Coalitions of the willing (UKAWA)

Coalitions of the willing (UKAWA)

Nimesema hivi: Ningependa kujua mwaka 2000 (kama sikosei) wakati Chadema walipoungana na CUF na kumsimamisha mgombea urais mmoja (Prof. Lipumba) ili swala la ruzuku na viti maalum lilitatuliwaje? Kama mwaka 2000 walipata mhafaka kuhusu ruzuku na viti maalumu kinachoshindikana kwa wakati huu ni nini?

Utaona kuwa swala la muugano wa vyama vya siasa si jambo geni kwani Cuf walishaungana na Chadema pia NCCR mageuzi walishaungana na Chadema katika urais.. Swali langu ni je swala la ruzuku lilitatuliwaje?
Kama sikosei swala la wabunge wa viti maalum kwa limeanza mwaka 2005 au?

CUF na Chadema hawakuwahi kuungana bali walifikia maridhiano ya mwanzo kusimamisha mgombea Urais mmoja, wakati wakipingana Ubunge katika majimbo na walishindwa vibaya. Na 2005 kila mmoja alikwenda kivyake, Muafaka bora ulikuwa ule wa vyama vyote vya Upinzani baada ya uchaguzi huu (2005) lakini wakaja korofishana kwenye kugawana majimbo katika serikali ya mitaa 2009. Wwakabakia CDM na CUF, nao wakaweka Uhasama baada ya CCM na CUF kuweka muafaka juu ya Zanzibar..

Swala la Ruzuku haliwezi kutatuliwa na moyo wa kimaskini hata siku moja, isipokuwa kwa wao VYAMA kuungana. Kama mirathi wanapotaka ndugu kugawana mirathi, udugu huwekwa kando na mali imechukua nafasi kubwa. Kwa hiyo hapo hakuna UMOJA mnapogombania ruzuku za majimbo.
 
Mwanzo sikutegemea hata siku moja yaliyo semwa na Kagame yanaweza kuwa na mantiki, kwa kuwa watu mnapoamua kushirikiana katika jambo fulani, lengo lenu huwa ni moja, lakini kama wenzako au mwenzenu hayuko tayari na anaanza kuwa na sababu, au visingizio visivyo na msingi au ucheleweshaji usio na maana katika kutimiza malengo yenu, huyo anakuwa ama hana nia ya dhati au hajiwezi, hapo anatafuta sababu ili awakwamishe walio tayari.

Hali kama hiyo inapotokea hulazimisha maamuzi au njia mbadala itumike kuweza kukamilisha malengo mliyo jiwekea. Malengo pia huongozwa na muda au time frame.

Nimesikia mengi kuhusu ukawa na mengi yanaendelea sasa hivi, nilimsikia Mbatia akilalamika CHADEMA wasijifanye wao ndio UKAWA wakaelekea kwenda kwenye uchaguzi bila wenzao akatoa na uangalizo kuwa wakifanya hivyo watatandikwa vibaya sana, hapa hofu ya Mbatia ilikuwa kuwa CHADEMA walikuwa na nia ya kujitoa katika UKAWA na kuwaacha wenzao solemba hivyo ndivyo nilivyo muelewa Mbatia.

Juzi tulitegemea jina la mgombea wa UKAWA kuwa lingelitangazwa lakini kwa mshangao wa wengi haikuwa hiyo, maneno mengi yakafuatia mara CUF hawakualikwa wala hawakuwa na taarifa ya uwepo wa mkutano huo, ingawa awali professor Lipumba alitoa ratiba ya lini mgombea wa UKAWA angelipatikana.

Kwa hali iliyotokea na taarifa mbali mbali zinazao tufikia, zingine zina pingana inatufanya tuamini kuwa kuna tatizo kama sio matatizo makubwa ndani ya UKAWA.

Kama haya yametokea ni dhahiri huu umoja huu una matatizo, hapo ndo inakuja ili dhana mzima ya mheshimiwa Kagame linakuwa na maana.

"COALITION OF THE WILLING" Ukawa lazima wajue muda sio rafiki tena na ni vigumu wapinzani wote waingie kwenye mashua moja walio tayari Mashua ing'oe Nanga maisha yaendelee, kuendelea kuwa subiri CUF haitasaidia na italeta madhara makubwa zaidi.
Heshima kwako!
 
Back
Top Bottom