Coalitions of the willing (UKAWA)

bulunga

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
303
49
Mwanzo sikutegemea hata siku moja yaliyo semwa na Kagame yanaweza kuwa na mantiki, kwa kuwa watu mnapoamua kushirikiana katika jambo fulani, lengo lenu huwa ni moja, lakini kama wenzako au mwenzenu hayuko tayari na anaanza kuwa na sababu, au visingizio visivyo na msingi au ucheleweshaji usio na maana katika kutimiza malengo yenu, huyo anakuwa ama hana nia ya dhati au hajiwezi, hapo anatafuta sababu ili awakwamishe walio tayari.

Hali kama hiyo inapotokea hulazimisha maamuzi au njia mbadala itumike kuweza kukamilisha malengo mliyo jiwekea. Malengo pia huongozwa na muda au time frame.

Nimesikia mengi kuhusu ukawa na mengi yanaendelea sasa hivi, nilimsikia Mbatia akilalamika CHADEMA wasijifanye wao ndio UKAWA wakaelekea kwenda kwenye uchaguzi bila wenzao akatoa na uangalizo kuwa wakifanya hivyo watatandikwa vibaya sana, hapa hofu ya Mbatia ilikuwa kuwa CHADEMA walikuwa na nia ya kujitoa katika UKAWA na kuwaacha wenzao solemba hivyo ndivyo nilivyo muelewa Mbatia.

Juzi tulitegemea jina la mgombea wa UKAWA kuwa lingelitangazwa lakini kwa mshangao wa wengi haikuwa hiyo, maneno mengi yakafuatia mara CUF hawakualikwa wala hawakuwa na taarifa ya uwepo wa mkutano huo, ingawa awali professor Lipumba alitoa ratiba ya lini mgombea wa UKAWA angelipatikana.

Kwa hali iliyotokea na taarifa mbali mbali zinazao tufikia, zingine zina pingana inatufanya tuamini kuwa kuna tatizo kama sio matatizo makubwa ndani ya UKAWA.

Kama haya yametokea ni dhahiri huu umoja huu una matatizo, hapo ndo inakuja ili dhana mzima ya mheshimiwa Kagame linakuwa na maana.

"COALITION OF THE WILLING" Ukawa lazima wajue muda sio rafiki tena na ni vigumu wapinzani wote waingie kwenye mashua moja walio tayari Mashua ing'oe Nanga maisha yaendelee, kuendelea kuwa subiri CUF haitasaidia na italeta madhara makubwa zaidi.
 
I support you 100% mkuu, mimi nawashangaa sana CHADEMA, hivi hawana think tank wa kuwashauri mpaka sasa? Tuna ushahidi ulio wazi uchaguzi uliopita Lupumba aliuza kura kwa kikwete kumsaidia Muislamu mwenzao, leo hii CHADEMA wanaingia mtegoni kirahisi hivi.

Shame to CHADEMA
 
Naungana na mtoa mada kws asilimia zote. waliotayari waamue kuwasubiri cuf ni kupoteza muda.
 
Kaz ipo...
 
Attachments

  • 1437062529732.jpg
    1437062529732.jpg
    21 KB · Views: 648
Kama CUf, walikuwa yote haya ambayo yamekuwa yakifanyika na nia nilikuwepo kwann, vikao vyaokwann havikupangwa ku accommodate haya, kama ni Bahati mbaya Nina waswas na uwezo, nia yao ni nini
 
Subira yavuta kheri, CUF wasubiriwe ila UKAWA wawe tayari to bow down to CUF demands. Niliwahi kusema mahali kuwa CUF ina wagombea wa kudumu kwenye urais. Prof. Lipumba na Maalim Seif wamegombea mara 4 hii ni ya 5!. Angalau Maalim akijaribu tena ana posibility ila Lipumba kura zake zimekuwa zikipungua mwaka hadi mwaka na kwa vile hakuwahi kugombea ubunge, kwake kugombea urais ndio full lifetime profession yake akikubali mwingine yeyote kugombea, he will be rendered jobless!. Kwa Lipumba kugombea urais kwake sasa imekuwa ni hobby anagombea tuu ili agombee tuu na sio kwa lengo la kupata ushindi!. Yuko tayari ku risk kulazimisha mgombea wa UKAWA lazima awe yeye and it doesn't matter kama anagombea kushinda au kushindwa kwa sababu lengo ni kugombea tuu na sio kushinda after all ameisha zoea kushindwa hivyo hata akishindwa kwake ni sawa tuu!.

Msubirieni tena yeye atajinyamazia kimya na kujifanya ni WanaCUF ndio walioamua lazima ama awe yeye mgombea wa UKAWA ama CUF watajiondoa ndani ya UKAWA.
Pasco
 
Pasco, ni kweli subira yavuta kheri,unasema nn juu ya kauli za CUF na muda uliobaki
 
I love you pasco....one day fikiria kuvua gamba broo
 
I always watched cuf with triangle eyes...! CHADEMAS are lenient but never with cuf...! Never on earth
 
Unaweza ukakasirika ukakuta umejipigiza ukutani, na ukajuta kuijua CUF, tulifurahi ilipojitoa kuwa CCM B, pamoja na CCM kutumia polisi kumtandika Lipumba bado analeta simtomfaamu, hakika malengo ya ukawa yanakatisha tamaa
 
bulunga

Kimsingi sisi wana chadema tulikiwa tunasita sana kulisema hili ila sasa inabidi tuliseme.Wenzetu walishakuwa tayari na majibu.Waliamini kuwa mgombea ndiye ambaye angepita lakini imekuwa kinyume na matarajio yako.Mpaka nina uhakika wenzetu hawako tayari.Hivyo inatupasa sisi chadema tusonge mbele.Imeshangazwa kusikia eti mpaka kamati kuu yao ikae tarehe 25.Kwani walipokuwa wanaingia makubaliano na UKAWA kamati kuu hawakushirikishwa??? Yaani ni mambo ya kitoto ambayo hayafai kwa mtu mzima.Chadema tusonge mbele hao hata wakikubali "masharti"yao yatakuwa mengi sana na ya ajabu ajabu!
 
Last edited by a moderator:

Agiza za barrrrdi za kutosha kabisa
 
Kuna hekima kubwa katika andiko hili. UKAWA ni lazima ifanye maamuzi sasa, hakuna sababu ya kuwatesa wananchi kwa kuwaweka katika hali isiyoeleweka. Ninaamini sana kuwa NCCR, NLD na CHADEMA wana dhamira isiyo na mashaka na isiyoyumba. Kama CUF mpaka leo hii hawana maamuzi, ni lazima washirika wa UKAWA walio tayari wafanye maamuzi.

Kuchelewesha kufanya maamuzi kuna athari kubwa kuliko kufanya maamuzi mapema. Hivi kama CUF wakendelea kujivuta vuta kama wananvyofanya sasa mpaka mwishoni mwa July, halafu baadaye ikaonekana hakuna uwezekano wa kupanda mashua moja, ni lini washirika waliobakia watawaandaa wagombea wengine katika majimbo yale waliokuwa wameachiwa CUF? Sioni dhamira ya dhati ya CUF kwenye UKAWA. UKAWA halikuwa jambo la dharula.
bulunga
 
Last edited by a moderator:
Subira yavuta kheri, CUF wasubiriwe ila UKAWA wawe tayari to bow down to CUF demands. Niliwahi kusema mahali kuwa CUF ina wagombea wa kudumu kwenye urais. Prof. Lipumba na Maalim Seif wamegombea mara 4 hii ni ya 5!. Angalau Maalim akijaribu tena ana posibility ila Lipumba kura zake zimekuwa zikipungua mwaka hadi mwaka na kwa vile hakuwahi kugombea ubunge, kwake kugombea urais ndio full lifetime profession yake akikubali mwingine yeyote kugombea, he will be rendered jobless!. Kwa Lipumba kugombea urais kwake sasa imekuwa ni hobby anagombea tuu ili agombee tuu na sio kwa lengo la kupata ushindi!. Yuko tayari ku risk kulazimisha mgombea wa UKAWA lazima awe yeye and it doesn't matter kama anagombea kushinda au kushindwa kwa sababu lengo ni kugombea tuu na sio kushinda after all ameisha zoea kushindwa hivyo hata akishindwa kwake ni sawa tuu!.

Msubirieni tena yeye atajinyamazia kimya na kujifanya ni WanaCUF ndio walioamua lazima ama awe yeye mgombea wa UKAWA ama CUF watajiondoa ndani ya UKAWA.
Pasco

Ndugu yangu pasco tuwe wakweli,naamini kati ya member wa ukawa kuna watu kiukweli wanabebwa na hiyo nembo,mojawapo ni cuf kwa huku bara,ila husifikirie wewe ndio unaliona hilo no,kila mwenye macho analiona.
 
Unaweza ukakasirika ukakuta umejipigiza ukutani, na ukajuta kuijua CUF, tulifurahi ilipojitoa kuwa CCM B, pamoja na CCM kutumia polisi kumtandika Lipumba bado analeta simtomfaamu, hakika malengo ya ukawa yanakatisha tamaa

Mkuu bado tunazidi kuomba mambo yaende sawia
 
bulunga Acha propaganda za ajabu, wote mbatia tumemsikia wewe unayoyasema umetunga mwenyewe
 
suala hapo ni ruzuku, chama kitakufa bila ruzuku. pili viti maalumu vya ubunge. ndo maana hayo yote lazima yawekwe sawa. kumbukeni chama kitakachoweka mgombea wa urais ndo chenye haki ya vyote hivyo.
isitoshe chadema walishawaambia CUF ni ccm B na nccr ni ccm C. kwa hiyo sioni cha ajabu. na CUF wawe makini sana kushirikiana na hao jamaa. hawatabiriki. cuf wakiwa chama kikuu cha upinzani waliwashirikisha chadema. lakini kwa chadema walipokuwa chama kikuu cha upinzani waliwakataa.

Back
Top Bottom