Mahakama yamng’ang’ania baba aliyembaka mwanae

Oldmantz

JF-Expert Member
Jan 24, 2023
430
998
Mahakama Kuu Kanda ya Songea, imemng’ang’ania dereva bodaboda (jina linahifadhiwa) aliyefanya mapenzi kwa nguvu na mwanawe wa kumzaa akisingizia ni maelekezo ya mganga wa kienyeji na kusisitiza kuwa kifungo cha miaka 30 alichopewa ni sahihi.

Tukio hilo lililotokea Machi 13, 2023 katika kijiji cha Subira katika Manispaa ya Songea ambapo baba huyo alifanya mapenzi na mwanae wa kumzaa miaka 17.

Hukumu hiyo imetolewa leo Oktoba 19, 2023 na Jaji Upendo Madeha, ikiwa ni siku chache tu baada ya Polisi wa Mkoa wa kipolisi wa Rufiji, kumkamata mzee mwingine (jina limehifadhiwa) akituhumiwa kumgeuza mwanawe wa kumzaa kama mke na kuzaa naye watoto watatu.

Matukio hayo yanaonekana kuongezeka nchini kwa baba kufanya mapenzi ama kwa nguvu, kuwalaghai au kwa imani za kishirikina na watoto wao wao wa kike na katika baadhi ya matukio ya aina hiyo ni ya baba kulawiti mtoto wake.

Katika hukumu yake ya rufaa iliyotolewa na Jaji Madeha leo, mtoto mwenyewe ambaye jina lake limehifadhiwa ndiye aliyetoa ushahidi uliomkaanga baba yake.

Mtoto huyo kulingana na hukumu hiyo, ameieleza mahakama ya Wilaya ya Songea kuwa Machi 13, 2023, baba yake alirudi saa 6:00 usiku ambapo alipoingia ndani na kuketi katika makochi, alimweleza ana jambo anataka wazungumze.

Baba ambaye sasa anatumikia kifungo cha miaka 30 ambacho mahakama kuu Songea imekibariki, alimtaka asiwe na wasiwasi na kumweleza kuwa ana tatizo ambalo angehitaji mwane huyo mwenye umri wa miaka 17 amsaidie kulitatua.

Alimuuliza kama anajua kuwa ana kutoelewana na mama yake, lakini akamwambia hafahamu ndipo akamweleza kuwa alikwenda kwa mganga wa kienyeji aliyemueleza kuna watu wana mloga na yeye ndio mtu pekee wa kumsaidia.

Kwa mujibu wa mtoto huyo, baba yake wakati anamshawishi alionekana kuwa na hasira na kumtaka mwanae huyo amkalie kwenye mapaja, kauli iliyomfanya mtoto akimbie kuelekea kwenye chumba cha watoto wa kiume, ambapo baba alimfuata na kumkamata na kumrudisha sebuleni.

Hapo alimsukuma mtoto wake kwenye sofa, kumvua nguo na kumuuingizia uume wake na alipomaliza, baba alikwenda chumbani kwake kulala ambapo siku iliyofuata mwanae aliamua kumuleza mwalimu wake kila kitu kilichomtokea.

Ni kutokana na ushahidi huo na wa mashahidi wengine akiwemo mwalimu wa shule ya sekondari ya Londoni aliyetoa taarifa za tukio hilo na daktari aliyemfanyia uchunguzi mtoto, mshitakiwa alitiwa hatiani na kuhukumiwa miaka 30.

Hata hivyo, hakuridhika na hukumu hiyo ambapo alikata rufaa akiegemea sababu mbili kuwa Hakimu aliyemfunga alikosea kisheria kwa kuwa upande wa mashitaka haukuthibitisha shitaka hilo na pia hakuzingatia ushahidi wake wa utetezi.

Jaji Madeha alitupilia mbali sababu hizo na kueleza kuwa ameridhika kuwa upande wa mashitaka uliweza kuthibitisha shitaka hilo kwa viwango vinavyokubalika kisheria na ushahidi wa mtoto, ulitosha kabisa kumtia hatiani.

“Kwa ufahamu wangu, naona shitaka la kufanya mapenzi na ndugu wa damu lilithibitishwa bila kuacha mashaka kwa kuwa ushahidi uliopo unathibitisha mrufani kufanya mapenzi na mwanae kwa imani za kishirikina,” alisema Jaji.

Kuhusu utetezi wake katika mahakama ya wilaya ya Songea kuwa alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa Ngiri na kwamba uume wake haufanyi kazi, Jaji alisema mrufani alishindwa kuthibitisha na pia utetezi wake ulijichanganya.

Jaji Madeha alisema wakati baba akisema alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya ngiri, lakini mashahidi wake wawili aliowaita kumtetea walisema alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Figo, hivyo kushindwa kuthibitisha maradhi yake.

Kutokana na maelezo hayo, Jaji Madeha alisema rufaa hiyo haina mashiko kwa ujumla wake na haoni sababu ya kubatilisha kutiwa kwake hatiani na hukumu ya kifungo cha miaka 30 aliyopewa hivyo akaamuru aendelee kutumikia adhabu hiyo.

CREDIT: MWANANCHI
 
Hahaaaa, Mwanaume ni mwanaume tuu, kuna kesi nilisikia jamaa naye alijitetea kua hadindishi, Wazee wakamuweka vishawishi, hahaaaa alikaza sanaa, kilichofuata ni kubana miguu kuzia mzigo usiinuke sana,
Halafu akiona ngoma inainuka anaanza kuliaa.
 
Back
Top Bottom