Simuamini tb joshua na ninashangaa watu wanaacha wapakwa mafuta hapa wanakimbilia jina alafu tangu lini uponyaji ukauzwa eti anauza maji pia izo stika zake zinamsifia tu yeye na sio Mungu nakumbuka kuna kipindi alikuwa anakusanya wagonjwa wa kuombea hapa tz sharti no.1 ni kwamba uwe na cheti kutoka hospitali ya serikali kudhibitisha ugonjwa wako bila hivyo uombewi ivi kwa ikristo wa kawaida tu kunakujiorodhesha kwenda kupokea uponyaji kwa details ni Mungu gani huyo anehitaji details za ugonjwa na mgonjwa? kuna mambo mengi sana huyu baba anashangaza kama utafutilia kwa makini tv yake pia iweje ukimsaidi mtu umbandikie kiasi ha fedha kwenye baasha wakati neno linasema utoapo ata mkono wako wa kushoto usijue kilichotolewa na mkono wa kulia!!
Hasason, huhitaji kumwamini mtu yeyote maana vitu vyote ni watumishi wa Mungu na hivyo Mungu anaweza kutumia chochote akitakacho katika kukamilisha makusudi yake. Biblia inaonyesha alitumia hata punda wa Balam alinena. Na Mungu alitumia, udongo, moto, kijiti, vazi ya Elia/Elisha, Mate na udongo, maji, vazi la Yesu,fimbo,maneno ya kinywa n.k. Lakini pia Mungu amekuwa akitumia watu wa aina zote, wanawake, wanaume, wazee, vijana, watoto, bila kubagua social status.
Zaidi ya yote, Bwana Yesu Kristo alifanya mambo mengi sana kwa mifumo mbali mbali kiasi hata wale wanafunzi wake, kina Petro, Yohana, Mathayo na wengine wote walimshangaa japo walikuwa naye wakati wote akiwafundisha. Kabla hajapaa, kwenda kwa Baba alisema "Wamuaminio watafanya aliyoyafanya na kuzidi".
Unapoquestion uponyaji unaofanyika kwa njia ya Imani, unatakiwa uwe na vigezo sahihi vya Ki Biblia. Ni kweli Biblia inasema msiamini kila roho bali zijaribuni kama zatokana na Mungu. Sasa unapokuja na urgument za kuonyesha kwamba roho ile inayofanya kazi si ya Mungu uwe na vigezo vya ki maandiko ili ku justify hoja.
Kusema kwamba watu wanaacha kupakwa mafuta hapa na kukimbilia jina, unapaswa kwanza kuelewa kwamba Mungu amegawa Karama na Huduma mbali mbali kwa watu tofauti lakini anayefanya kazi ni Roho yeye yule. Karama na huduma hizi haziipingani wala kushindana na badala yake zina complement each other. Unapaswa kutambua Mgawo huu wa Mungu wa Karama na Huduma za rohoni na utofauti wa utendaji kazi yake toka mtu hadi mtu. Na hii inawafanya watu waende kufuata wanachohitaji ambacho hakipo mahala walipo. Bado hapo si kumfuata mtu. Wanafuata Karama za Mungu kwa namna alivyozigawa na zinavyofanya kazi katika kanisa.
a Usidhani ni suala la kupaka mafuta tu na wala si kama quinine kwa Malaria. Kuhusu kuwa na vipimo vya Dr, ni kwa sababu hata wakati wa Yesu watu wagumu na wabishi walikuwepo. Ndiyo maana hata Yesu kuna wakati wakoma walipopona aliwaambia waende kujionyesha kwa mafarisayo;
Kwa mtindo huo huo, watu wengi hata wakiambiwa huyu mtu alikuwa na maradhi yaloshindikana kama Cancer, Fibroid ama ukimwi kapona kwa Jina la Yesu hawasadiki. Watumishi wengi wanataka upimwe kabla hujaombewa na baada ya kuombewa ukapimwe tena ili dunia ya wabishi ione kwa macho Yesu anavyoponya.! Japo hata wengine wakiona bado hawasadiki.
Lakini kama Mtu yeyote mwingine hapa Tanzania ambaye Mungu aunamtumia kukutana na mahitaji ya watu walioonewa na ilibilisi, na aseme wazi. Na wewe kama unao ushuhuda juu ya Mtumishi mwingine wa jinsi ile, hata kama anatumia mafuta ya korie, naomba utangaze hapa ili watu wapunguze msongamano wa kusurbiri Nigeria pamoja na gharama za fedha na muda.
Na kama una unaushuhuda kwamb TB Joshua hatumiwi na Mungu useme lakini si kwa kujifurahisha. Kama huna nyamaza na uendelee kujifunza na kuomba Mungu usije ukajikuta umemkosea Mungu bila kujua.