CONFIRMED: Manara alikuwa anaihujumu Simba SC

msovero

JF-Expert Member
Jun 30, 2019
839
1,472
Leo kwenye kipindi cha sports HQ kinachorushwa na E-fm aliyewahi kuwa msemaji wa club ya simba 'simba sports club' Ndg. Haji Manara ameweka bayana kuwa hajawahi kuipenda club hiyo na hajawahi kuwa miongoni mwao. Kwa kinywa chake haji manara amesema "sijawahi kuwa simba"

Itakumbukwa kuwa ni wiki chache zimepita tangu msemaji huyo aaminishe mashabiki wa simba na Watanzania kuwa aliipenda club hiyo kutoka moyoni na kuwa alijitolea kwa nguvu zake zote kwa jasho na damu kuipigania kufa na kupona hadi kufikia hapo ilipofikia.

Lakini kwa kauli yake aliyoitoa leo naungana na wana soccer wengine kuamini pasina shaka kwamba huyu bwana alikuwa yupo simba kwa kazi maalum ya kuhijumu na baada ya kushitukiwa na kutimuliwa ameamua kujitangaza hadaharani kwa kinywa chake mwenyewe.

Kufuatia kauli yake hiyo, mimi kama mdau wa soccer na mkereketwa wa Dar es Salaam Young africans 'Yanga' naishauri kuwa makini na huyu mtu kwa sababu 'what goes around is what comes around'. Kama mtu huyu huyu alitumiwa na wao kututukana na kutukejeli leo amewageuka wale wale waliomtuma na kumlipa kututukana basi ipo siku hata sisi atarudi tena kutugeuka na kututukana vile vile na hapo ndipo msemo wa "what goes around is what comes around" unapodhihirika. Tuwe makini na huyu walking bomb he can erupt anytime.
 
Aisee huyu jamaa anapitia wakati mgumu sanaa
Yote haya aliyataka yeye badala ya kuwa msemaji akageuka kuwa afisa mipasho wa simba akaanza kutukejeli wana yanga na club yetu mara atuite 'utopolo' sasa baada ya kurejea nyumbani kwa mabingwa wa kihistoria naona anatumia nguvu kubwa sana kujisafisha kwa makosa aliyotutendea wananchi kwa kuropoka kila linalomjia kichwani ambapo kwangu naona ndio anazidi kujiharibia zaidi.
 
Wa kulaumiwa sio Manara bali waliomleta Simba na kumpa uongozi. Sifa ya mwanachama wa simba ni kuwa mwaminifu lakini Manara hakuwa na sifa hizo na bado wakambeba matokeo yake akawa anaenda kutoa siri za Simba kwa wapinzani ila usaliti huwa haumwachi mtu salama.

Pia viongozi wajifunze waache kuwatafuta kina Mwijaku, Salama au Dr. Kumbuka kwani wote hao wapo kimaslahi zaidi.
 
Back
Top Bottom