Confusion ya Marafiki, Please help!

nakubaliana nawe kabisa kuhusu urafiki na undugu.... hapo nilitoa tu mfano.
Rafiki hata wale ambao unafahamu wana tabia njema haimaanishi mnafanana kabisa tabia zenu, kuna vitu ambavyo hamfanani kabisa, lakini hiyo haimaanishi urafiki wenu utakufa sababu kuna baadhi ya vitu hamlingani......
hali kadhalika kama rafiki yako ni mwizi au changudoa. huweji jua urafiki wenu ulianzia wapi. labda wakati mnaanza hakuwa changudoa ila katikati ya safari basi inaibuka hiyo tabia ya uchangudoa.....
concern yangu hapa ni je uue urafiki na huyo mtu sababu sasa kawa changu? hata kama hakupeleki kweny hiyo biashara yao na wala hamuongei kuhusu hiyo biashara yake?
kuna siku (hii ilinisikitisha kidogo) kuna dada kamwambia best friend wake kuwa hawezi kuendelea na urafiki wao sababu tu yeye kaolewa na huyo shosti hajaolewa kwa hiyo akiendelea kuwa naye basi watu watafikiri na yeye ni muhuni tu (nadhani hapa alikuwa anamlenga mumewe).....
nilijiuliza maswali mengi na sikupata jibu. labda utanisaidia mtu kama huyu utamchukuliaje?
 
FP nadhani waliosema tuchague marafiki walikuwa na maana yao nzuri
Ngoja nifanye kazi ya mkoloni nitakuja kusema why nasema hivi
 
Last edited by a moderator:

mie sitaweza kuwa na rafiki ambae ninaona/hisi hatuendani, kila mtu ana mapungufu yake but atleast yawe ya kawaida, sitaweza kuwa na rafiki ambae siwezi kumrekebisha/badilisha tabia kama naona hazipendezi, nadhani urafiki ni kusaidiana/kujaliana kwa namna moja au nyingine, kuliko niwe na mtu ninaeona tunapishana sna kitabia ni bora nim delete pole pole tu.
 

Hapo kwenye RED ndivyo ninavyooishi....... Ukiishi kwa kutegemea maneno ya jamii utapasuka kichwa!!!
 
hapa mimi nasemea rafiki ambaye mambo mengi tu mnaendana....
she/he is always there unapomuhitaji......
pamoja na litabia lake "libaya" hakulazimishi wewe kufanya hicho anachofanya yeye...
na muda wote unapohitaji ushauri unapata the best ushauri toka kwake.
Utaachana naye tu sababu ana hiyo tabia ambayo wewe haikuhusu?
 

Mpendwa sana FP,
Kwanza naomba nikueleze kwamba hakuna sababu yoyote inayoweza kuhalalisha uovu kama uchangudoa au ujambazi.Uovu kama huu haukubaliki bila kujali hali za maisha yetu. Kwa hiyo, rafiki akibadilika njiani, ujue huyo ni dhaifu kwa maana hiyo wewe kama mtu wa karibu unatakiwa kumshauri kuachana na uovu huo na wala siyo kuuendeleza uovu wake. Kama ni rafiki yako kweli na anakuheshimu, ataacha na kuuendeleza urafiki wenu.
Pili, kuhusu best kuolewa. Inategemea na mazingira ya urafiki wao ulivokuwa. Yawezekana ulikuwa urafiki wa kiujana sana kama kwenda kutumia aka kuspend na kutafuata wanaume kwa ajili ya kuwa waume zao. Ukweli ni kwamba, mwanamke anapoolewa anakuwa amaebadilisha mazingira sana. Kwa hiyo, hawezi kuishi kama alivyokuwa akiishi zamani. Na mwanamke mwenye marafiki wengi mara nyingi inaweza kupelekea ugomvi kwa sababu hamuelewani katika maisha. Yawezekana yeye bado anatafuta na mwezie keshapata au mume wa rafiki yake alishanote kitu fulani kwa rafiki yake huyo. Si unajua tena wanaume tunadarubini za mbali sana. Pia yawezekana rafikiye ameonyesha nia ya kumtaka mumewe na mume anamtahadharisha mkewe kukaa mbali naye. Sasa asiposikia, ni yeye sasa kwani anaweza kutaifishwa mume. Mimi binafsi huwa namwambia wife kuwa makini na rafiki zake ambao nao mapepe kwani yawezekana asione yeye kwa sababu ya kimvuli cha urafiki.

Mwisho, daima usipuuze watu wa karibu au majirani wakikwambia kwamba kaa mbali namtu fulani kwani yawezekana wao wanaona zaidi yao, Na sauti ya wengi ni ya sauti ya Mungu.
 
Ogopa sana mume anayekuchagulia uwe na nani na usiwe na nani......
unaweza kubaki lonely..... na hapo ndo utaona rangi zote za dunia hii.... mark my words
 


Naamini hivyo pia. Nilipokuwa O Level, marafiki zangu wa karibu sana walikuwa ni wavuta bangi.

Walikuwa wanavuta bangi mbele yangu. Wapo baadhi pia walikuwa ni walevi pia, nk.

Lakini kwa muda wa miaka yote minne sikuvuta bangi wala kuwa mlevi.

Huwa naamini kuwa rafiki ni rafiki regardless ya tabia yake.

Binadamu hatuko sawa. Pia no body is perfect.

But kuna tabia ambazo zinaweza kukufanya umtenge rafiki yako au kuachana nae kabisa.

Kwa hiyo inategemea na aina ya tabia. Pia neno "tabia mbaya" ni relative.

Unaweza kuona tendo fulani kama ni tabia mbaya lakini mwingine akaona siyo tabia mbaya.
 
Ogopa sana mume anayekuchagulia uwe na nani na usiwe na nani......
unaweza kubaki lonely..... na hapo ndo utaona rangi zote za dunia hii.... mark my words

FP hakuna mtu anachanguliwa rafiki, ila anatahadharishwa tu kwa kuelezwa uzuri na ubaya wa kuwa na rafiki huyo. Urafiki hasa kwa wanawake mara nyingi huwapofusha sana. Wazazi, dungu na mume/mke anayekupenda atakushauri kwa wema tu. Kwa nini nikukataze kuwa na rafiki tena wa jinsi yako? Unafikiri ni wivu? Hapana. Unaweza kuangalia sababu zinazotolewa na ukiziona hazina uzito unaendelea tu. Lakini mume, wazazi na dungu wengi watakushauri kwa lengo la kukutakia mema tu na vizuri kuwasikiliza na ikiwezekana uchue hatua. Lakini uamuzi kwa kuwa na rafiki huyo physically au mentally upo mikononi mwako. Na matokeo yake utayaona mwenyewe wakati wasahuri wako wengi watajiita kuwa ni watabiri wazuri sana.
 
This question is what separates a Buddha from a Bodhisattva in Buddhist philosophy.

A possibly boggling shining compassion vs. The cold detachment bent on self advancement.

Kwenye ukristo, Yesu angekataa kuwa rafiki wa Mary Magdalene na watoza ushuru naye angekuwa farisayo tu.Asinge inspire dini inayojali upendo (sheria mpya) kuliko sheria nyingine.

On the other hand usijitie majaribuni na kukithiri katika nyendo za wezi na wahalifu kwa kisingizio cha compassion. Not everyone can pull a Jesus like tightrope walk.

Mwisho wa yote ni wewe tu unayejijua limits zako, na hata wewe mwenyewe nyingine huzijui, kwa hiyo usimuachie mwingine akupe imla wala amri kuhusu nani anafaa kuwa rafiki.

Ving'aavyo vyote si dhahabu, don't judge a book by it's cover. Some people have more layers than an onion, more personalities than the layers of a Russian doll.

Simpletons would only see the outer layer and not be able to gain the wisdom of a Shakespearean fool.
 

inategemea, nina rafiki kama ulivyoelezea, namtegemea sana sana, mshauri etc, enzi hizo tupo uraiani(hatujaolewa) yeye alikuwa na tabia ambayo sikuipenda kabisa,alikuwa hawezi kuwa na mwanaume mmoja, leo atanitambulisha kwa asprin kesho DC, kesho kutwa Bujibuji,ikafika wakati nikampiga stop kunialika kwenye mitoko yake,mana nilihisi ntafahamishwa mji mzima sasa,tulikuwa tunaongea sana juu ya hilo, namuuliza ni nini hasa kinachomfanya ahangaike hivyo? alinijibu "sio nahangaika bado sijapata ninachokitaka" baadhi ya marafiki zetu wengine walikuwa wananisisitiza sana kuachana nae coz "ataniharibu" sikuweza mana kati ya wote yeye ndio my best friend kutoka rohoni, alipata alichokuwa anataka sasa hivi ni bonge la mama wa ukweli na anaeijenga familia yake mbaya kabisa,huyu niliendelea nae coz tulikubaliana kwenye hizo purukushani zake asinialike kabisa kabisa, nilikuja kualikwa kwenye uchumba, soo inategemea sana tunaendanaje.
 

Yesu hakuwa rafiki watenda dhambi kwa muda mrefu zaidi ya kuwakaribisha ili wabadirike.
 
Naam dada yangu FP umeuliza swali zuri sana na ntalijibu kama ifuatavyo kulingana na mtazamo wangu. Katika maisha mimi huwa naamini kuwa everything happens for a reason na kila binadamu amepewa hekima ya kutambua jema na baya lakini tatizo linakuja katika kuchagua jambo lifaalo kati ya jema na baya na hapo ndipo watu wengi tunapo angukia pua kwani wengi hufanya makosa kwa kufanya uchaguzi usio sahihi na at the end huishia kutoa lawama na visingizio vya ajabu ajabu.

Kuambatana na marafiki wenye tabia mbaya hakuwezi kukusababishia na wewe uige tabia mbaya kwa sababu wewe ndio maamuzi ya kuchagua kuiga au kutokuiga tabia hiyo mbaya hata kama ukishurutishwa kwa kuwekewa mtutu usoni. Hizo sababu nyingine tunazozitoa eti flani alinishawishi au eti...flani ndio alinifanya nikaiga hivi ni visingizio tu kwa sababu hakuna aliyenyimwa hekima ya kutambua jema na baya.

Nadhani kwa maelezo yangu hapo juu nitakuwa nimejibu vyema swali lako...embu tuangalie wadau wengine tuone nao wana lipi la kusema kuhusu hili.
 
Last edited by a moderator:
hapo kwa RED inakuwa uamuzi wako, wewe mwenyewe umeamua kutengana na mtu kwa sababu unazozijua, siyo sababu watu wanaona hamuendani.
kwa mfano mimi nikiwa na rafiki ambaye muda wote nikiwa naye hatukubaliani maongezi yetu basi ni rahisi sana kupoteza mawasiliano naye
 
hii waime wengi wanafanya siyo sababu ya wivu..... huwa kuna sababu nyingi.
sababu nyingine inawezekana pia anamtaka rafiki yako kwa hiyo anaina ni vizuri kwanza akawatenganisha ili iwe rahisi kwake.... zinaweza zikawa sababu nyingine pia.
 
umeongea vizuri na asante kwa ufafanuzi mzuri.....
 
hapo sasa... kama rafiki anafanya mambo yake huko hanihusishi na mimi haina shida. shida itayokea kama atataka nifanye yale anayofanya yeye
 
Napenda kuwa na marafiki wenye tabia njema..

Na ikiwezekana niwe nina jambo naloweza kujifunza kutoka kwao.. Na wao pia kutoka kwangu.

Kama rafiki zangu wanatabia mbaya basi huenda hata mimi ni hivyo.. As wanakuwa marafiki zangu kwasababu kuna kitu tunaweza share au tuna vitu tunalandana.


Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…