GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,212
Katika hali isiyokuwa ya kawaida imegundulika ya kwamba vituo viwili vya redio hapa nchini Tanzania na ambavyo vimejizolea umaarufu mkubwa sana kwa wasikilizaji huku vikiwa vinafanya vizuri vya E-FM na Clouds FM vimejikuta vikiingia katika vita kali a.k.a bifu zito ambalo kwa dalili zinazoonekana kama mamlaka husika hawataingilia kati uadui wao huu utafika pabaya.
Chanzo cha bifu cha awali
Mara baada ya mtangazaji wa michezo Ibrahim Masoud " Maestro " kuhitilifiana na wenzake hasa hasa na mtangazaji mtumbuizaji Mbwiga Mbwiguke na baadae Alex Luambano kwa tabia za Ibrahim Masoud kuwadharau na kuwadhulumu wenzake katika mambo kadha wa kadha ilipelekea mtangazaji huyo " Maestro " kukosa ushirikiano hali iliyopelekea kuanza kutafuta ajira mahala pengine kisha ndipo akapata kazi E FM.
Bifu la pili
Mara baada ya kuwepo kwa bifu kali na zito la watangazaji wawili wa kike Dina Marios na Zamaradi Mketema juu ya mume mmoja waliyekuwa wanamgombania hapo Clouds media ila sasa zamaradi kaonekana kakamatia ( jina nalihifadhi ila nadhani wote mnamjua huyo bosi kiwembe) ambapo huyo bosi alionekana wazi kumpenda zamaradi mketema huku akimfanyia mambo makubwa mazuri na ya kimaendeleo na kuachana na Dina Marios ilipelekea wawili hawa kuwa na uadui uliotukuka hadi dina marios alipoona hatakiwi na hathaminiwi na bosi kiwembe wa Clouds Media Group na kuamua kutafuta kazi na kubahatika kupata ajira mpya redio ya E FM na sasa anafanya vizuri.
Bifu la tatu
Hakuna asiyejua kuwa watangazaji Maulid Kitenge (sasa ni mkuu wa idara ya michezo E FM) na Shaffi Dauda (sasa ni meneja vipindi Clouds Media Group ) wana bifu kali na zito ambalo lilianzia kipindi kile cha iliyokuwa kamati ya saidia Taifa Stars ambapo baadae tukafungwa goli zetu saba (7 ) nzuri tu huko kwa Waarabu.
Ikumbukwe kuwa katika kamati hiyo waliteuliwa waandishi wa za michezo magwiji hapa tanzania Saleh Ally, Mahmoud Zubeiry, Maulid Kitenge na Shaffi Dauda waongoze kamati ndogo ya uhamasishaji ambapo shaffi dauda wazi wazi alijitokeza na kusema kuwa hawezi kuwepo humo kwakuwa watu aliokuwa nao wapo wasiojua mpira hasa mambo mazima ya kimkakati hivyo akaamua kujitoa ila maulid kitenge alijisikia vibaya na kudai kuwa katukanwa kisaikolojia na Shaffi Dauda kuwa yeye hajasoma bali anaishi tu kiujanja unjanja na hicho kipaji cha utangazaji. Hadi hivi ninavyoandika uzi huu Shaffi Dauda na Maulid Kitenge ni sawa sawa na wanamgambo wa al - shabaab na nchi ya kenya (nikimaanisha wana uhasama mkubwa mno).
Bifu la nne na ambalo ndilo la hatari zaidi
Tokea mtangazaji mtumbuizaji Mbwiga Mbwiguke akubalike ( nikiri hata mimi namkubali kunakotukuka) na wasikilizaji kutokana na vionjo vyake ambavyo vinanogesha kipindi cha michezo cha Clouds Fm imesababisha hadi waandishi wengine wa habari za michezo na hata wananchi pia waanze kuyatumia hayo maneno ya Mbwiga kama neno la "figisu figisu" na yameshika mno.
Kuna neno moja ambalo Mbwiga Mbwiguke anapenda kulitumia la "kampa, kampa tena " linalomaanisha kuwa wachezaji wanapigiana pasi sana. Katika kuelekea katika mpambano wa Dar es salaam derby au ilala derby au wakongwe wasio na maendeleo derby au wasanii derby la Simba na Yanga mtangazaji muongozaji wa E FM Maulid Kitenge amekuwa akilitumia sana na hasa anapokuwa anatangaza habari ihusuyo timu ya simba ambao kiuhalisia ndiyo hucheza hivyo.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida jana usiku katika kipindi cha michezo cha Clouds FM mtangazaji na mchambuzi mahiri wa michezo shafii dauda alisikika akisema tena kwa hasira na vijembe kuwa kuna watu wapuuzi tu wanatoka huko walikotoka wanatumia hilo neno la "kampa kampa tena" ndivyo sivyo na wanadandia tu ndipo akaibuka mwenye neno mtangazaji mtumbuizaji Mbwiga Mbwiguke na kusema kwa madoido yake kuwa watu waache kusafiria nyota za wenzao na kwamba hawatamuweza ng'o na wakae wakijua kuwa hapa nchini Tanzania redio mama kwa mambo yahusuyo michezo ni Clouds Fm tu lakini baadae wakapotezea na kuendelea na taarifa zingine za michezo.
Tukio linaloendelea sasa hivi E-FM
Sasa hivi katika kipindi cha sports headquarters ambacho kipo hewani wakati Maulid Kitenge anatangaza akalisema tena hilo neno la "kampa kampa tena" ndipo akaibuka mtangazaji mwenzie Ibrahim Masoud " Maestro " na kusema kwa kukejeli na sanifu kuwa wamekatazwa kulitumia hilo neno, (ila hakusema na nani ila wafuatiliaji wa redio hasa vipindi vya michezo tukaelewa anamlenga nani) ndipo Maulid Kitenge akadakia na kusema maneno haya ninayoyanukuu, "Aaaaaaagh achaneni nao hao watoto wadogo wanaoanza kazi leo sisi wenzao sasa treni ipo katika mwendo" hali iliyopelekea watangazaji wenzao wote waliopo sasa kipindini kumuiga Kitenge na sasa kila mara wanapiga tu vijembe na mlio na redio zenu kisikilizeni hicho kipindi msikie vijembe.
Hofu yangu
Kama hali hii haitadhibitiwa haraka na TCRA au na wamiliki wa hivi vyombo viwili vya redio kuna uwezekano hili bifu likazidi na pia likaathiri kabisa tasnia nzima ya uandishi wa habari hasa hii ya utangazaji kwani kiuhalisia wote wanaenda kinyume kabisa na ueledi wa masuala mazima ya utangazaji.
Hata hivyo niseme tu kwa E FM kuwa ni kweli wamekuja vizuri katika ushindani ila wakatae wakubali bado watabaki kuwa ni wachanga na wana mengi ya kujifunza kutoka kwa Clouds Fm na hili halina ubishi labda uwe ni popoma uliyetukuka, ila na nyie Clouds Fm msitumie ukongwe wenu katika kuwadharau au kuwadidimiza E FM kwani hata nyie pia naamini mna vitu vya kujifunza kama siyo kuiga kutoka kwao.
Binafsi nawapenda wote Clouds Fm na E FM ila mkiendelea na huu upopoma wenu wa kitaaluma mtanikosa kama msikilizaji wenu mkuu niliyetukuka wa michezo.
Acheni ushamba na utoto wenu huu jirekebisheni kukiwa bado mapema.