Clouds kwa hili la Clouds Plus mmezidi!

~~>>>Acha kulalamika.. Kama unaona anakudhulumu acha kilipia. Kwani umelazimishwa???
 
~~>>>Acha kulalamika.. Kama unaona anakudhulumu acha kilipia. Kwani umelazimishwa???
Utakuwa mbuzi kama unahisi kuhoji ni kulalamika, mwanadamu ni lazima utafute why? Katika kila jambo si tu kukubali kisa umeletewa. Acha tuwasaidie na wengine we nenda kamliwaze mkeo kitandani
 
Kuna wizi wa kutumia shule ndo huu mkuu. Kama shule hamna kichwani watu wa hivi watawapata wengi sana, si unajua wajinga ndio waliwao
 

Kuangalia Clouds Plus ni hiyari Jamaa ameiweka kibiashara hivyo kama unahitaji lipia, mbona Azam walipoongeza Azam sports2 wameoongeza elfu tatu ili uione? kifurushi mwanzo kilikuwa 15,000/= lakin kwa sasa tunalipa 18,000/= hilo hujaliona na wewe unasema nimtumiaji wa muda mrefu wa AzamTv, ukilipia ile 15,000/= huoni Azam Sport2. Acha chuki binafsi kama huwezi lipia piga kimya
 
ndiyo maana imeitwa Clouds plus yaani wewe plus 3000 kama hutaki unaacha tu.
 
Download Afrobox japo ni yao, me naTafuta App ambayo in Channels za tz, at the end huyu lazma niangalie kvyovyote bila buku3.
Ukipiga hesabu ya bundle unayotumia kutizama via afrobox utakuta ni heri ulipe hiyo 3000 kwa mwez maana kutazama channels online kunahutaji bundle ya kutosha so kwa mwezi utatumia kiasi gani.
Hapo ni sawa na kuruka mkojo ukakanyaga mavi
 
ndiyo maana imeitwa Clouds plus yaani wewe plus 3000 kama hutaki unaacha tu.
Watanzania watu wa ajabu kweli, hii channel haina hata miezi mitatu toka iongezwe.
Wakati haipo wala hawakulalamika, kwahiyo kama mtu anaona kulipia 3000 ni bei si anaipotezea tu kama vile kipindi ambapo haikuwepo.
Mbona azam sports2 hawalalamiki inapowabidi walipie 3000 zaidi kuipata.
Wengine wanadai kuwa haina chochote, lakini still wanalalamika kutoiona.
Mimi personally sioni la maana kwenye hiyo clouds plus na siwezi kuilipia maana haina effect kwangu.
Mimi channel nnayopenda ni IDX, discovery na national geographic yani hizo hata wangesema kuipata IDx uongeze 3000 ngelipa tu.
 
Huyu Ruge na uongozi wake wana njaa ya tumbo kinouma.. mambo gani sasa haya wanaleta... hivi huko plus kuna nn cha ajabu...!!!
 
Slogan yao sasa wanasema fursa inaanzia sokoni kwa hiyo kafanya king'amuzi cha azamu kama soko kisha kaleta biashara yake ya clouds plus now anapiga tu hela buku 3 tatu
 
kaz kwa wapenda fiesta/clouds....... c wengine hatuna presha.
 
Wangeachia Rai Italy kwenye kifurushi cha 18000/- halafu wangefuta channel zote za bongo movie ningefurahi sana kwangu mimi binafsi.
 
Nunua DSTV hutojutia pesa yako. Achana na Haya makitu
 
Kwani kwenye hiyo channel kuna nini cha ziada? Kama ni michezo ukilipa 15 kuna channel kibao, kama ni muvi za kibongo sinema zetu IPO, kama ni muziki zipo kibao; mfano etc, eatv, AZAM 2 NA za nje. Clouds plus kuna nn special? Naomba mnijuze. Ikiwezekana kwe dikoda yangu waiondoe tu hiyo channel sina haja nayo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamaa anajua kucheza na akili za watu..achana name hilo.hebu fikiria kaja na tatu mzuka..yote hiyo ni kutengeneza mifereji ya pesa..ila uzuri ni kwamba hulazimishwi..uamuzi ni wako.
Mbona hiyo tatu mzuka iko kila mahali, EA RADIO ipo na hata huko kenya ipo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu ni ujinga tcra wamelala tu

“Start where you are. Use what you have. Do what you can.”

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…