Clouds FM acheni Utoto



Mbona Mpaka Sasa Sijaona Taita Kusaga Na Mr. ARV Hando Wakijitokeza Kukanusha Hiki? au Mpaka Aseme Kitu GENTAMYCINE Tu?
 
Wanapeana kazi kwa kujuana,nina mashaka na elimu za watangazaji wake Nendeni Udsm,Udom na vyuo vingine kuna watu wanagraduate wenye degree za journalism acheni uzembe wa kuajili vilaza na wapenda rushwa wataiua clouds.


mi nafikiri unawaonea hao wafanyakazi wa clouds, vituko vyao hivyo hayo ni maagizo kutoka kwa maboss zao,kwa hiyo wa wakuwalaumu ni ruge na mwenzake
 

Nilitegemea ufanye utafiti kabla ya kitoa malalamiko! Kwenye mgogoro wa Clouds na Jide ..jide alisema hataki nyimbo zake zipigwe huko na hata kwenye mazishi yake wasiongelee wala Kuja!

Jide ndio aliye amua hiwe hivyo na aliwa tukana sana tena sana na hakutaka muafaka kabisa hadi sasa hivyo wana mgogoro hadi sasa!
Hivyo sitegemei kuisikia Sauti ya Jide Clouds Fm au TV kwanza muhusika ataki
 
Wanapeana kazi kwa kujuana,nina mashaka na elimu za watangazaji wake Nendeni Udsm,Udom na vyuo vingine kuna watu wanagraduate wenye degree za journalism acheni uzembe wa kuajili vilaza na wapenda rushwa wataiua clouds.
By the way hiyo ndio style yao ya maisha though walichotakiwa ni kutopiga nyimbo za Lady jaydee kwa kuwa mwenyewe alitaka iwe hivyo lakini kwa ambazo ameshirikishwa inakuwa unamuumiza yule mwenye nyimbo yake pamoja na wapenzi wa huyo msanii na wala hakomeshwi Lady Jaydee, kama taasisi inabidi waangalie kwenye hili vinginevyo leo utatamba ipo siku mambo yanageuka
 
Ukishirikishwa kwenye wimbo mwenye mali sio Jide bali yule mwenye wimbo hivyo kukata vipande vya Jide kwenye wimbo amba ameshirikishwa au ametajwa sio kumkomesha JD bali wengine kabisa, just imagine mpaka msikilizaji akihojiwa akionekana kumtaja JDkama ndio star wake unaona wanapeleka faster na kuhamisha agenda, kama taasisi kuna maeneo wanatakiwa waache kama yalivyo na kuacha ile hali tuliyonao sie mfano mie nikiwa na bifu na wewe. Kwenye kutokupiga nyimbo za JD wapo sahihi kabisa naungana mkono na wewe kabisa ila hayo mambo mengine ya kukata vipande vyake kwenye maeneo abayo aeshirikishwa ni kuwaumiza waliomshirikisha
 
wanadai sambaza upendo sasa sijui ni upendo wa aina gani kama wenyewe wanakuwa na bifu na baadhi ya watu tutasambaza vipi huo upendo
 
Ila haya ni mabifu ya kiutu uzima tofauti na hayo mengine yapo open sana kiasi kwamba kuyagundua inakuwa kazi kidogo, mie sio mzoefu sana wa kusikiliza radio ila kwa uzi huu ukiangalia comment utagundua kuna ambao wanawachukia kweli clouds bila sababu, kuna wanaowapenda clouds hata kama wamekosea wao wanaona kama wanaonewa alafu kuna kundi lingine wao wanaeleza maoni yao kutoka moyoni kabisa bila ushabiki. Kutopiga nyimbo wapo sahihi tatizo approach wanayotumia ku-deal na JD kidogo ina kushikeri ndio maana kuna watu wanaoiangalia kama taasisi kuna sehemu inatakiwa warekebishe. Wapo sahihi kutopiga nyimbo za JD kwa kuwa msanii ana mgogoro nao tayari na alitaka iwe hivyo lakini pia kupiga wimbo ambao ameshirikishwa JD na kukata kwa makusudi vipande vyake pale hawamtendei haki mwenye wimbo pia hawamkomeshi Jide zaidi ya kuwaumiza wasikilizaji (tatizo wasikilizaji wapo wa aina mbili kuna ambao msimamo wowote wa kituo utakaoonyeshwa wao wapo tayari kuufuata na hawa ndio watafurahia hii hali lakini wale wanaoipenda clouds kwa mazuri yake ikitokea kuna mapungufu wataumia)
 

Acha mbwembwe ndg kujifanya mwema wakati unawakandia. Ashatangaza vita na media na kutoa angalizo kuwa sauti yake isisikike kwenye media yao. Ninachofuata ni utekelezaji tu. Hata akisikika kwenye wimbo anakohoa wata-mute. Kampuni haiwezi kupelekeshwa na kinyamkela mmoja eti kisa wewe unampenda. Ukimtaka kasikilize media nyingine. Hao wasanii waliomshirikisha ashakorogana nao kitambo hivyo kusema clouds inawaharibia nyimbo walizomshirikisha jide kwa ku-mute sauti yake ni majungu yako.

Umewauliza wakakwambia hayo au ni hisia zako? Make me navyojua hata hao wasanii hawapendi kusikia sauti ya huyo kinyamkela kwenye nyimbo zao.
 
Hapo bold nakuomba kama Mtz mwenzangu badilika maana kwa tabia hii ikikomaa tutajenga taifa lenye hofu ya kuchangia mjadala kwa kuogopa kwenda kinyume na wengine. Sifa kuu ya binadamu ni kutofautiana kwa hoja na ndio maana kukawa na mikutano, bunge, vikao vya familia na mwisho majukwaa kama haya ili kila mmoja kwa mtazamo wake anatoa kile ambacho anadhani ni busara kwake alafu mwisho wa siku kunakuwa na consensus na ndio maana kwangu mie niliona wapo sawa kwa kutokupiga nyimbo zake (ukaitwa mbwembwe za kujifanya mwema) pia nikaona hawapo sahihi kutoka na piece of information niliyokuwa nayo (ukaniita kuponda japokuwa sio kuponda bali ni kuwa tofauti ya kimtazamo tu na kilichotakiwa ni kunieleza tu kama ulivyomalizia paragraph ya mwisho kwa kuniambia ningeuliza, na mtu wa kunipa info ni wewe kwa kuwa mie ni mchangiaji sio kwamba nimeleta uzi). Mie radio kwa ujumla wala mie kwenye radio utanikuta kwenye sports leo na wao saa 3 sports extra ambapo ni soka kwa kwenda mbele huko kwingine kwenye miziki sipo kabisa
 
Hakuna media yenye mizengwe kama hii hapa nchini.....

Waache mambo ya kihuni kwenye Professional businesses...

Hivi nani huwa anaisikiliza...? ?

kipindi cha Lisaa (59 Minutes) kuna matangazo dakika 22 (22 minutes):juggle::juggle::juggle::juggle:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…