Coalitions of the willing (UKAWA)

Coalitions of the willing (UKAWA)

UKAWA una mtihani mkubwa katika kuishinda tamaa ya ruzuku na madaraka..Muungano huu unapaswa kudhihirisha ukomavu wao wa kisiasa ndani ya siku chache zijazo

Itakuwa habari ya kusikitisha pia kama hizo taarifa za uma tata zitakuwa za uongo. Maana kila kitu ni kama kitendawili.

La msingi tuwaombee mema maana kwa ujumla upinzani wameitendea nchi yetu mazuri mengi!
 
Tukiongozwa na unafiki hatuwezi kufika. Hivi CUF mwenye mgombea Urais aliyeteuliwa na Vikao vya Chama mkononi na CDM ambaye mpaka sasa hawana Mgombea Urais aliyeteuliwa na vikao vya Chama, nani yupo Tayari? Au kuna vyama vyenye hatimiliki na Ukawa na Wengine ni Waalikwa?
Tuliaminishwa kila chama kitateua mgombea ili wachujwe na UKAWA, labda mtuambie tusio na Upande CDM mgombea wao nani?
 
Kwa hili naunga mkono hoja ila vipi home boy wako edo atakuja na ntoke vipi?

subira yavuta kheri, cuf wasubiriwe ila ukawa wawe tayari to bow down to cuf demands. Niliwahi kusema mahali kuwa cuf ina wagombea wa kudumu kwenye urais. Prof. Lipumba na maalim seif wamegombea mara 4 hii ni ya 5!. Angalau maalim akijaribu tena ana posibility ila lipumba kura zake zimekuwa zikipungua mwaka hadi mwaka na kwa vile hakuwahi kugombea ubunge, kwake kugombea urais ndio full lifetime profession yake akikubali mwingine yeyote kugombea, he will be rendered jobless!. Kwa lipumba kugombea urais kwake sasa imekuwa ni hobby anagombea tuu ili agombee tuu na sio kwa lengo la kupata ushindi!. Yuko tayari ku risk kulazimisha mgombea wa ukawa lazima awe yeye and it doesn't matter kama anagombea kushinda au kushindwa kwa sababu lengo ni kugombea tuu na sio kushinda after all ameisha zoea kushindwa hivyo hata akishindwa kwake ni sawa tuu!.

Msubirieni tena yeye atajinyamazia kimya na kujifanya ni wanacuf ndio walioamua lazima ama awe yeye mgombea wa ukawa ama cuf watajiondoa ndani ya ukawa.
Pasco
 
bulunga Acha propaganda za ajabu, wote mbatia tumemsikia wewe unayoyasema umetunga mwenyewe

Nimetunga nn hapo, unataka kupotosha na ku divert ukweli,
Ukweli upo na kumbukumbu zipo stop diversion!
 
suala hapo ni ruzuku, chama kitakufa bila ruzuku. pili viti maalumu vya ubunge. ndo maana hayo yote lazima yawekwe sawa. kumbukeni chama kitakachoweka mgombea wa urais ndo chenye haki ya vyote hivyo.
isitoshe chadema walishawaambia CUF ni ccm B na nccr ni ccm C. kwa hiyo sioni cha ajabu. na CUF wawe makini sana kushirikiana na hao jamaa. hawatabiriki. cuf wakiwa chama kikuu cha upinzani waliwashirikisha chadema. lakini kwa chadema walipokuwa chama kikuu cha upinzani waliwakataa.

Ningependa kujua mwaka 2000 (kama sikosei) wakati Chadema walipoungana na CUF na kumsimamisha mgombea urais mmoja (Prof. Lipumba) ili swala la ruzuku na viti maalum lilitatuliwaje? Kama mwaka 2000 walipata mhafaka kuhusu ruzuku na viti maalumu kinachoshindikana kwa wakati huu ni nini?

Kwa maoni yangu muungano huu watakaofaidika ni CUF, Nccr na NLD kuliko Chadema maana CUF wana wabunge wawili (kama sikosei) wakuchaguliwa huku bara, na kwa hali ilivyo uwezekano wa Cuf kupata wabunge zaidi bila Ukawa ni mdogo..
Hivyo hivyo kwa NCCR wabunge ni watatu wa kuchanguliwa na hata hivyo mmoja keisha jiengua kwenda ACT na bila shaka hata hawa wawili waliobaki uwezekano wa kwenda ACT ni mkubwa kuliko kubaki NCCR, hivyo basi utaona hata kwa NCCR uwezekano wa kupata wabunge zaidi ya 3 haupo ila kwa kupitia Ukawa NCCR wanaweze kutapa walau wabunge 5 mpk 10 (ukijumlisha na wabunge wa NCCR walipo sasa)

NLD nayo stori ni ile ile..

Tukirudi kwa Chadema uwezekano wa kupata wabunge zaidi iwe ndani ya Ukawa au nje ya Ukawa ni mkubwa maana Chadema wamejijenga tangu mwaka 2010, viongozi wao wanaotarajia kugombea katika majimbo mbali mbali wameweka mzizi yao tangu mwaka 2010 tofauti na vyama vingine.

Hivyo basi ni muhimu kwa vyama vinavyounda Ukawa kuangalia kwa mapana faida zinazopatika wakiwa pamoja.. kuliko kuangalia faida wanazopata viongozi wa hivyo vyama.

Ukawa wekeni maslahi ya Watanzania mbele, watanzania wako tayari kwa mabadiliko..
 
Subira yavuta kheri, CUF wasubiriwe ila UKAWA wawe tayari to bow down to CUF demands. Niliwahi kusema mahali kuwa CUF ina wagombea wa kudumu kwenye urais. Prof. Lipumba na Maalim Seif wamegombea mara 4 hii ni ya 5!. Angalau Maalim akijaribu tena ana posibility ila Lipumba kura zake zimekuwa zikipungua mwaka hadi mwaka na kwa vile hakuwahi kugombea ubunge, kwake kugombea urais ndio full lifetime profession yake akikubali mwingine yeyote kugombea, he will be rendered jobless!. Kwa Lipumba kugombea urais kwake sasa imekuwa ni hobby anagombea tuu ili agombee tuu na sio kwa lengo la kupata ushindi!. Yuko tayari ku risk kulazimisha mgombea wa UKAWA lazima awe yeye and it doesn't matter kama anagombea kushinda au kushindwa kwa sababu lengo ni kugombea tuu na sio kushinda after all ameisha zoea kushindwa hivyo hata akishindwa kwake ni sawa tuu!.

Msubirieni tena yeye atajinyamazia kimya na kujifanya ni WanaCUF ndio walioamua lazima ama awe yeye mgombea wa UKAWA ama CUF watajiondoa ndani ya UKAWA.
Pasco

Kwa hili chadema hawawezi ku-bow down kwa c.u.f. eti wanao mtaji wa kudumu Zenj. usilolielewa ni kua hata huo mtaji wao wa Zenj hawawezi kumpigia kura mkristo eti kwa kuwa wamenyenyekewa haitatokea wao watampigia Seiff wao kura za bara ni za maruhani tu zitakazohesabiwa. Kwa kikao kama kile cha tarehe 14/7 cha ukawa kumtangaza mgombea wao sio Lipumba wala Seiff walihudhuria bali alitumwa mwakilishi asie na mamlaka. Wenyeviti na makatibu wa vyama vingine wote walikuwepo. Baadae tukaambiwa na makamu wake bara kuwa m/kiti wao ilibidi asubiri kwanza maelekezo ya vikao vyao vya ndani. Aliepanga tarehe ya kikao cha kumtangaza mgombea uraisi wa ukawa ni Lipumba huku akielewa lazima vikao vya kumruhusu vingefanyika kabla ya siku ya kikao cha ukawa.Eti tuwasubiri hadi tarehe 25 ndio watoe jibu. Nasema hili halikubaliki wala kuendelea kuvumiliwa.Kwanza toka mwanzoni kabisa wanaungana nilidhani ni pale bungeni tu kutuletea katiba nzuri. Ilipofikia hatua ya kushirikiana uchaguzi mkuu eti kwa kumteua kwa pamoja mgombea uraisi toka chama kimojawapo ndani ya ukawa,kuachiana hata majimbo nikatahadharisha tena maana nilishaona huu muungano utavunjika hata kabla ya uchaguzi kwani niliyaona mapandikizi. Hata Wassira aliliona hilo. Kwanza mitaji yao ya kura kwa wananchi hailingani. Wabunge hivyo hivyo mmoja ana wawili/watatu na hata wa pili idadi ni hiyo hiyo mwingine anao 48 na mwingine hana kabisa. Ile intelijensia ya chadema ililogwa? Hivi walisahau uchaguzi uliopita 2010 Lipumba akiwa anagombea uraisi kwa tiketi ya chama chake aliacha kukipigia debe chama chake na kumsaidia Kikwete kupitia waislamu. Hili alikiri mwenyewe tena kwa mashekh msikiti mmoja Dar.eti aliona hali ni mbaya kwa Kikwete. Ajabu kwenye mikutano yake yeye ndio anadundwa zaidi.Aliwaomba lini radhi watz na wanachama wake kwa usaliti huo? Akiwa ukawa aliwahi kumwalika Zitto kuhutubia mkutano wa c.u.f.huko kusini. Hilo lilitoa ujumbe gani kwa chadema?Ni kweli tulimsikia Mbatia akiwapa chadema tahadhari kuwa wasijifanye wao ndio ukawa. Hili halikuwa vyema kwani angeweza kuyasema ndani ya vikao vyao vya ukawa. Tulimsikia hiyo tarehe 14 akitoa tamko kwa niaba ya ukawa kuwa watamtangaza mgombea baada ya siku tano. Nadhani sasa ifike mwishe waende coallition of the willing.C.u.f.tumewapa nafasi ya uraisi Zenj nako bara mwataka.Sasa hata wananchi wanaanza kuona hata wakiwachagua bado mtakuwa viongozi wababaishaji. Pia kwako Mbatia nasikia idadi ya wabunge wako wamepunguzwa na Zitto kwani Machali wa Kasulu ameshanyakwa na ZZK na wengine wako mbioni haswa hao wa Kigoma ila Kafulila nina hakika ana msimamo thabiti. Ubunge wako Vunjo nakujakikishia utashinda kwa kishindo.
 
Ningependa kujua mwaka 2000 (kama sikosei) wakati Chadema walipoungana na CUF na kumsimamisha mgombea urais mmoja (Prof. Lipumba) ili swala la ruzuku na viti maalum lilitatuliwaje? Kama mwaka 2000 walipata mhafaka kuhusu ruzuku na viti maalumu kinachoshindikana kwa wakati huu ni nini?

Kwa maoni yangu muungano huu watakaofaidika ni CUF, Nccr na NLD kuliko Chadema maana CUF wana wabunge wawili (kama sikosei) wakuchaguliwa huku bara, na kwa hali ilivyo uwezekano wa Cuf kupata wabunge zaidi bila Ukawa ni mdogo..
Hivyo hivyo kwa NCCR wabunge ni watatu wa kuchanguliwa na hata hivyo mmoja keisha jiengua kwenda ACT na bila shaka hata hawa wawili waliobaki uwezekano wa kwenda ACT ni mkubwa kuliko kubaki NCCR, hivyo basi utaona hata kwa NCCR uwezekano wa kupata wabunge zaidi ya 3 haupo ila kwa kupitia Ukawa NCCR wanaweze kutapa walau wabunge 5 mpk 10 (ukijumlisha na wabunge wa NCCR walipo sasa)

NLD nayo stori ni ile ile..

Tukirudi kwa Chadema uwezekano wa kupata wabunge zaidi iwe ndani ya Ukawa au nje ya Ukawa ni mkubwa maana Chadema wamejijenga tangu mwaka 2010, viongozi wao wanaotarajia kugombea katika majimbo mbali mbali wameweka mzizi yao tangu mwaka 2010 tofauti na vyama vingine.

Hivyo basi ni muhimu kwa vyama vinavyounda Ukawa kuangalia kwa mapana faida zinazopatika wakiwa pamoja.. kuliko kuangalia faida wanazopata viongozi wa hivyo vyama.

Ukawa wekeni maslahi ya Watanzania mbele, watanzania wako tayari kwa mabadiliko..
Unachokosea ktk kufikiri ni kwamba UKAWA sio chama kila mmoja wao anatafuta viti zaidi ama kunufaika na UMOJA HUU sio swala la kujali wananchi wala kutaka kuiondoa CCM madarakani. Hivyo huwezi kusema vyama vingine watafaidika kuwa na Chadema, kwa mfano CUF wanaona Chadema ndiye anawatumia ili akubalike Zanzibar ambako Chadema hana hata kiti kimoja..

na kitu kikubwa ambacho wapenzi wa Chadema na CUF hawakukifikiria kwa makini ni kwamba pande zote mbili wana interest zao toka mwanzo. Tanganyika Huru kwa CDM, na Zanzibar Huru kwa CUF ikimaanisha - UTENGANO. How can they UNITE...A Puzzle!
 
Kuna hekima kubwa katika andiko hili. UKAWA ni lazima ifanye maamuzi sasa, hakuna sababu ya kuwatesa wananchi kwa kuwaweka katika hali isiyoeleweka. Ninaamini sana kuwa NCCR, NLD na CHADEMA wana dhamira isiyo na mashaka na isiyoyumba. Kama CUF mpaka leo hii hawana maamuzi, ni lazima washirika wa UKAWA walio tayari wafanye maamuzi.

Kuchelewesha kufanya maamuzi kuna athari kubwa kuliko kufanya maamuzi mapema. Hivi kama CUF wakendelea kujivuta vuta kama wananvyofanya sasa mpaka mwishoni mwa July, halafu baadaye ikaonekana hakuna uwezekano wa kupanda mashua moja, ni lini washirika waliobakia watawaandaa wagombea wengine katika majimbo yale waliokuwa wameachiwa CUF? Sioni dhamira ya dhati ya CUF kwenye UKAWA. UKAWA halikuwa jambo la dharula.

Mkuu ktk siasa timing ni kitu cha Msingi Sana.
Kwa mtanzania Kama mm nisiye na chama na hata nikiwa nacho basi nitaifa langu Tanzania
Nimeumia Sana na Tamaa binafsi za wamoja hawa na real Inanipa picha negative nikiwa nawatathimin.

All in all my desire nikuwaona wakiwa pamoja na wakilitetea taifa langu
 
Practically muungano wa Ukawa unakufa mwezi huu hata August hautafika
 
Hivi vyama vyote vinavyounda UKAWA haviaminiani kabisa. CUF wanajua kabisa CHADEMA wakisimamisha mgombea wa urais na akashinda basi wao hawana chao, mawaziri wote watatoka CHADEMA vivo hivyo kwa CHADEMA. Sasa hapa ili wasiendelee kutupotezea muda kila mtu achukue time zake na asimamishe mgombea anayemtaka yeye toka chama chake kuliko kuendelea na haya maigizo yasiyoisha.
 
Unachokosea ktk kufikiri ni kwamba UKAWA sio chama kila mmoja wao anatafuta viti zaidi ama kunufaika na UMOJA HUU sio swala la kujali wananchi wala kutaka kuiondoa CCM madarakani. Hivyo huwezi kusema vyama vingine watafaidika kuwa na Chadema, kwa mfano CUF wanaona Chadema ndiye anawatumia ili akubalike Zanzibar ambako Chadema hana hata kiti kimoja..

na kitu kikubwa ambacho wapenzi wa Chadema na CUF hawakukifikiria kwa makini ni kwamba pande zote mbili wana interest zao toka mwanzo. Tanganyika Huru kwa CDM, na Zanzibar Huru kwa CUF ikimaanisha - UTENGANO. How can they UNITE...A Puzzle!

Nimesema hivi: Ningependa kujua mwaka 2000 (kama sikosei) wakati Chadema walipoungana na CUF na kumsimamisha mgombea urais mmoja (Prof. Lipumba) ili swala la ruzuku na viti maalum lilitatuliwaje? Kama mwaka 2000 walipata mhafaka kuhusu ruzuku na viti maalumu kinachoshindikana kwa wakati huu ni nini?

Utaona kuwa swala la muugano wa vyama vya siasa si jambo geni kwani Cuf walishaungana na Chadema pia NCCR mageuzi walishaungana na Chadema katika urais.. Swali langu ni je swala la ruzuku lilitatuliwaje?
 
Back
Top Bottom