Clouds TV na propaganda ya vita kisiasa

Clouds TV na propaganda ya vita kisiasa

Clouds ilishanunuliwa kwasasa ni chombo cha propaganda cha ccm

Asante Mkuu kwani tetesi hizi nilizisikia kuwa Rostam Aziz kanunua na kweli nimeona Jana tangazo la uchapaji kazi was Lowasa alipokuwa PM!!!
 
Clouds nikiiskiaga tu najihisi kutapika. Nikiwa kwenye daladala nashuka. Nikiwa mgahawani naacha chakula
 
Clouds ilishanunuliwa kwasasa ni chombo cha propaganda cha ccm

Ha ha haaa CLOUDS SUPER BLUNT Ha ha haa Efraim Kibonde aka bwabwa la CCM, Aliefeli pepa zake zote,Akibisha ntapost hum kopi ha hahaa, Yupo pale kwa hisani ya CCM, hatuwataki mpo too biased
 
Ha ha haaa CLOUDS SUPER BLUNT Ha ha haa Efraim Kibonde aka bwabwa la CCM, Aliefeli pepa zake zote,Akibisha ntapost hum kopi ha hahaa, Yupo pale kwa hisani ya CCM, hatuwataki mpo too biased

Post mkuu, hiyo ndo inaitwa Muhongo style.
 
Mkuu hiyo kituo ilishanunuliwa na rostam tayari kwa maandalizi ya mwakani ndo maana Jose ameenda Dubai

Hii nimeinasa sehemu pia.......ingawa tetesi mwanzo zilikuwa ni Manji
 
Kumbe hii ndiyo ID ya Ruge Mutahaba. Nilikuwa sijui


Hapana Mkuu,Pasco ni. Mwandishi wa habari(mwenyewe anapenda aitwe mwandishi huru) ambae ana "unasaba" fulani na ukada wa CCM na pia wagombea fulani wa uraisi ukianza na Lowasa, ila Rutashobola utakua umempata ndugu yake Rugemarila wa clouds!!!
 
Last edited by a moderator:
Hapana Mkuu,Pasco ni. Mwandishi wa habari(mwenyewe anapenda aitwe mwandishi huru) ambae ana "unasaba" fulani na ukada wa CCM na pia wagombea fulani wa uraisi ukianza na Lowasa, ila Rutashobola utakua umempata ndugu yake Rugemarila wa clouds!!!

Mbona ametiririka kama ruge mwenyewe
 
Last edited by a moderator:
clouds aina tofauti na radio uhuru!

Sincerely siwezi kukaa sebuleni kwangu eti nafungulia clouds natazsma. huo naiona lm tv ya mizaha zaha tu. ze comedy fulani hivi!nawafananisha na magazeti ya shigongo. umbea umbea na udaku tu!
 
Kituo hiki binafsi cha TV kinahatarisha upendo baina ya wanajamii katika Taifa hili na kuchochea chuki na uhasama kwa kutumika kufanya propaganda za wazi wazi dhidi ya chama pinzani-CHADEMA kwa makusudi kwa kushirikiana na CCM kwa indirect way kwa kichaka cha kutangaza uzalendo!! Tabia hii umekubuhu clouds radio na sasa inaanza kumea kwenye TV!

Kwa watazamaji wa kituo hiki,wataona kuna Tangazo ambalo linaonyeshwa siku hizi linaloanza na wimbo wa Taifa na hatimae mshereheshaji kuanza kuongea na kutaka taifa liombewe huku picha za mnato zikipita!!

Propaganda hii chafu imejaa kwenye picha hizi za mnato ambapo 70% zinaonyesha wabunge wa CHADEMA wakiwa bungeni na kwa kuhusisha pia maneno ya vita na kutolea mifano ya Nigeria,Somalia,Syria,Ukraine etc huku pia yakionyeshwa mafuvu ya watu!!!

Tatzo lipo kwa nini wamebezi tu kuwaonyesha; Tundu Lissu kwa kurudia rudia akiongea na sio Mwanasheria Mkuu aliyejaribu kumpiga Kafulila ndani ya Bunge na hata kumkata kichwa??!!

Anaonyweshwa Ezekiel Wenje mara kadhaa huku akipunga vidole viwili juu na sio Serukamba aliyesema Fuc.k you ndani ya bunge???!!

Anaonyeswha Joseph Mbilinyi akivutwa na walinzi wa bunge na kwa nini sio Juma Nkamia aliyesema haongei na mbwa bali mwenye mbwa ndani ya bunge huku akimjibu binadamu mwenzie??!!

Kwa wafuatiliaji inafahamika wazi kuwa wamiliki wa kituo hiki wapo karibu na watawala na imefikia pahali sasa wakiandaa na kuhodhi dhifa za kitaifa kama tukio la uzinduzi wa video ya uzalendo ya wasanii pale Dodoma,birthday ya Kikwete na keki juu,uzinduzi wa mradi wa Malaria miaka kadhaa iliyopita utafikiri hakuna vyombo cha serikali-TBC TVS na Radio!!

Imefikia pahali hadi Raisi na mawaziri wanatumika na kituo hiki binafsi kuandaa jingles za radio huku wakikiacha solemba kituo cha Umma!!!

Hata propaganda za raisi kijana zilianzia clouds Fm 2012 kwa kuwahusisha January Makamba na Zitto kwenye segment ya kitaa kinasema katika kipindi cha XXL na vinginevyo!!

Mauaji ya Rwanda hata na kule Kenya wakati wa uchaguzi yalichochewa na vituo binafsi vya radio kwa kuchochea chuki dhidi ya upande mwingine/kabila lingine na ndio maana kuna wakurugenzi kadhaa wameshitakiwa kimataifa,clouds nao naona hawaridhiki na faida wanazopata na sasa wanajiingiza kwenye chuki za siasa kwa hadaa za uzalendo!!!

You don't like it change the channel thank you!
 
Kwa upande wangu mimi wanakosea uwaonesha wapinzani. Je kesho itokee upinzani unachukua dola. Ni risk kwao kwa cku za mbele. Watangaze uzalendo bila kunyoosha vidole kwa watu fulani.
 
Back
Top Bottom