Connect Dot: Nani anataka kumtisha Rais Samia na umaarufu wa Hayati Magufuli?

Fortilo

JF-Expert Member
Apr 10, 2012
4,722
14,248
Nchi yetu haiishiwi mambo na mengi ni yakutengeneza, jaribu kukonnect dots kwa mambo yafuatayo;

1. Ni Wiki ya pili sasa lakini hakuna chombo cha habari chochote kinachotaka tumjue vizur Rais Samia, na si kwa bahati mbaya, baada tu ya kuapa malori ya kujaza watu kwenda msibani yaliongezeka na coverage zikaongezeka sana, yani hadi waombolezaji waliozimia huku mikono ikiwa imeshikilia viroba vya vitoweo.

2. Kwamba msiba unafuatiliwa na watu karibu bilioni 4, sio kauli ya bahati mbaya, message ni kwamba huyu mtu ni mashuhuri sana na italazimika uenzi metendo yake(Offcorse nawateule wake) la sivyo wananchi wanyonge na dunia haitakuelewa.

3. Nyani wanafurahi kufa kwa Bwana shamba bila kujua kesho watakula wapi; hoja hapa wala sio wapinzani, ni kundi lisilofaidika na cheo kipindi Mzee akiwa hai, ndio limepigwa dongo, kwamba hata kama mnafurahi lakini hata hicho kidogo mlikipata kwa ubavu wake.

4. Waraka mrefu wa mema ya JK(Unaozunguka mitandaoni), unaonesha kwamba tunataka kuanza upya, kujenga nchi kwa usawa, ila pia unajibu vitisho vya team iliyokuwa inasifia mambo bila takwimu lakini pia kujibu mapigo kwamba nani atasaidia kujenga miradi mingine

5. Mimi ni Rais lakini mwenye maumbile ya mwanamke, ni kujibu vitisho kwa ujumla wake, lakini pia kuonesha kwamba akiamua anaweza kufanya hata kuzidi mtangulizi wake.

Turudi kwenye makundi ya CCM;

Kundi lililofaidi lakini lenye wasiwasi
Wamo kina Kabudi, Pole pole, Bashiru, Majaliwa na team tano tena 2020; hasa walioshinda bila kupingwa na kura za kwenye mabegi kama kule Kawe... hali yao ni ngumu kuliko maelezo.
Pia wamo waliomnanga JK vibaya mno akiwemo Madelu.

Kundi la waliotengwa licha ya uwezo wao na utendaji wao;
Wamo kina Muhongo, Januar, Nape na Kina Kimei.

Kundi la kuunga Juhudi mkono ;

Kina Covid 19, Katambi, Waitara , Silinde, Mollel na wengine, hawa hawajui nini mustakabali mama akitulia kwenye madaraka hivyo dawa ni kujiunga na kundi la kina Majaliwa.

Swali la msingi hapa; nani anataka kumtisha Rais Samia, au wanatumia umaarufu wa Hayati kutaka kumtisha asifanye lolote mambo yaende business as usual?
 
Akishazikwa Tu end of story...

Alikuwepo Nyerere hapa akiitwa Mlima Kilimanjaro na wengine vichuguu
Lakini alisahaulika haraka Sana ..

Bottom line .. waliokuwa wanamheshimu Samia toka zamani ndio watakaofaidika
Na waliompigania

Wengine wasubiri mkeka walio bet
 
Wajinga sisi tunajiingiza kwenye makundi na ushabiki tusiojua nyuma ya pazia wanapanga nini kwaajili ya Taifa hili. Kuna Cartels now zinapigana kushika mpini .... miongoni mwao ni wazalendo ambao ukitoa uzalendo wao lakini pia wanajilinda na Cartels ambazo waliziumiza kipindi wakipoka wezi mali zilizoibiwa.

Tuombee vyombo vyetu vya ulinzi na usalama wazalendo waliomo wapitishe salama Taifa kwenye hili, not by compromising ila ustawi wa Tanzania.
 
Watu wana wivu wa kijinga sana wapi umeona mtu kabebwa kwenda msibani? acheni story zenu za vijiweni kila mtu kujifanya mchambuzi wa maswala ya kisiasa mmeaminisha wabeberu kuwa huyu mtu hapendwi now mnaanza kuleta majungu yenu Samia akiwasikiliza na akashindwa kufanya majukumu yake chama chake ndo kitawajibika 2025 na ndo itakuwa furaha yenu kwani Lissu si ndo anakuwa Rais
 
Hizo ni fikra na ni maoni yako, Tanzania kuna uhuru mkubwa sana wa kujieleza na ni haki ya kila mtanzania kutoa maoni! Hongera kwa kuitumia haki yako ipasavyo.
🤔
 
Wajinga sisi tunajiingiza kwenye makundi na ushabiki tusiojua nyuma ya pazia wanapanga nini kwaajili ya Taifa hili. Kuna Cartels now zinapigana kushika mpini .... miongoni mwao ni wazalendo ambao ukitoa uzalendo wao lakini pia wanajilinda na Cartels ambazo waliziumiza kipindi wakipoka wezi mali zilizoibiwa.

Tuombee vyombo vyetu vya ulinzi na usalama wazalendo waliomo wapitishe salama Taifa kwenye hili, not by compromising ila ustawi wa Tanzania.
Hapa naona kuna mawili kwenye hizo cartels zinazopigana kushika mpini.

Kuna vita ya ndani ya makundi ya CCM, na vita nje ya CCM lakini inayohusisha makundi ya wana CCM ambayo yanaweza kupata uungwaji mkono wa vyombo vya usalama.

Jambo moja nalodhani litakuwa gumu ni hivi, inawezekana vipi kundi linaloungwa mkono na vyombo vya usalama kushinda mahala ambapo nguvu ya uungwaji mkono wa mtu husika haipo ndani ya chama?

Nionavyo, regardless ya uungwaji mkono wa vyombo vya usalama kama tunavyoaminishwa (sijui kama ni kweli), binafsi bado naiona nguvu ya kura ndani ya cham mwisho wa siku ndio itaamua mshindi.

Unless otherwise, huyu nae aingie na majina yake mfukoni, ila sio kutegemea nguvu ya vyombo vya usalama kwasababu haitahusika kwenye vikao vya maamuzi ya chama ( wajumbe kuhongwa, ukabila, etc).

Kuvitegemea vyombo vya ulinzi na usalama kwenye mambo yanayohusu maamuzi ndani ya chama kwangu naona ni sawa na kupotea njia.
 
Kaa kimya huna lolote, ramli zako na poorly thoughtful dots. Nawe unajiita bonge LA mchambuzi. Tulia nchi iko salama, mtaanza tena kulialia na kumbka jpm, ngoja mama akaze maradufu
 
nguvu ya kura ndani ya cham mwisho wa siku ndio itaamua mshindi.

Kura hizo za ndani zimenunuliwa tayari na kundi la mafisadi ambapo kura moja ya mjumbe wa sisi iliuzwa kwa shs. 20,000,000!!!
 
Back
Top Bottom