Confirmed - Serikali kununua Mashangingi zaidi ya 100 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Confirmed - Serikali kununua Mashangingi zaidi ya 100

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Superman, Jan 9, 2009.

 1. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #1
  Jan 9, 2009
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  The Guardian, Friday January 9, 2009

  THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA MINISTRY OF INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT MINISTERIAL TENDER BOARD

  TENDER NO. ME/0l5/2008-2009/HQ/G/13 FOR THE SUPPLY OF MOTOR VEHICLES.

  Using Framework Contract

  Invitation for Tenders

  1. The Government of Tanzania has set aside funds for the operation of Central and Local Governments during the financial year 2008/2009. It is intended that part of the proceeds of the fund will be used to cover eligible payment under the contract for the supply of Motor Vehicles.

  2. The Ministerial Tender Board now invites sealed tenders from eligible Suppliers of the mentioned vehicles below:

  LOT
  Number Item No.Description Unit Quantity
  1 I Executive Station, 4WD Wagon PCS 35
  2 I Station Wagon, 4WD Automatic PCS 12
  3 I Station Wagon, Manual, 4WD PCS 101
  4 I Hardtop (3doors),4 WD PCS 47
  I Hardtop (5doors), 4WD PCS 20
  5 I I Pickup Double Cabin, 4WD PCS 32
  Ii Pickup Single Cabin, 4WD PCS 2
  I Motor Cycles, 125cc PCS 35
  Ii Motor Cycles, 200 cc PCS 50
  6 Iii Motor Cycle side car Ambulance PCS 20
  IV Three Wheelers Motor Cycles PCS 10
  V Motor Cycles (110 cc) PCS 15
  7 I Mini Station Wagon, 4WD PCS 30
  8 I Bus 65 Seats PCS 1

  All tenders in one original plus two copies, properly filed in, and enclosed in plain envelopes must be delivered to the address below at or before 10:00 hours local time on Tuesday, 24th February, 2009Tenders will be opened promptly thereafter in public and in the presence of Tenderers’ representatives who choose to attend in the opening at the Conference room of the Ministry of Infrastructure Development, Tancot House, 3 Floor, Pamba road of Dar es salaam and shall be marked “TENDER NO. MEIOI5/2008-209/HQIG/13 FOR SUPPLY OF MOTOR VEHICLES TO BE OPENED UNTIL Tuesday, 24t February, 2009.

  Aeeee mama weeeeee ingekuwa wewe ungefanyaje . . . Aee mama weee ingekuwa wewe ungefanyaje . . . ?

  Habari ndo hiyo . . . Mizengo Pinda upo hapo?
   
 2. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #2
  Jan 9, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Pia kuna habari kwamba kuna Magari manne aina ya Benzi yako pale Uwanja wa Ndege wa Dar, yametoka Lubya kwa ajili ya IKULU. Mwenye ziada ya habari atujuze, yamekuja na ndege na kwanini yamechelewa kutolewa pale Cargo?
   
 3. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #3
  Jan 9, 2009
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Halisi Mkuu;

  Kweli Nchi hii hakuna Kiongozi mwenye Uchungu.

  - Muungwana wakati anaingia madarakani siliamali alichakarika akmwachia Gulf na Merc Benzi Limosine Mpya, leo Muungwana kabadili anatumia BMW.

  - Sasa kama kuna Merc Benz tena Airport ni za nani?

  - Na huyu naye Mizengwe Iliyopinda katupa matumaini kuwa Serikali sasa itakuwa inanunua Matrekta na hakuna kibali cha Magari bila yeye. Hii Mishangingi Executive Cars za nini sasa? Watendaji wengi kwa sasa wana magari yao na ni mazuri tu . .

  Hivi ni nani hasa atatuokoa?

  Au tubinafsishe Uongozi wa Nchi pia? Watu wazima tunakuwa kama hatufikiri.
   
 4. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #4
  Jan 9, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Too sad !!!!!
   
 5. r

  rpg JF-Expert Member

  #5
  Jan 9, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 3,516
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Kama kampeni za ubunge Mbeya vijijini zinagharimu million 150 (hizi ni zilizotajwa na chama kimoja, yawezekana mamilioni zaidi yatatumika), billion 2 kwa mgombea mmoja tu wa UWT, na messup kibao kama hizo za kununua magari ya bei juu yasiyohitajika, bado Mnaimani kuwa kuna kiongozi ana huruma na wadanganyika tena? Hakuna hata mmoja!! Baadhi ya viongozi wanaingia madarakani wakiwa wasafi, wanapambana, wanashindwa, wanaamua kujiunga (if they cant fight, they join them) na kuwa mafisadi vilevile. Itatuchukua miongo kadhaa kuondokana na hali hii. Mind you, gari la milioni sitini, linatumiwa na mtu mmoja ama wawili tu. Je kama wangelinunua trector moja lingehudumia wakulima wangapi??
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Jan 9, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,572
  Likes Received: 82,075
  Trophy Points: 280
  Hawa wanaotumia pesa za walipa kodi kununulia magari ya kifahari yenye bei mbaya ambayo hatuyahitaji na wakati huo huo Wanafunzi chungu nzima wa shule za msingi waliopasi wamekosa nafasi ya kuendelea eti kwa kuwa hakuna madarasa, mahospitali yetu hayana madawa, vifaa muhimu na vitanda nao ni MAFISADI wa aina yake, inabidi nao tupambane nao.
   
 7. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #7
  Jan 9, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Bora walivyotoa tenda hadharani, unaonaje kama yangenunuliwa kinyamela tu? Ingeitwaje? ufisadi dabodabo ama..?

  Hapana shaka Wizara hiyo inashida kubwa na vyombo vya usafiri, ukichukulia ni wizara ya Miundombinu, sidhani kama wanapaswa kuikagua Tz yote kwa baiskeli ama ST 11
   
 8. K

  Koba JF-Expert Member

  #8
  Jan 9, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  ....juzi tuu pinda kaja na story zake kuhusu huu ufisadi lakini cha ajabu wanafanya yale yale,hawa watu hawako serious kwa chochote,nchi haina umeme,wanafunzi wamefukuzwa kwa ajiri ya sababu ya pesa,barabara ni foleni kwa kwenda mbele,bandarini kumejaa mizigo kwa sababu ya uzembe mpaka nchi nyingine wanahamishia biashara zao mombasa ingawaje ina cost zaidi lakini wanaona bora kulipa zaidi ya ile karaha ya pale Dar...shirika la ndege wamekula mpaka wameliua..etc.
   
 9. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #9
  Jan 9, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  That reflects how the "wapiga kura wasivyooogopwa wala kujaliwa!!"
   
 10. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #10
  Jan 9, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Hoja yako kuhusiana na uwazi sawa kabisa Kibunango, lakini huoni kuwa hiyo balance ingelikuwa bora zaidi kama katika hiyo tenda 'Bus 65 Seats' zingelikuwa kama 3 au nne hivi ili kufyeka ukubwa wa FWD zilizo nyingi huko juu yake? Vi-min bus vingelifaa tu zaidi kwa ajili ya kubeba wafanyakazi zaidi ya 10 at a go na kupunguza magari yanayobeba watu 4 pekee kwa mpigo..
   
 11. SaidSabke

  SaidSabke JF-Expert Member

  #11
  Jan 9, 2009
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 1,968
  Likes Received: 222
  Trophy Points: 160
  Upuuzi mtupu hivi nyie mnaopinga mnataka serikali isinunue magari mnataka wananchi tuhudumiwe vipi.Yakweli mnayosema au basi furaha yenu kutoa lawama.mbona hamjaeleza seriakali inunue magari yapi yaliyo rahisi kwa matumizi ya maafisa wa kiwango kipi.au hamjawahi kufanya kazi za kuzunguka kutoa huduma kwa watu hata ikiwa ni ya biashara katika kampuni binafsi.
   
 12. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #12
  Jan 9, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Bwana asifiwe mkuu,tatizo sio kutangazwa kwa tenda tatizo liko kwenye kinachotangaziwa tenda...serikali yetu na sisi ni maskini wa kutupwa haman haya ya ku spend mil 100 kwa gari moja la kifahari tena FWD lenye kubeba watu 6 mjini dar es salaam...
   
 13. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #13
  Jan 9, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Jumla wizara hiyo itahitaji vyombo 410


  Wazo lako ni zuri sana katika suala zima la utunzaji wa mazingira na kupunguza gharama za ununuzi pamoja na uendeshaji. Aidha sina hakika kama hizo 4WD zote zitatumika hapo DSM, kama zitatumika hapo basi hapana haja ya kuwa nazo katika wingi kama huo na ni bora kuwa na mabasi kama ulivyoshauri.

  Tz bara ina zaidi ya mikoa 20, na kila mkoa una Resident Engineer/Director ama cheo cha juu katika kuwakilishwa wizara hiyo, hapana shaka zitatumwa huko. Then kuna wasaidizi, kuna watu wa maabara, kuna watu wa research, kuna wahasibu...Kwa hulka ya Bongo hawa lazima watagawiwa katika mafungu na kukabidhiwa 4WD... Kuna kundi la mafundi, wakaguzi n.k hawa wote wanahitaji usafari... naona kuna pikipiki pale, hapana shaka ni kwa kundi hili.

  Katika yote ununuzi wa Motor Cycle side car Ambulance bado sijahufahamu vizuri wanakusudia kuzitumia kwa shughuli gani?
   
 14. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #14
  Jan 9, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Je ni kweli upepo wa Pemba unanukia marashi ya karafuu?
   
 15. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #15
  Jan 9, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Lazima niseme naona sasa tumechanganyikiwa, tunajadili vitu ambavyo hatuna details navyo, hatuna information za kutosha kuweza kuchallenge... yet inaonyesha sisi twajua kuliko wenzetu walioko serikali... this is simply bullshit.

  Nikilazimika kuungana kiimla na wachangiaji wengi, bado ni line ya kwanza tu ndio ambayo nawezak kuwaelewa... hizo gari zingine zote ni za kawaida sana kwa ajili ya kupeleka huduma vijijini na mawawilayani...

  Pia kumbukeni kwamba wizara ya miundo mbinu ndio inamiliki magari ya serikali kwa hiyo sio lazima magari hayo yawe ya kwao ndio maana ya line hii ambayo niko sure ni kwa ajili ya wizara ya afya.
  Ukiwa mchambuzi mzuri unastahili kujua kwamba gari zinanuliwa kwa ajili gani then ndio useme kwani nini?

  Gari zingine zinakuja ku-replace gari chakavu ambazo huenda ni expensive kuzi-maintain....

  Wenzangu na mimi hapa mnadhani kila kitu hapa ni idadi ya magari ya serikali yanaongezeka...

  Tuwe objective kidogo kwa ajili ya taifa letu.
   
 16. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #16
  Jan 9, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Naam, na hasa wakati wa mavuno ya karafuu, kisiwa chote unukia karafuu...
  BTW hii ni commercial break ama...?
   
 17. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #17
  Jan 9, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Hii ni classic Nyani Ngabu....kuteka nyara mada....lol
   
 18. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #18
  Jan 9, 2009
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Haya mambo ya kutangaza tender ni uizi kwanini wasiwasiliane na kampuni moja kwa moja????????? Ufisadi ndiyo huu
   
 19. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #19
  Jan 9, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,358
  Likes Received: 5,656
  Trophy Points: 280
  Ishieni huko mkifika kuichunguza na eeeewwuuuuraaaaaa

  mtakoma na nchi yetu!!!
   
 20. Sober

  Sober JF-Expert Member

  #20
  Jan 9, 2009
  Joined: Jun 6, 2008
  Messages: 289
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwenye hio list mi naona hio item no.1 tu ndio "mashangingi".... Hayo mengine yote ni magari ya kazi.

  Hayo mashangingi 35 ndio ya kutolewa na kuyabadili na hardtops. Nchi yetu kubwa na haina miundombinu mizuri,... kama tunataka hands on uongozi wa watumishi kufika mpaka vijijini, gharama za vitendea kazi kama 4WDs haziepukiki....kuna barabara huko hata mvua ya masaa mawili tu inatosha kuifanya iwe haipitiki bila 4WDs.
   
Loading...