Unataka kutuaminisha kuwa TBC wana vipindi vizuri sana, muonekano mzuri sana kuliko chanel nyingine ila wananchi wameisusa kisa wanaipendelea ccm? Unapotoka kabisa, kama kuipendelea ccm ndio kufa hao clouds wameshindwa vip kufa tangu 2015 walipoipendelea ccm?
Hebu TBC waje na muonekano mzuri na vipindi vizuri tuone kama watakupotea, nani aangalie chanel yenye muonekano wa zamani na vipindi vya mwaka 47 wakati kuna chanel nyinyine zenye muonekano mzuri,vipindi vinavyogusa jamii kubwa, watangazaji wenye mvuto kwa watazamaji, matukio yenye mvuto kwa watazamaji wengi.
Mchawi wa TBC usijidanganye kuwa ni watu kuwaambia wananchi bali ni ubunifu wao wenyewe.
Clouds wamejipanga kufanya biashara na sio kumfurahisha kila mtu na chama chake, kama wanajua wengi wanataka burudani katika muda fulan watahangaika naye wapate wanachokitaka, kama ni ziara za makonda wenzako wamecheza kibiashara kwani walijua hata wapinzani watataka kujua Makonda karopoka nini leo.
Kama unafatilia sakata la Clouds na upinzani limeanza lini basi usijihangaishe kabisa hao ni wafanyabiashara wazuri tu, waukize wenzako wa hip hop waliongizwa mkenge na sugu leo wako wapi na clouds iko wapi.
Sio kila anayeipenda ccm anaweza kupotea kizembe , Diamond waliyemsusia yuko wapi sasa hivi ukilinganisha na wale wengine? Biashara ni akili na sio kumridhisha kila mtu. Clouds wana uwezo wa kubadilika kutokana na muda, siku ukawa ikawa na maslahi kwao watajipeleka ila kama hakuna watatafuta kwingine.