Ama kweli raha jipe mwenyewe. Ukisubiri mwingine kukupa raha, mbona waweza kusubiria mno?
Tumetangaziana kwa bashasha kuwa tumeshashinda vita. Wagonjwa wamekuwa wakipungua tokea mamia hadi mamoja. Haiyumkiniki kwa mwendo huo kufikia sasa, si haba Corona itakuwa kwishney!
Vita hii si ndogo kwani wenzetu wengi hata walio washupavu mno kuliko hata sisi wangalimo bado kulia wala kushoto kungali kufahamika.
Cha ajabu na kweli katika mazingira ya kawaida ushindi huwa haukosi pongezi tokea kwa washirika yaani ndugu na marafiki.
Sasa huu ushindi wetu usiokuwa na pongezi tokea kokote isipokuwa chereko chereko za kivyetu vyetu peke yetu na mh. Makonda tu utakuwa ushindi wa namna gani huu?
Hatuna washirika kweli hata wa kukodi tu? Hata Burundi ambako rais wao mteule atakuja kututembelea sisi kama priority 1 wameshindwa kutupongeza hata kwa kutupaka mafuta kwa mgongo wa chupa na tuko vizuri tu?
Kwa mwendo huu, pana hatari kuwa ushindi wetu huu unaweza kuwa na walakini au wa kimagumashi kama kwingine wanavyoita. Waswahili wanasema "hala hala kabla ya hatari".
Haya mengine ya kuitana majina kuwa ooh pana watu walipenda watanzania wafe kama nzige mbona itakuwa kujaribu kujishasha tu ili kujaribu kuzima mawazo huru pasipo kuwa na hoja?
Kwa nini mtu awe na maslahi yoyote kwa watanzania kufa? Kwanini isiwe kwa warundi, wacongo, wasauzi, wajamaica, wajerumani nk kufa? Kwa nini hakuna nchi yoyote ile duniani yenye mawazo kama haya? Mawazo duni kabisa.
Tupende tusipende, pana vitu (na si kidogo) upande wetu na hii vita haviko sawa hata kidogo.
Pasipo na kupepesa maneno, ushindi huu tunaojinasibu nao utakuwa uko fyongo.