Computer yangu imezima ghafla

Computer yangu imezima ghafla

kyesha

Member
Joined
Feb 17, 2019
Posts
40
Reaction score
66
Habari za Midaa Wadau!!

Mtaalamu wa computer anisaidie, nimepata changamoto.

Daaah, laptop yangu inagoma kuwaka

Adapter Iko gudi tu, ni Dell
 
Habari za Midaa Wadau!!!
Mtaalamu wa computer anisaidie, nimepata changamoto .
Daaah, laptop yangu inagoma kuwaka

Adapter Iko gudi tu, ni Dell
Inamda gani tangia ununue na unatabia ya kuazimisha
 
Habari za Midaa Wadau!!

Mtaalamu wa computer anisaidie, nimepata changamoto.

Daaah, laptop yangu inagoma kuwaka

Adapter Iko gudi tu, ni Dell
Embu Nijib kwanza aya maswali kisha tupate ufumbuzi;
Umejuaje kama Adapter ipo sawa?
Na imegoma kuwaka ukibonyeza power button inafanyaje?
Umetoa battery na kuwasha kwa kutumia adapter?
Je Pc yako inatabia ya kupata moto sana wakati wa kuitumia?
 
Wakuu msaada tutani desktop yangu inasumbua. Mouse haifanyi kazi wala keyboard haibonyezeki. Please assist.
1000346330.jpg
 
Wakuu msaada tutani desktop yangu inasumbua. Mouse haifanyi kazi wala keyboard haibonyezeki. Please assist.
View attachment 3607564
Naomba kujibu maswali haya ili iwe rahisi kugundua chanzo cha tatizo:
Je, desktop inawaka kawaida na picha inaonekana kwenye monitor?
Mouse na keyboard ni za USB au PS/2?
Ukiunganisha mouse au keyboard, taa zake zinawaka?
Umejaribu kuzichomeka kwenye USB port nyingine?
Tatizo lilianza baada ya kufanya nini (mfano kufunga programu, kufanya update, au kuzima umeme)?
Ukiwasha upya (restart), bado mouse na keyboard hazifanyi kazi?
 
Mkuu nashukuru kwa ushauri; baada ya kubadilisha keyboard sasa mashine inapiga kazi vizuri.
 
Hivi ni kweli HDD ikifa hakuna namna ya kupata data zako kwenye hyo HDD?

Na kama ndyo sasa mzungu alishindwa nini kuipa computer kimemory cha backup ikitokea issue kama hzo..!!
 
Hivi ni kweli HDD ikifa hakuna namna ya kupata data zako kwenye hyo HDD?

Na kama ndyo sasa mzungu alishindwa nini kuipa computer kimemory cha backup ikitokea issue kama hzo..!!
Jibu ni kwamba hapana, si kweli kwamba wahandisi walishindwa kutengeneza backup ndani ya kompyuta. Sababu ni kwamba backup ya kweli haiwezi kuwa kwenye kifaa kilekile kinachoweza kuharibika.
Fikiria mfano huu:
Ukiweka nakala ya funguo zako ndani ya nyumba, nyumba ikiteketea kwa moto, funguo zote mbili zitapotea.
Vivyo hivyo, ukiweka backup ndani ya HDD hiyo hiyo, HDD ikiharibika, backup nayo itaharibika.
Ndiyo maana wataalamu wa IT hufuata kanuni ya 3-2-1 Backup:
Nakala 3 za data zako.
Zihifadhi kwenye vifaa 2 tofauti (mfano HDD ya ndani na external HDD).
Nakala 1 iwe sehemu nyingine, kama kwenye cloud (mfano Google Drive, Microsoft OneDrive, au Dropbox).
Pia, kompyuta nyingi za kisasa zina teknolojia zinazosaidia kulinda data, kama:
RAID (hasa kwenye server na baadhi ya PC) ambapo data huandikwa kwenye diski zaidi ya moja.
Cloud backup zinazofanya nakala kiotomatiki.
Programu za backup zinazohifadhi data kwenye external drive.
Kwa hiyo, si kwamba "mzungu alishindwa". Badala yake, kwa sababu hakuna kifaa kinachodumu milele, suluhisho salama ni kuwa na backup nje ya kifaa hicho. Hiyo ndiyo njia inayotumiwa duniani kote.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom