Common Market: Watanzania tuamke tuache woga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Common Market: Watanzania tuamke tuache woga

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Ogonga, Apr 28, 2010.

 1. O

  Ogonga Member

  #1
  Apr 28, 2010
  Joined: Apr 26, 2010
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ogonga has come with Common Market Protocals. Watanzania tusihofu ila tuchukue tahadhari kama ifuatavyo.

  Tuutumie uwezo tulio nao kielimu kwa nguvu zote tuhakikishe kuwa tunapata mafanikio kupitia Common Market. Napenda kuwatia moyo kwamba uwezo wetu ni mkubwa, mipango yetu ni safi ila tu hatujui kumarket tulicho nacho ama kwa kukosa ujuzi wa marketting au kwa kutokujua uwezo wetu au tulicho nacho au tunachojua. Hapo ndipo tunahitaji msukumo wa kila mtu kutafiti uwezo wake, au alicho nacho au anachojua na akiuze kwa nguvu zote. Pia tusikubali kuburuzwa kwa ujira mdogo au bei ndogo kwa sababu tu ya kiingereza.

  Ongea Kiswahili, Kiswanglish au hata Broken English ali mradi utetee haki yako na maslahi yako. Tanzania ni nzuri sana na raslimali ni nyingi na watu ni wengi. Tunachotakiwa ni kuwathibiti viongozi ili mambo yaende sawa. Mifano michache: Sheria ya Madini, Richmond, Sheria ya gharama za uchaguzi na mambo mengi yamethibitiwa ama na makundi ya jamii, vyombo vya habari au mtu mmoja aliyethubutu na hakuna kilichotokea. Tuache ukondoo tuamke, hatutauawa. Ila ukianza jambo hakikisha una facts za kutosha.

  Achana na UMBEA.
   
Loading...