Labda inabid upitie hapa mkuu, hawa jamaa ni kweli wana nguvu kiasi, japo siamin sana kama mwandishi alivyoandika hapa
========
88.5 Fm ndo frequency zinazokufanya uipate redio hii ukiwa katikati ya jiji la Dar es Salaam, na Viunga vyake.
Kwa takribani miaka mitano sasa hakuna ubishi kuwa clouds fm ndo redio inayopendwa, na kusikilizwa na wengi nchini.
Wasanii wa muziki wa bongo fleva wengi wanaamini kuwa kama wimbo wako usipopigwa katika kituo hiki basi wimbo huo hauwezi kutoka, na wasanii hao hao wengi wana amini kuwa kwamba kama msanii asipokuwa na mahusiano mazuri na kituo hiki, basi hata kama Vituo vingine vikicheza nyimbo zake masaa yote hawez fika popote, hawezi fikia mashabiki wake, hawez pata hata dili za matamasha na zile za matangazo (Endorsement) kwa urahisi.
Kampuni za matangazo na maofisa masoko wa makampuni mbalimbali nao hawapo nyuma katika hili, wengi wanaamini kuwa kama unafanya kampeni ya kutangaza bidhaa yako, ni lazima CloudsFm iwe katika list na ikibidi itengewe bajeti ya kutosha, kwani wanaamini kuwa Redio hiyo ina ushawishi mkubwa sana kwa wateja wa bidhaa na huduma zao mbalimbali.
Huku mtaani watu wanaamini clouds wapo katika kila jambo kubwa linalotokea nchini, na Mkurugenzi wa vipindi Bwana Ruge Mutahaba amekuwa akitajwa kama mmoja kati ya watu wenye ushawishi mkubwa na nguvu kubwa na katika tasnia ya burudani nchini Tanzania.
Matokeo ya Tafiti za taasisi ya Ipsos Tanzania, Taasisi inayojishugulisha na utafiti wa masoko kwa nchi mbalimbali Duniani, zimekuwa zikiitaja Clouds fm kama redio inayoongoza kwa kusikilizwa,
Mwaka 2014 Network Africa, yenye mako yake nchin Uingereza iliifanya utafiti wa redio bora 20 zaid Afrika na katika list hiyo Clouds ilikuwa ni ya nane, kwa Afrika, wakati kwa Afrika Mashariki ikishika nafasi ya Pili nyuma ya Citizen Fm ya kenya iliyokuwa ya Kwanza, Pia Clouds Fm imetajwa kuwa moja kati ya superbrands za Afrika mashariki kwa miaka mitatu mfululizo, 2013, 2014 na 2015.
Swali la kama Clouds ni redio kinara au laa, sio swali tena, jambo muhimu la kujiuliza ni kuwa ni namna gani wameweza kuwa kinara katika sekta yenye ushindani mkubwa kiasi hiki, kumbuka Kuna redio takribani 123 zilizosajiliwa na TCRA.
Ukiacha sababu ya kwamba wanawalenga vijana (Target Market) ambao ndo asilimia kubwa zaidi ya wananchi wa Watanzania, kuna vitu vingine vya ziada ambavyo pengine redio nyingine ambazo nazo zimewalenga vijana wa rika hilo hazijafanya na ndio maana clouds fm imebaki kuwa redio inayosikilizwa zaidi.
Hizi ni siri tano ambazo
Fidelis Madaha mjasiriamali na mshauri wa biashara toka
SIYB Association of East Afrika anatushirikisha kuwa zimechangia Clouds fm kuwa juu katika redio nchini Tanzania
- Ni Wabunifu na wana ari ya ujasiriamali (Entrepreneurship spirit): Tangu kuanzishwa kwake mwaka 1998 Clouds fm wamekuwa vinara wa ubunifu kwa kuleta vipindi vilivyoleta mapinduzi makubwa sana katika muziki na maisha ya kawaida. Ubunifu wa Miradi mbalimbali iliyo chini ya Clouds media group inayotekelezwa na vijana wabunifu na walio hamasika. Mwanzilishi wa redio hii Ndugu Joseph Kusaga, na mbia wake wa karibu Ruge Mutahaba, ni mfano sahihi wa namna ambavyo kijana akifuata kile kitu kilicho ndani ya moyo wake, na kuwa na bidii anaweza akafikisha malengo yake. Ni wazee wa fursa, na hawaachi fursa ipite hivi hivi.
- Wanajua Vipaji na wanashiriki Kuvivumbua: Kuna msemo kuwa “Good managers knows how to spot their top talent”, na huu ni ukweli sana, haswa kwa Mkurugenzi wa uzalishaji na vipindi Ndugu Ruge Mutahaba. Walio karibu nae wanasema ni mtu ambaye ana sikio la kusikia kitu kizuri na macho ya kuona, ni mtu ambaye akimsikia mtangazaji kwa mara ya kwanza, anaweza jua kama mtangazji huyo ana kipaji au laa na kama ana kipaji ni wapi anaweza mweka ili afanye vizuri zaidi. Kwa clouds fm utangazaji ni zaidi ya shule na vyeti ambavyo mtangazaji atapeleka. Uwezo binafsi wa mtangazaji kujiongeza unaangaliwa pia.
- Wakiona Kipaji wanakifungulia njia ya kukua: Wana kampeni yao wanasema tunakufungulia njia kuwa unachotaka, pengine inaweza kutumika hata kwa wasikilizaji wao, lakini haswa haswa nadhani ni kwa wao wenyewe (Watangazaji ) na wasanii. Wengi wa watangazaji na wafanyakaz wengine wa Clouds fm walikuwa ni watu wenye vipaji lakin pengine kutokana na kutokuwa na uzoefu wa kutosha au Elimu ya kutosha wasingeweza kupata nafasi ya kufanya kazi kwenye Media houses nyingine, lakin Clouds fm walipowaona wakawapa nafasi ya wao kuonesha kile walicho nacho, nafasi ambaye wasingepewa na watu wengine, mwisho wa siku, Clouds fm wananufaika na vipaji hivyo na wakati huo huo mwenye kipaji nae ana nufaika pia, hii ni sawa sawa pia hata kwa wengi wa wasanii wa muziki wa Bongo Fleva, wakongwe kama Dully Sykes, Mwasit Godziller na Diamond Platnumz wote kwa nyakati tofauti wamekaririwa wakisema kuwa kama Clouds fm wasingehusika katika namna moja au nyingine katika kuvumbua vipaji vyao yamkin wasingekuwa hapa.
- Wamegundua namna bora zaidi ya kufanya kazi na vijana: Vijana wanapenda uhuru na wanapenda kuaminiwa na wakiaminiwa wanafanya kazi kwa kujituma , Clouds fm wamelitambua hilo na wanalitekeleza, wametengeneza utamaduni wa kazi ambao unaruhusu vijana kuwa huru na kufanya kazi kwa kujituma. Ukiangalia Mtangazji wa Clouds anavyotangaza na anavyojitawala katika kipindi chake unaweza dhani kwamba kile kipindi na redio nzima ni yake, hii ndo siri kubwa kuliko zote na ndo sababu inayowafanya wazidi kuwa juu kila siku. Kumbuka Asilimia kubwa ya wafanya kazi wa Clouds Fm ni Vijana, na ni vijana wa kisasa haswa, baadhi wanaweza kuqualify kwa definition ya Millennials, lakin wengine hawapo katika rika hilo, ila ni ukweli usiopingika kuwa uongozi wa Clouds fm umejua namna bora ya kuwafanya vijana kufanya kazi na kuwa wabunifu, Watangazaji wanaachwa huru kuwa na vitu vyao vya pembeni ambavyo media houses nyingine zingechukulia kama ni kuleta mgongano wa maslahi, lakin kwa Clouds fm wanaruhusiwa na hivyo ndivyo vijana wanavyopenda kufanya kazi.
- Mpangilio mzuri wa vipindi na Mpangilio wa Watangazaji: Kama kuna kitu kingine kikubwa Clouds wanachowazidi redio nyingine, ni mpangilio wao wa vipindi, na namna ambavyo team za watangazaji zimepangwa. Watangazaji wanaopangwa kutangaza pamoja ni wale ambao chemistry ina match, na wanakuwa hawapati ugumu wa kufanya kazi pamoja. Hii inabebwa na ule uwezo wa kutambua vipaji na kujua kuwa wapi nikiweke ili kitumike vyema. Pamoja na kwamba Clouds fm wamevishwa nafasi ya redio ya taifa, wameaminiwa na wasikilizaji, wameaminiwa na serikali na katika ulimwengu wa sekta binafsi ya Tanzania, bado wanajituma na wanaendelea na ari ileile waliyokuwa nayo wakati bado ni wachanga. Pengine si ajabu tukiona kuwa wameendela kushikilia nafasi hii waliyonayo.
Disclaimer:
Maoni haya ni ya Fidelis Madaha, siyo ya SIYB Association of East Afrika,Tzinsight wala taasisi yeyote inayohusiana na Fidelis Madaha kwa namna yeyote ile.