Comoro inafikikaje kutokea Tanzania?

WatesiWETU

Senior Member
Jan 2, 2022
106
245
Habarini wana jamii..

Nilikuwa nataka kutembelea Comoro ili nijifunze mahitaji yakule nifaye itafiti kama naweza kuwa na supply biashara kule kisiwani kwao kutokea huku Dar es Salaam.

Sasa najiuliza maswali kadhaa..

1. Usafiri wakwenda kule unapatikana wapi?
2. Nauli inakuwa bei gani?
3. Je, kuna wabongo wanao fanya biashara kule na huku?
4. Kuna vikwazo vyovyote maana sijawahi kusikia Wafanyabiashara wakizungumzia Comoro.

Naomba mwenye connections na Wacomoro wanaofanya biashara na Tz anisaidie mawasiliano yao nijadiliane nao namna ya kufanya nao biashara kwa kuzingatia mahitaji yao kule visiwani.

Asanteni
 
Fika pale zenj yakhee utapata usafiri.
Wacomorro ni watu wa karimu sana Sheikh
Kaka kwa huku bara hakuna boat au usafiri wa majini wa komoro ni mpaka nilipie kweda zanzibar kisha nikalipie kwenda Comoro tena??

Embu nidafanulie vizuri aisee maana I na maana nikiwa na mzigo nitaulipia forodha zanzibar na uko comoro tena na bado hapa dar bandarini nikague wanipige tena hela je hiyo biasharas itakuwa na faida gani basi..?? dah ..
 
Kwa mizigo kuna meli za mizigo kwenda Comoro zinaanzia Dar
 
Nenda pale bandarini kwenye ofisi za Azam utapata maelekezo kuhusu boti.

Ila pia unaweza kukwea pipa nadhani Air Tanzania inafika kule na hizi ndege ndogo ndogo Kama Zan Air, Assalam Air etc. Nenda pale pale bandarini kuna ofisi pia za kufanya booking za ndege.
 
Kama hujui jinsi ya kufika Comoro na unataka kwenda , USIENDE. utapotea, Ulizia vizuri stendi mpya ya MAGUFULI **** mabasi yanaenda huko
 
Unaweza kwenda na meli ya mizigo nauli kama laki hivi,lakini utafika umechoka,kama mfuko unaruhusu panda ndege ,ni jumamosi ,jumatano na jumatatu,nauli go and return kama laki saba mpaka milioni moja,inategemea ,nitumie namba yako pm nikuunge nao
 
Kwenye meli inachukua siku ngapi
 
Usafiri salama ni kwa ndege tuu, Air Tanzania wanayo route ya huko nenda travelling agent iliyo karibu nawe utapata maelezo zaidi.
Pili, fika maeneo ya Madina restaurant mtaa wa Kongo, maeneo yale ndio wa-Comorro wanafikia na kula, utawapata wengi watakupa picha halisi, na wanazungumza kiswahili.
Tatu, tembelea ubalozi wa Comorrow Tanzania watakusaidia kupata majibu au maswali yako yote.
Ukifanikiwa kupata picha halisi uje utupe mrejesho.
 
Huwa inategemea na hali ya hewa na hali meli,kama mawimbia sio makali,na meli ni imara,siku mbili mpaka tatu
Daah usafr wa majini full stress Sana , hasa mkifika sehemu ambayo kila upande ni maji alaf Hali ya hewa ikazingua
 
Usafiri salama ni kwa ndege tuu, Air Tanzania wanayo route ya huko nenda travelling agent iliyo karibu nawe utapata maelezo zaidi.
Pili, fika maeneo ya Madina restaurant mtaa wa Kongo, maeneo yale ndio wa-Comorro wanafikia na kula, utawapata wengi watakupa picha halisi, na wanazungumza kiswahili.
Tatu, tembelea ubalozi wa Comorrow Tanzania watakusaidia kupata majibu au maswali yako yote.
Ukifanikiwa kupata picha halisi uje utupe mrejesho.
Wazo zuri la kutembelea ubalozi wa comoro Tanzania, mm nilipata rafiki m comoro lkn alichonitahadhalisha kuhusu biashara akaniambia aidha nijipange niende nikafanye survey au nitafute connections na ubalozi wa Tanzania nchini Comoros. Pia aliniambia mazao ya chakula yanalipa sana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom