Pichaa
Je, ni komedian (mchekeshaji) gani hapa Bongo anayeweza kulinganishwa na Eric Omondi wa kenya? Kwa mnaomfahamu naomba mnijuze nicheki ukali wake.
Bambo kabarikiwa sana.Ana kipaji cha aina mbili za vichekesho.Aina hizo ni:Bambo, the guy anajua bwana na kingwendu
Hebu nieleze vizuri warumi. Eti uliona kazi ya eric omondi aliyokopi toka kwa diamon?KUmbe yule jamaa ni mkenya? By the way siwezi kum judge coz nimeona kazi yake moja tu aliyo copy kwa diamon, so I rate him 2/10
btw Zamaulid, pichaa ni mtanzania? Katika pitapitaClip...
We nawe umeuliza halafu umeandaa majibu bila kutafakari mzee MAJUTO yupo kundi gani ????????????Kwa ujumla hapa Bongo hakuna solo stand-up comedian aliye kwenye class ya anna kansiime, eric omondi au gwiji jimmy carr. Comedian wetu hapa bongo wanafanya kwenye kundi tu - ze komedi, futuhi,pikabom nk.
btw Zamaulid, pichaa ni mtanzania? Katika pitapita
yangu mtandaoni nimenasa clip hii hapa chini ya pichaa.
CLIP YA PICHAA
Haloo samsu, mzee majuto katika uchekeshaji anatumia staili ya stori za kuchekesha na kukuhamasisha ucheke kwa kutumia uso wake! Mara nyingi hafanyi mwenyewe, anafanyia kwenye kundi.Labda kama kakodishwa na kampuni/shirikaWe nawe umeuliza halafu umeandaa majibu bila kutafakari mzee MAJUTO yupo kundi gani ????????????
Hebu nieleze mwallu.Kwa kutumia clip hapo chini, joti ni huyo mkunja midomo anayesoma tangazo au ni huyo alevaaJoti.....
Mpoki nilishamzungumzia kwenye post za mwanzomwanzo ukurasa labda wa pili au tatu hivi.Mpoki unamuonaje
Asante FYATU kwa uelewa wako mkubwa kuhusu fani ya uchekeshaji. Comedy za maana zinahitaji a concerted team work of experts -script writers, costume and trade mark designers, etc. Lakini kijana wa kitanzania aneyejua kukunja uso ukafanana na uso wa fisi halafu watu wakamshangaa na kucheka anasema na kutamba yeye ni mchekeshaji (comedian) na hataki kusikia chochote eti kuhusu kupanua ujuzi nk. Sijui kwa nini vijana wengi wa kitanzania ni so complacent (betweka).Wakiingia kwenye kikundi wakapata laki mbili tatu za kununua smartphone wanaona wameshafika na wanashindwa kabisa kufanya maonesho ya solo stand-up comedy kama afanyayo eric omondi.Changamoto iliyopo upande wa tasnia ya filamu ndio iliyopo kwenye standup comedy, pamoja na kipaji binafsi cha mchekeshaji bado anahitaji kuwa na uwezo wa KUFUNDISHIKA.
Wapo wengi wanaoweza kuchekesha kwenye vikundi vya watu mashuleni, sehemu za kazi n.k...lakini inapokuja haja ya kutaka kufanya hivyo "kikazi zaidi" unahitaji zaidi ya kipaji tu...na kama unatamani jukwaa la kimataifa zaidi basi lazima na kichwani uwe vyema, kwa kupata elimu ya darasani au la basi uwezo mkubwa wa kuelewa mambo.
Wasanii wakubwa wa kimataifa wa kuchekesha jukwaani huwa na mtu au timu nyuma yao, sidhani kama wengi wetu tunajua kuwa wanayoongea pale huandikwa kabla (hata kama sehemu kubwa au yote ni mawazo ya mchekeshaji mwenyewe), kisha hufanyika reharsal chini ya wa/mtaalamu/director/sound/lights/camera operators n.k....mchekeshaji huandaliwa jinsi ya kupangilia hoja ya mwanzo, kati na ya mwisho, jinsi ya kutumia jukwaa, kupatiwa taarifa sahihi kwa kila analotaka kuongelea pale jukwaani, na sio kwa kuwa ni mchekeshaji basi unaongea tu chochote bila kujali usahihi wake.
Hivyo utaona kipaji pekee hakitoshi, bali mtu anahitaji skills za kuelewa miongozo na kukumbuka mistari (lines) hata kama yeye ndio ameandika script, Hakuna jambo linalofanywa hovyohovyo tu haswa katika level ya kimataifa.
Hivyo tujiulize kati ya wasanii wetu wote tunaowataja wangapi tunaona wapo kwenye nafasi hiyo ? Nimeshaangalia kazi kadhaa za Eric, kwa kweli anajitahidi sana kulinganisha na wasanii wetu.