashule hata yakafunguliwa) ndani ya siku 45 tukiwa salama.
Kwa nini tusijipe nafasi katika kufanikisha jambo hili lenye tija kuu kama hili kwa nchi yetu?
Ni wazi kuwa, kuna maisha mengi yatakayookolewa kwa jitihada kama hizi, ambapo itakuwa ni thawabu kubwa kwako hapa duniani na hata huko mbinguni.
Eeeh mzee baba, hebu yaone haya kwa moyo mweupe, ukayajaribu.
Kwa hakika hautajilaumu.
Ninawasilisha.